johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,897
- 141,832
- Thread starter
- #81
Mkuu jambo la heri halina msimu wa uchaguzi!Ni sawa....lakini!
Ukiangalia kwa undani na objectively, unaona kuna unafiki unafanyika au ni siasa za kilaghai tu. Nitafafanua.
Kodi inatozwa kwa kufauata sheria za kodi. Baada ya mwanzo Rais kutoa maelekezo, waziri alipeleka mapendekezo ya kubadilisha sheria za kodi. Kabla ya mapendekezo (mswada) ya kupelekwa bungeni, yanapita kwanza kwenye baraza la mawaziri (BLM) ambalo mwenyekiti wake sote tunamjua. Baada ya BLM mswada wa sheria unapelekwa bungeni. Baada ya mswada kupitishwa na bunge hauwezi kuwa sheria mpaka Rais akubali (accent). Kwa hivyo inashangaza sana (kama sio dharau kwa wananchi) mtu ambaye amehusika moja kwa moja na uwepo wa sheria hiyo (mbovu??) akiwa wa mwanzo kuilalamikia. Hakujua alichosaini? Ni wazi alijua kila kitu.
Tunaweza kuwalaumu TRA katika hili lakini kwa hakika anayepaswa kubeba hilo zigo la sheria mbovu ni waziri wa fedha, Bunge letu na zaidi Rais (kama kweli tunataka kuwa fair na objective). Maana kama Rais aliletewa sheria ambayo inaenda tofauti na maelekezo yake alikuwa na uwezo wa kuizuia ndani ya BLM kabla hata muswada haujaenda bungeni. Au la kapitiwa katika stage hivyo, angeweza kukataa kusaini. Mind you imeshapita karibia miezi 18 sasa tangia mabadiliko yafanyike.
Najua uchaguzi wa serikali za mitaa unakaribia kwa hivyo, kwa sisi wengine wenye makengeza sio vigumu sana kuona sababu ya hizi sarakasi zinazoendelea. Wengine mnayo haki ya kuoiga makofi na vigeregere.