Nimejikuta uzalendo na nchi yangu Tanzania umepotea, nimepata uzalendo wa nchi ya China

Mwenye akili ataona hapa kuna shida kubwa sana!!

Kwahiyo uko tayari kuwa jasusi la china hapa tanzania?

Mtu kama wewe ukipata kazi BoT alafu china wakakufwata uwape data utakataa kweli?

Sikulaumu wewe mkuu, ila kuna kitu hakiko sawa kwenye hii nchi!!
Sina uzalendo tena!
Yan wanirushie mpunga kidogo tu !
Kila data nawapa!
 
Hata Tanzania kuna baadhi ya maeneo watu ni wakarimu sana, kuna baadhi ya maeneo watu ni watukutu...

Tembelea Beijing, uone wachina walivyo wabaguzi na dharau... wanabaguana mpaka wenyewe kwa wenyewe...

Unless wajue wewe ni Diplomat ndiyo watajishaua shaua...


cc: mahondaw
Beijing sikukaa sana ndio maana!
Ila Shanghai pako safi sana
 
wachina tuko nao Kariakoo hapa wanauza mpaka pipi na mahindi ya kuchoma...hawataki kurudi kwao.....subiri upazoee ujue na lugha yao uone walivyo wabaguzi ...
 
Naipenda Tanzania,Naipenda nchi yangu hakika nitarudi na kuishi Tanzania ,nitarudi kuijenga nchi yangu, hiyo ndo zawadi nilipewa na Mungu.Wakati mwingine nasikiliza wimbo wa Tanzania Tanzania,Wimbo wa Taifa, najisikia kuwa nyumbani,wakati mwingine ukiangalia taarifa kwenye vyombo vya habari,utasikia habari za kukatisha tamaa lakini hiyo hainibadilishi mimi kuwa mtanzania.
Hao Shanghai wamefika hapo walipo na ustaarabu huo walio nao kwa sababu kuna watu walipigana,walijitolea kufikia hiyo hatua,una nafasi ya kufanya kitu kwa ajili ya nchi yako.
Mungu ibariki Tanzania
 
Mwenye akili ataona hapa kuna shida kubwa sana!!

Kwahiyo uko tayari kuwa jasusi la china hapa tanzania?

Mtu kama wewe ukipata kazi BoT alafu china wakakufwata uwape data utakataa kweli?

Sikulaumu wewe mkuu, ila kuna kitu hakiko sawa kwenye hii nchi!!
hiyo sentensi yako ya mwisho ndio point ya msingi sasa
 
Kupenda sikizote Ni moyo .moyo ndio unaamua upende wapi.
Miaka kama miwili nimejikuta kuichukia sana Tanzania sijui kama tatizo Ni LA nchi au nilangu binafsi hilo bado natafakari mpaka Leo!
Nimejikuta natamani kuishi CHINA na kuwa Mmoja wa raia wa nchi ile kutokana na Maisha niliyoishi Kwa muda mfupi katika nchi ile.

Ubora wa hali yakimaisha.ukarimu wa watu wa Shanghai umenifanya nipoteze tumaini na nchi Yangu nimekuwa nikitamani nife Kwa ajili ya nchi ya CHINA hata kama wakiihitaji nikatumikie military army Niko tayar pia.
Kiukweli siko tayari kufa Kwa ajili ya Tanzania kutokana na kutoona ubora wowote wa nchi hii.
Niko tayari kufa Kwa ajili ya CHINA at all means!
Niko tayari kuwa Afisa usalama wa nchi ya CHINA na kulitumikia taifa hilo Kwa maslah ya nchi ya CHINA.

Maisha ya watu wa Shanghai yamenifundisha how to live a life !
Kwa kweli ukarimu wa watu wa China sijawah kuona sehemu nyingine nyingine yoyote dunia! Labda Ni kwasababu sijatembea dunia nzima!! Nimependa kuishi Shanghai kutoka na kuonekana Ni Mmoja wa watu wa sehemu ile licha ya kuwa Ni mwafrica.

Sitasahau siku moja nilitoka mwenyewe kwenda pembeni ya eneo nililokuwa kupata chochote Ni mbali kidogo maana hapo karibu chakula kinachopatika sio kizuri kwetu waafrika .
Nilipofika nikaagiza nikipendacho wakati nasubiri order akasogea Dada Mmoja wa kichina akaniuliza kwanini Niko mwenyewe Kwa lugha ya kiingereza .nikamwambia wenzangu wanakuja akafurah sana .
Basi akaniletea kitu kama laptop hivi ila kimekuwa programmed katika lugha ya kichina akaniambia wakati nawasubiri wenzangu niangalie movie za magharibi ila
Nikitaka kuondoka nimstue kama atasahau!
Niliwaza sana ingekuwa kwetu bongo ingekuwaje?


Kiukweli the life of Shanghai is very amazing!
Kwa kweli mnaoishi south Africa mnamoyo sana pale siwezi kuishi hata Kwa mtutu wa bunduki.


Nahisi ndio maana hata wao China wamebarikiwa kiuchumi kutokana na baraka zinazoachwa na wageni.

Sijajua kwa mliotembelea nchi zingine ila Mi nimezurura kidogo ila kwa CHINA nimependa kuishi asilimia 100.
I will back in Shanghai for sure!

GOD BLESS CHINA
Ningekuona wa maana kama ungekuwa na uzalendo na Somalia.
 
Uzalendo umebakia midomoni tu lakini moyoni hakuna kitu chochote.

Siyo kwako tu hata viongozi wetu Wa juu hawana uzalendo.
 
Tusijekufika walipo Ethiopia, tunaambiwa uchumi wa nchi unakuwa huku raia wake hasa vijana wanaikimbia nchi kila uchao...
 
Siwezi kukulaumu.

Kuna binamu yangu mmoja nilikuwa naongea naye wikiendi hii. Baba yake mtu mmoja ana cheo kikubwa serikalini.

Nikawa namuuliza, hivi imekuwaje Tanzania haijawakilishwa Davos?

Akaniambia binamu, mi naishi zangu huku ughaibuni, naangalia maisha yangu, mke wangu na mwanangu. Siasa za Tanzania hata sina interest nazo. Wewe ishi zako huko uliko habari za Tanzania achana nazo.

Nikasema mimi nilikuwa nafikiri sina interest sana, lakini huyu zaidi.
 
Back
Top Bottom