Nimeitwa Shetani baada ya kutoa ushauri ambao nimeombwa. Nikirudishia haya matusi najua tu itakuwa issue kwa ndugu

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,471
23,744
Mijitu mingine sijui ikoje....hovyo sana. Mtu anakuomba ushauri halafu kumbe tayari ana maamuzi yake kichwani. Unataabika kufikiri unampa ushauri anaanza kuongea shit tena.

Mijitu kama hii ngekuwa na uwezo ngekuwa naiponda tu na nyundo ya kupondea kokoto kichwani.

Mjomba wangu ana kansa inamsumbua muda sasa. Na ukimcheki umri wake nao ushakuwa usiku sana tu miaka ya late 70. Si umri mdogo. Kansa inamsumbua sana na kiukweli ashaambiwa kwa hatua yake utokee muujiza tu.

Kimeitishwa kikao leo tumeongea ndugu n.k kuwa tuchangishane kila mtu pesa isiyopungua Mil moja.sawa mi nimekubali. But pia watoto wake wanataka uza nyumba na some stuff (mali) kaja mama mdogo ananiuliza sasa hili suala la ugonjwa litakuaje.

Mimi nlishawahi sema ugonjwa mwingine watu msilazimishe mtu aishi. Mnamchosha tu mtu mwenyewe ashakula chumvi sana tu.mwacheni ende. Mnamlazimisha kuishi mtu ana kansa, ana BP mnataka aishi kufanya nini?

Sasa nikasema tunaweza changa hizo pesa akaenda India akadanja na hapo nyumba pia imeuzwa n.k hamuoni ni hasara? Wakati tu tungemwacha hapa na kumpeleka kwenye maombi? Sasa naye hataki maombi. Anataka aendelee kunywa mkojo wa shetani(pombe) so anapinga kabisa hbr za maombi.

Basi angekuwa anapinga maombi na kuendelea kupata kinywaji chake huku anasubiri kudanja. Unakuta mbishi. Hataki. Anataka apelekwe India. Sasa nawaza huyu India akafanye nini? Why anang'ang'ania kuishi wakati hana issue yoyote ya maana hapa duniani?

Mtu anatolewa ndani sometimes anaanikwa nje, halafu ana anuliwa kurudishwa ndani. Meno mengi keshapoteza age imeenda. Imekuwa usiku ila mbishi. Sasa nawaza hata akipona lengo lake la kuishi ni nini? Huyu mzee ni kama mchawi tu.

Mimi nimeshauri afanyiwe tu maombi hapa hapa bongo. Mali zisiuzwe ana watoto watano. Wabakize mali ziwasaidie. Hao wawili wa mwishoni wadogo kabisa hawajafika hata miaka 20 wapewe mali kuliko kumtibia mzee ambaye bado anaweza danja wakapoteza mali na mzee mwenyewe. Si bora wabaki na mali?

Mama mdogo anasema nina roho ya kishetani. Sasa nashangaa why alitaka ushauri kwangu? Lakini kibaya nilichosema hapo ni kipi?

Kuharibiana siku tu kwa mambo ya hovyo hovyo. Nirudi zangu tu home nikalale.
 
😂 in other side huo ndio uhalisia wa mambo, lkn upande mwingine piah, mkuu una roho ya kibabe sana ✊😂😂😂shout out to you Joh... 😆 naomba Mungu anipe moyo kama huo kwenye kutafuta pesa lakini... 😄😄😄🙌
 
Mijitu mingine sijui ikoje....hovyo sana. Mtu anakuomba ushauri halafu kumbe tayari ana maamuzi yake kichwani. Unataabika kufikiri unampa ushauri anaanza kuongea shit tena...
eti roho yaki shetani..
 
Binafsi naona ushauri wako ni sahihi zaidi. Japo ni mchungu kwa mpokeaji.
 
Kwani hamkuwai kutumia mali zake pindi ana nguvu zake.

Waambie madogo marehemu hufa na chake...wapambane watafute chao.
 
Mkuu kwani ukifika 70 ndo unakaribia kufa?? Mbona watu wanafika mpaka 100....
Issue sio kufika 100 je utakua productive katika huo umri kiasi cha kuteketeza urithi wa watoto wake.
 
Yeye nyumba hakuirithi. Hivyo hata akifanayo watoto watajenga zao. Tatizo ni pale nyumba inauzwa anaenda India na anapona. Sijui anakuja kuishi vipi. Maana nguvu hana na Mali ishauzwa
 
Kwa upande mmoja uko sahihi lakini haina maana kuwa mtu akishafikisha miaka 70 atafariki, kifo ni juu ya Mungu huwezi jua Mungu amempangia kuishi miaka mingapi angekubali kwenda kwenye maombi na kuwa na imani ingesaidia zaidi maana lisilowezekana kwa wanadamu kwa Mungu linawezekana.
 
Back
Top Bottom