Boflo
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 4,384
- 4,409
Wana JF Huyu Mdada an serious problem.....mnaweza kumsaidiaje?
Habari zenu
Mimi nina miaka 31, na mwaka 2000 baada ya kutoka tanzania na ngozi yangu asili (originol) ambayo ilikuwa ni nyeusi na ya kun'gaa, marafiki zangu hapa texas, walinishawishi niwe mweupe ili nami ning'ae. basi nikapata vidonge vya kungarisha mwili, yaani kuwa mweupe.
Na kusema kweli, nilibadilika ngozi, nikawa mweupe sana, na siyo rahisi mtu kujua kama kweli nimetumia madawa, isipokuwa walionifahamu tangu utotoni ndio wanaoshangaa uweupe huu nimeutoa wapi.
Sasa nilipataga mimba, ambayo ilikuja kutoka, ila sikujua tatizo ni nini. Hapa majuzi tena, nikashika mimba ya pili bahati mbaya mtoto kafa (yaani mimba imeharibika) nilienda kwa dakitari kutaka kujua tatito liko wapi, hapo ndo nikaambiwa kwamba kuna chemicals kwenye mwili wangu ambazo ndio chanzo cha watoto wangu kufa.
Nimeambiwa kwamba hayo madini ni mengi mno, na nisipoangalia nitakufa na cancer ambayo inaweza kuanza muda wowote. suluhisho linaweza kupatikana nikisafisha damu, na uwezo huo sina, au kama naweza kurudisha ngozi yangu ya zamani kwa sababu sasa hivi ngozi yangu haina kinga tena.
Sisikitikii weupe, kwa maana nikitu ambacho nilikitamani sana, kwa hiyo mzigo lazima niubebe, ombi langu ni ushauri wa kuweza kutoa hizi kemikali mwilini mwangu.kama ni kufa basi tena. cha ajabu ni kwamba mchumba wangu ametishia kuniacha kwani siwezi kuzaa tena. yaani sasa hivi analala nje full, naumia lakini sina jinsi..... naombeni ushauri wenu, niko njia panda
mdau, texas usa