Nimeipenda hii gari aina ya bajaji qute; nitaipataje, kwa bei gani na ubora wake ukoje?

kimpango

JF-Expert Member
Apr 24, 2011
600
716
Nikiwa katika pitapita za miangaiko ya asubuhi maeneo ya ubungo mataa nilimwona mwanamama moja akiwa amerelax akiendesha gari dogo sana nilipolisoma ni aina ya bajaji qute, kweli nikiri sijawahi kumuona mtu mwenye gari kama hili inawezekana huyu mama ni wa kwanza, nilisogea nimuulize maswali kadhaa kuhusu gari bahati mbaya muda huo huo trafki akaruhusu foleni ,sasa wadau ikiwemo walio karibu na huyo mama mniambie;

1. Hii gari/quadricycle hapa bongo nai[pata wapi?

2.Bei yake kuagiza ni sh ngapi nimeona zinatengenezwa india

3.Je ubora wake ukoje

Hayo tu nimefikiria katafaa familia yangu kwa shughuli za hapa Dar na hali ya uchumi
NAWASILISHA.

bajaj qute.jpg

bajaji qute.jpg

bajaj qute..jpg
5.jpg
 
Attachments

  • bajaji qute.png
    bajaji qute.png
    61.8 KB · Views: 181
  • 6.jpg
    6.jpg
    97.3 KB · Views: 159
nikiwa katika pitapita za miangaiko ya asubuhi maeneo ya ubungo mataa nilimwona mwanamama moja akiwa amerelax akiendesha gari dogo sana nilipolisoma ni aina ya bajaji qute,kweli nikiri sijawai kumuona mtu mwenye gari kama hili inawezekana huyu mama ni wa kwanza ,nilisogea nimuulize maswali kadhaa kuhusu gari bahati mbaya muda huo huo trafki akaruhusu foleni ,sasa wadau ikiwemo walio karibu na huyo mama mniambie
1. Hii gari/quadricycle hapa bongo nai[pata wapi/
2.bei yake kuagiza ni sh ngapi nimeona zinatengenezwa india
3.je ubra wake ukoje
hayo tu nimefikiria katafaa familia yangu kwa shughuli za hapa dar na hali ya uchumi
NAWASILISHA
Sikushauri kabisa.. Bei yake haina tofauti na carina Ti used
 
lakini uchumi mbovu hii gari wenzetu hawaangalii hayo swala inakufikisha kwenye mihangaiko kwa haraka kuliko daladala,ulaji wa mafuta mdogo,easy to park popote ,service yake kama bajaj ..ila niambie hapa dar naipata wapi
Nenda TFL pale Msasani/Mikocheni uwa wanazo, mara nyingi nazikuta pale
 
Nilimnunulia Nuru mwaka jana kwa milioni tisa hela ya kitanzani ila saizi ameishaipaki ni vibovu kichizi.
 
Nilimnunulia Nuru mwaka jana kwa milioni tisa hela ya kitanzani ila saizi ameishaipaki ni vibovu kichizi.
haiwezekani hii ni gari bro sio toy ok tumeshajua ulitaka kusema mwaka jana ulikuwa na milioni tisa ukatoa kununua toy usawa huuuu du?
 
nikiwa katika pitapita za miangaiko ya asubuhi maeneo ya ubungo mataa nilimwona mwanamama moja akiwa amerelax akiendesha gari dogo sana nilipolisoma ni aina ya bajaji qute,kweli nikiri sijawai kumuona mtu mwenye gari kama hili inawezekana huyu mama ni wa kwanza ,nilisogea nimuulize maswali kadhaa kuhusu gari bahati mbaya muda huo huo trafki akaruhusu foleni ,sasa wadau ikiwemo walio karibu na huyo mama mniambie
1. Hii gari/quadricycle hapa bongo nai[pata wapi/
2.bei yake kuagiza ni sh ngapi nimeona zinatengenezwa india
3.je ubra wake ukoje
hayo tu nimefikiria katafaa familia yangu kwa shughuli za hapa dar na hali ya uchumi
NAWASILISHA
Hivi vidanga navikubali sana asee
Kama hizi.
 
Attachments

  • 4C8BAA9A-4A45-4516-93EB-908A0C6826DC.jpeg
    4C8BAA9A-4A45-4516-93EB-908A0C6826DC.jpeg
    21.4 KB · Views: 137
haiwezekani hii ni gari bro sio toy ok tumeshajua ulitaka kusema mwaka jana ulikuwa na milioni tisa ukatoa kununua toy usawa huuuu du?
Mkuu we fuata kitu roho inapenda.
Ukitaka kuishi kwa kufuata watu wanasema nini huwezi kufanikiwa maishani. Unakuta mtu hana hata gari daily yuko kwenye daladala full kubanana we uko na ki baby walker chako wala music na ac juu huna habari lakini anakucheka.
Sasa si kila mtu anaishi kadri ya uwezo wa mfuko wake unataka mtu amiliki gari asiloweza kulihudumia wese mwisho wa siku analitumia weekend tu siku nyingine zote anapanda daladala ukimuuliza anadai acha lile gari linabugia mafuta hatari.
Hata bakhresa huenda wakati anauza mandazi aliambiwa ni biashara za akina mama awaachie akina mama
 
Kama hivi vya kubebea abiria wanauza vipya kuanzia milion 4. Yawezekana hako wakauza hata milioni saba fedha ambayo unaweza kununua gari halisi
 
Kama hivi vya kubebea abiria wanauza vipya kuanzia milion 4. Yawezekana hako wakauza hata milioni saba fedha ambayo unaweza kununua gari halisi
kwa hyo hako si halisi wakati kanatumia petrol ,kana plate number ,unalipia tra ,bima,sumatra na makorokoro yote alafu uwe na leseni ya gari
 
kwa hyo hako si halisi wakati kanatumia petrol ,kana plate number ,unalipia tra ,bima,sumatra na makorokoro yote alafu uwe na leseni ya gari
Basi weka na bei basi afisa masoko? wateja wana njia nyingi za kuuliza bidhaa na saa nyingine tunakera unakuta kama mimi sina hata baiskeli na nina kihitaji lakini nakiuliza stail kama hii
 
Basi weka na bei basi afisa masoko? wateja wana njia nyingi za kuuliza bidhaa na saa nyingine tunakera unakuta kama mimi sina hata baiskeli na nina kihitaji lakini nakiuliza stail kama hii
nitake rradhi mimi mwenyewe nataka kujua
 
Back
Top Bottom