Nimeiona picha ya Lissu nikamkumbuka Benazir Bhutto Pakistan

Kwenye dashidashi hapo ni Kharumwa? Naam, Nyalubele pale kwenye daraja....Waweza pia kwenda Kafita, Kayenze (Msalabani), Bukwimba, Nyangh'olongo na pengine Nyamtukuza (kule kwenye Ukingo wa Ziwa Nyanza....
Nyangh'olongo hadi Nundu ukiutazama ule mlima uliounganika kuelekea Segese
 
Nyangh'olongo hadi Nundu ukiutazama ule mlima uliounganika kuelekea Segese
emoji12.png
Naam. Hapo utakuwa tayari Jimbo la Nsalala......
 
Sa mbona hizo picha za Lisu na Bhuto hazifanani? Kila nikizifananisha naona hazifanani hata chembe

Sasa ndugu unataka wafananaje huku ukijua kabisa kuwa huyu ni mwanamume huku mwingine akiwa mwananke?

Na kwa ushauri tu wa uelewa, rudia tena kuisoma article yote ya mwandishi utagundua kuwa maudhui yake si kuwalinganisha kwa sura hawa watu wawili i. e Lissu na Bhuto!
 
Unaweza kukufuru kwa kubariki kulipiza kisasi lkn ukaamua kumwachia mungu.

Wakati nahangaikia kupata mafunzo ya kupata kumunio katika kanisa la Roman Catholic kijijini kwetu na baadae mtihani wa kupata kumunio............... (makao makuu ya wilaya ya Nyanghwale zaidi ya miaka 29 iliyopita tukisimamiwa na Padri Alphonce Twimanye aliyekuwa parokia ya Nyalubele hapo ndipo nilizisoma kwa uelewa amri za mungu na zile za kanisa. Nilifundishwa kusamehe na kuishi katika maisha kama vile yesu alivyokuwa amejitoa sadaka kwa ajili yetu. Hivyo kadiri nilivyokuwa nikisikia bibi yeyote amekatwa mapanga basi niliamini hao wauaji hakika hawakupitia mafundisho ya dini lkn nimekuja kutambua kuwa zile zilikuwa akili za utoto. Leo katika post ya Facebook ya rafiki yangu Mtanzania mwezangu nimeona ameiposti picha ya Lissu akiwa amekaa kitandani huku akilazimisha tabasamu!!

Wakati nikiwa naitafakari picha ya Lissu gafla nikakumbuka Zanzibar mtaa wa Amani (ulipo uwanja wa Amani Zanzibar) nikiwa nasubiri gari za abiria kunipeleka mtaa niliokuwa naishi (MWEMBE MCHOMEKE MELI SITA) mara nilijisogeza kwenye radio ya mzee mmoja baada ya kusikia mlio wa taarifa ya habari ya BBC, nilikuwa mpenzi sana wa kufatilia taarifa za habari za BBC na ilikuwa 2007 kama sitakuwa nimekosea, mwandishi wa BBC alisikika akitangaza kwa sauti ya woga shambulizi mbaya la mwanasiasa, mama jasiri BENAZIR BUTHO!! BBC walikuwa kwenye kampeni za huyo mama huko Pakistani katika jimbo la LAWALPIDI. Mama wa watu (kumbuka wanawake mimi huwachukulia kama mungu wa pili) aliuwawa kwa kupigwa risasi kichwani mbele ya halaiki ya mashabiki zake akihutubia huku akielekea nyumbani kwake jijini Karachi na kama haitoshi muuaji akamalizia kwa kujilipua.
Nimeandika haya kwa machungu na katika hali ya kukata tamaa kwa siasa za dunia hii, naamini vijana wengi waliokuwa wanapenda siasa za ujasiri kama wanazofanya akina Hussein Bashe, Zitto na mhanga Lissu huko nyumbani watakuwa wanatafakari sana aidha kuzitegea mgongo ama kusubiri kwanza.
Usidaganyike, waliomuua Benaziri ni wacha mungu wazuri tu na kila ijumaa wako msikitini pia waliokusudia kumchakaza risasi Lissu na kumuua ni washiriki wakubwa tu Kanisani tena hata machozi hutoa wakitembelea vituo vya watoto yatima.

Tafakari je wewe uko kundi gani!? Tusimkebehi mungu kwa kuomba tuombewe na kuliombea Taifa huku mkituzomea.
3b65a671ac785b8f4fa880bb37257bc4.jpg
74c8fe15afb30e5f436e2d07b241a5bb.jpg
Padre Alfonse Twimanye kwa kumbukumbu zangu nadhani alipata daraja la upadre mwaka 1989 Na hivyo Si sawa kusema ulipata mafundisho ya komunio kwake zaidia ya Miaka 29 iliyopita
 
Back
Top Bottom