Nimejikuta uzalendo na nchi yangu Tanzania umepotea, nimepata uzalendo wa nchi ya China

Veyron

JF-Expert Member
Feb 6, 2012
550
500
Kupenda sikizote Ni moyo .moyo ndio unaamua upende wapi.
Miaka kama miwili nimejikuta kuichukia sana Tanzania sijui kama tatizo Ni LA nchi au nilangu binafsi hilo bado natafakari mpaka Leo!
Nimejikuta natamani kuishi CHINA na kuwa Mmoja wa raia wa nchi ile kutokana na Maisha niliyoishi Kwa muda mfupi katika nchi ile.

Ubora wa hali yakimaisha.ukarimu wa watu wa Shanghai umenifanya nipoteze tumaini na nchi Yangu nimekuwa nikitamani nife Kwa ajili ya nchi ya CHINA hata kama wakiihitaji nikatumikie military army Niko tayar pia.
Kiukweli siko tayari kufa Kwa ajili ya Tanzania kutokana na kutoona ubora wowote wa nchi hii.
Niko tayari kufa Kwa ajili ya CHINA at all means!
Niko tayari kuwa Afisa usalama wa nchi ya CHINA na kulitumikia taifa hilo Kwa maslah ya nchi ya CHINA.

Maisha ya watu wa Shanghai yamenifundisha how to live a life !
Kwa kweli ukarimu wa watu wa China sijawah kuona sehemu nyingine nyingine yoyote dunia! Labda Ni kwasababu sijatembea dunia nzima!! Nimependa kuishi Shanghai kutoka na kuonekana Ni Mmoja wa watu wa sehemu ile licha ya kuwa Ni mwafrica.

Sitasahau siku moja nilitoka mwenyewe kwenda pembeni ya eneo nililokuwa kupata chochote Ni mbali kidogo maana hapo karibu chakula kinachopatika sio kizuri kwetu waafrika .
Nilipofika nikaagiza nikipendacho wakati nasubiri order akasogea Dada Mmoja wa kichina akaniuliza kwanini Niko mwenyewe Kwa lugha ya kiingereza .nikamwambia wenzangu wanakuja akafurah sana .
Basi akaniletea kitu kama laptop hivi ila kimekuwa programmed katika lugha ya kichina akaniambia wakati nawasubiri wenzangu niangalie movie za magharibi ila
Nikitaka kuondoka nimstue kama atasahau!
Niliwaza sana ingekuwa kwetu bongo ingekuwaje?


Kiukweli the life of Shanghai is very amazing!
Kwa kweli mnaoishi south Africa mnamoyo sana pale siwezi kuishi hata Kwa mtutu wa bunduki.


Nahisi ndio maana hata wao China wamebarikiwa kiuchumi kutokana na baraka zinazoachwa na wageni.

Sijajua kwa mliotembelea nchi zingine ila Mi nimezurura kidogo ila kwa CHINA nimependa kuishi asilimia 100.
I will back in Shanghai for sure!

GOD BLESS CHINA
 

McMahoon

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
1,189
2,000
Kwa sifa ulizo zitoa kwa China, hata ukipata bwana wa kichina utakubali kuolewa wallah....
Uzalendo ni matokeo ya upendo juu ya nchi yako. Je, upendo hutokana na nini?
Baba anayekupiga kila siku unaweza kumpenda? Acheni ush...ga kwenye mambo ya msingi
 

Veyron

JF-Expert Member
Feb 6, 2012
550
500
Hamtaki kujenga nchi yenu mnakimbilia kwa walio mwanga jasho lao kujenga nchi zao shitthole wew
Wanaotakiwa kutengeneza mazingira rafiki kumwaga jasho ili tufanikiwe ndio hao wanaotengeneza mazingira mabaya kwenye upande wa umwagaji wa jasho.
Sina maana mbaya ila mioyo huongea ukweli !
Kule Shanghai utawala umeweza kutengeneza policy zenye tija kwa wananchi .
Utajikuta as the days go unakuwa motivated to do better than !
Anyway Ni mawazo yako tu! Ila jaribu kuangalia vitu kwa undani utaelewa!
 

Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
41,746
2,000
Hata Tanzania kuna baadhi ya maeneo watu ni wakarimu sana, kuna baadhi ya maeneo watu ni watukutu...

Tembelea Beijing, uone wachina walivyo wabaguzi na dharau... wanabaguana mpaka wenyewe kwa wenyewe...

Unless wajue wewe ni Diplomat ndiyo watajishaua shaua...


cc: mahondaw
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom