Nimejitoa kwa mpenzi wangu nimegundua haya. Je, nifanyeje?

Kwani nyumba umemjengea? Kama ya kupanga kodi itaisha tu achana nao. We deal na mtoto wako tafuta manzi mwingine songa mbele. Akili itamkaa sawa siku moja.
 
Ila kuna watu mazwzwa sana daaaaah,

Yaani unamwendekeza mpumbavu mmoja tena na tabia zake unazijua hivyo,

Kaa nae mbali mpuuzi wewee

Acha nikufokee tu Kmmkqee
 
Mtoto tayari niko nae,aliniachia kwa hasira kwenye mkesha wa Christmas nikiwa Dar Nikaamua kumchukua next morning nikaja nae Arusha! Namfanyia utaratibu aingie Shule huku huku wiki hii!
Piga chini huyo kicheche siku utakuja kupigwa bisu la tumbo usije kusema sijakwambia.
 
Tatizo ameshakuona wewe kilaza chochote atachofanya utarudi tu kumbembeleza na kulia lia kuomba msamaha kua mwanaume acha uboya. Mimi mwanamke nikijua ana mwanaume mwingine hapo tunakua tumemaliza sasa wewe ulijua ana mwanaume mwingine bado ukajirudisha kuomba msamaha chukua mtoto peleka kwa mama yako mtafute dada wa kumsaidia kazi achana na hiyo takataka.
 
Tatzo wa kariba hyo weng wanakuaga wafup.weusi halaf sura personal(natania)..au ana kibamia.na hela hana..yaan lazima ana kitu personal...mwanaume aliekamilika anaejiamin hawez yumbishwa namna hyo..

Kama hana mwonekano basi atafute pesa maana anatuaibisha
Kwa kweli coz hajiamini.
 
Hey Bro , unajuwa maana ya kuitwa mwanaume? kabla ya uwepo wake yeye ulikuwa unaishi vp?
Je huwezi kumlea mtoto wako mwenyewe then ukasahau kila kitu ?
Wewe n mwanaume na sio wakiume
Nafikiri umenielewa hapo
 
Mkuu Hakuna haja ya ambush maana utazidi Kuumia tu. Kikubwa umesema Mtoto unaye hapo hilo ni bora zaidi,
Ushauri ni hivi wacha hiyo kodi iishe na usije ukalipa tena.
Halafu pia punguza kiherehere cha kupenda sana.
Kila la Heri mkuu
Aisee nishasahau kupenda kabisa..naishi tu Kwa kuwaongepea..
 
Mkuu kwanza unamoyo wakiume Sana ingekuwa Mimi nishawatoa
Yani kawatoe funga mlango wakaanze kwao cyo hapo nenda kawatoe Tena fanya haraka daaaah?
 
Nimekuwa Kwenye Mahusiano Na Huyu Binti Kwa Miaka 6 sasa! tumebahatika kupata Mtoto mmoja! ila hatujaoana. Kwa Sasa Yeye anaishi Dar Mimi niko kikazi Mikoa ya kaskazini! Mwanzo Nilianza Kufuata Taratibu za kumuoa nikatoa mpaka posa kwao tatizo likaja kwenye kikwazo cha dini! ikabidi tuweke pozi kwanza tufanye maisha mengine.

Kwenye Process za kupambana na Maisha Kuna Wakati tulitofautiana ikafanya akapata nafasi akawa anadate na mshkaji flani mfanyabiashara wa maeneo flani around Sinza Hapo.

Niliumia ila kwa ajili nampenda sana na sikutaka mustakabali wa maisha yetu,mahusiano na malezi ya mtoto yawe magumu niliamua kujishusha nikamwomba msamaha na kumwahidi kumpangia sehemu nzuri na kumnunulia vitu vyote vya muhimu kwa ajili ya Maisha. Kipindi Hiki hakua na kazi so ilibidi nimchukue mtoto kumleta Dar akaja kukaa nae huku mimi nikijitahidi kila wiki kuja Dar kwa ajili yao.

Maisha Yetu Yalirudi Kawaida yakawa Poa na Hata mawasiliano na yule mshkaji niliona yamepungua Kabisa Though Jamaa Nilikamata Mara Kadhaa Txt Zake Akiwa Anamsumbua warudiane akimshawishi kwa kumtumia hela alivyoweza .Lakini Mara Zote alikuwa akinionyesha hata the way alikua anamkataa jamaa nikazidi kumuamini.

Nikajua Sasa ni kufanya Maisha na kujipanga kwa ajili ya future yetu,nikaanza kuhangaika kumtafutia kazi ili tu asije pata vishawishi huku nikiendelea kumtunza yeye na mtoto kwa kadiri nilivyoweza.

Ilikua niko tayari kubaki hata na njaa ila nitimize mahitaji yao,Hata nikiwa na elfu 20 nitatuma 19 nabaki na elfu moja ilimradi niipambanie familia yangu. Nakatiza mwaka mzima sibadili nguo mpya wala viatu ilimradi familia iwe sawa. Nagombana na mwenye nyumba wangu nalimbikiza madeni ya kodi Lakini sikutaka kabisa nimpe stress za pango. Nimejikuta kwenye matatizo mengi lakini sikutaka kabisa yaniondoe kwenye Reli ya kumpambania yeye na mtoto.

Nikaachana na wanawake,nikapambana usiku na mchana,nafanya kazi ofisi 'A' Mchana usiku naingia office 'B' Nikaanzisha my side bussiness,Nasafiri usiku na mchana kwa ajili ya biashara zangu Yote kwa ajili ya kuhakikisha tunakua sawa.

Nikampangishia nyumba maeneo ya Sinza,baadae nimemhamisha kwenda kwenye nyumba kubwa zaidi maeneo ya Mbezi!
Hivi Karibuni kulitokea mgongano kati yetu uliofanya tujipe space kwa mda kwa ajili ya kujitathmini. Ila Nimekuja Kugundua Mwenzangu anatumia nafasi hio kunicheat Na amerudiana na mshkaji yule wa mwanzo na mara nyingi anaenda pale nyumbani!

Nimejaribu kuongea nae ila amenionyesha kama vile ndio maisha aliyoamua na hajali chochote nitakachoamua! Tumegombana Sana kabla ya mkesha wa christmas akawa ananijibu alivyojisikia akafikia hatua akanitukana tusi moja lisilovumilika nikamchapa vibao kama vitatu Vikamuachia Alama Za kutosha.

Niliumia Kwa Kufanya Vile Na Asubuhi iliyofuata Nilimwomba mshamaha sana na kuonyesha nimejutia kile kitendo kwa,Sikutaka kabisa kwenye maisha yangu to put hand on my woman!.Sipendi Kumuumiza cz najua akiumia mi naumia zaidi.Akatumia kile kigezo kupata nguvu ya kuamua anachotaka! akaanza kuwasiliana na jamaa kwa nguvu zote ikabidi nimyangany'e simu kwanza!

Usiku wa siku hiyo akaniambia anaondoka anaenda kwao,nikamuuliza vipi kuhusu mtoto akanijibu ''Kwani Umenikuta Na Mtoto??'' Akaniambia nimpe simu yangu ya kitochi kama sitaki Kumpa smartphone yake! nikampatia,Akaondoka kwa hasira nikamfuata nyuma nikiwa na boxer tu mpaka nje nikamkuta anapiga simu nikamnyang'anya Kuangalia anampigia nani nikakuta ni namba za yule jamaa!

Nikarudi nyumbani nikamuacha aende nikafika nikamuandaa mwanangu kwa ajili ya kuondoka sababu sikua na cha kufanya zaidi na nisingeweza kumuacha! Asubuhi nikaondoka Siku Ya chirstmas nikaondoka nae kurudi Arusha! nikampigia simu mama kumjulisha mjukuu wake anakuja kumsalimia.

Tukawa Tumerudi Na Mwanangu na kumuacha. Nikachunguza Kimya Kimya Nikagundua wameanza tena mahusiano na mshkaji na kuna siku nilikuja bila yeye kujua mpaka Dar nikalihakikisha hilo! nikaondoka Nikiumia Machozi Yakinitoka Bila Kumwambia Chochote! Nikakaa Nalo moyoni mpaka jana namuulizia kuhusu uwezekano wa kupata cheti cha mtoto kwa ajili ya taratibu za shule!

Nikamwambia nitakuja Dar kukichukua akaniambia Akanipa Onyo Nisifike sehemu anakaa! Nikamwambia Hicho anachokificha mimi nakijua though sijawahi muambia! akapanik akanijibu ''Ndio Kiko Hivyo Unavyojua... Usinisumbue,Sitaki Kuchanganywa akili It Doesn't Matter Anaenda Pale or Not Hainihusu!! Akaniblock.

Na Kinachonniumiza zaidi kuna wakati wakiwa kwenye mahusiano na huyu mshkaji alikua hataki hata nijue anapokaa kwa kusema sio heshima mimi kufika sehemu aliyopangishiwa na mwanaume mwingine.Akaniambia nifanye mpango tu wa kumhamisha ili tuwe huru ila sio mimi kwenda Pale.

Sasa Nawaza kama Aliweza Kufanya Vile Kwangu Wakati Ule,Kwanini ameweza kumruhusu mtu yule,yule alienizuia mimi kujua/kwenda wanapokaa Leo ndio anaenda mimi nilipompangishia tena bila aibu huku akijua kabisa kwamba mpaka tunahamia pale majirani walituona tukiwa nae na mtoto wetu tumeishi kwa mda kabla ya kutokea misunderstanding.

Nampenda,Nimelia,Nimeumia Mpaka Mda Huu ameniblock! nawaza alikua ananitumia kama daraja au ndio hali ya kuyumba kidogo kiuchumi imesababisha yote haya! Nikimuuliza ananiambia nimuache afanye maisha kwanza tutayejenga mbeleni!. Sasa niko Njia Panda,nimeongea nimefika mwisho.

Hapa Nilipo Nawaza nikafanye ambush la kushtukiza usiku nikipate ushahidi niwaondoe wote nifunge nyumba wakafanye Maisha yao sehemu nyingine! Au nikaushe niamue kumuachia Mungu! Naombeni Ushauri!
You may be aged, but not matured.

Maturity is knowing that you are responsible for your own happiness.

God forbid, this will never happen to me. Wakuskia na msikie.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom