Nimeishi ughaibuni (Ireland) miaka 10, nikachuma pesa huko nikarudi kuwekeza nyumbani Tanzania

Per Week

Member
Jul 19, 2018
92
232
Mimi ni mmoja watu ninaoamini hapa duniani hakuna nchi nzuri Kama Ireland(republic of Ireland), hii nchi ni nzuri Sana sijawahi kuona.

Nilienda Ireland kwenye masomo(baada ya kupata scholarship).

Nilipomaliza tu form 6 mwezi February 2008 nikaanza kufanya mishe za kutafuta scholarship, na hatimaye matokeo yalipotoka mwezi wa 5 nilipata bahati ya kwenda Ireland kimasomo na hakika nilitumia vyema nafasi hiyo. Matokeo ya advance yalinibeba.
Nilienda kusoma Agricultural Science

Baada ya kumaliza masomo niliingia mtaani, nilikuwa nishajiandaa nikimaliza nibaki huko hivyo kila kitu nilikuwa nimekiweka sawa.

Kutoka Knyama hadi Ireland haikuwa ngumu kwangu kutoboa kwani nilikuwa nafanya Sana kazi za hapa na pale.

Baada ya miaka 7 niliona matunda ya Kazi zangu, na hivyo hatimaye kurejea nyumbani mwanzoni mwa mwaka 2018. Nikiwa na uhakika wa $350,000 bank.

Huku TZ nilipata kazi kwenye taasisi fulani hivi kubwa, lakini sikuwa na malengo Sana ya kufanya kazi ya kuajiriwa ikiwa tayari nina capital ya kutosha Sana.

Baada ya muda nikiwa kwenye hii taasisi nikaona ni vyema Sasa nikafikiria kuoa, niliwahi pia kuja kuweka tangazo huku jf lakini nasikitika sikupata Mtu sahihi, sikupendezwa nao karibu wote walionitafuta.

Nilifanya kazi kwenye hii kampuni kwa mwaka mmoja nika-resign, na hivyo nikaendelea kuwekeza kwenye kilimo na Sasa ni mmoja wa watu wanaofanya vizuri Sana kwenye kilimo Cha zabibu. Nimeweka mtaji mkubwa kwenye kilimo hiki na faida inaonekana Sana.

Nilichogundua kule ni kwenda kuchuma alafu unarudi bongo kuwekeza, itakulipa Sana.

Assume unarudi na kama million 800, alafu unatumia mil 100 kuwekeza kwenye kilimo, hapo utasahau maisha yote ya Dublin.
Siku moja nitarudi Dublin kutembea na sio kuishi, maisha ni ghali sana ya wenzetu. Kama yangekuwa sio ghali ningerudi bongo na pesa nyingi zaidi. Ila pia inategemea na wewe utaamua kuishi vipi.

Wito kwa watanzania wenzangu mnapoenda kuchuma huko Europe nawaomba mrudi Bongo kuwekeza, miaka 10 inatosha Sana
 
IMG_3950.png

kwenye uzi wako huu mwingine unasema
1. Una degree ya uhasibu
2. Umeajiriwa kwenye taasisi wa kimataifa

halafu uzi wako wa leo unasema
1. Umesomea agricultural science
2. Ulifanya kazi kwenye kampuni

Hizo chai za JF za moto sana
 
Back
Top Bottom