Nimeingiza faida ya 1,092,600 baada ya siku 90 za biashara yangu

mi niliwah kufanya biashara ya ivo shida mteja akija narafiki yake unakuta wanaongea maneno ya kuchombeza chombeza nikawa nadindisha hatari.(ila mungu nisamehe nimetafuna Sana totoz plus wake za watu na nikafilisika bahati nzuri kipind icho icho jakaya akatema ajira) respect to you JAKAYA KIKWETE

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Siku tisini (90) baada ya kufungua Biashara.

Habari wana JamiiForums, leo nimekuja kwenu kupata maoni kuhusu mwenendo wa biashara yangu hii niliyoianza siku 90 zilizopita.

Nilifikiria kuanza biashara hii baada ya kazi niliyokuwa naifanya kufa. Wakati nafikiria kufungua biashara nilikuwa sina mtaji na sikujua nitaupata wapi lakini niliamua kutafuta wapi wanauza bidhaa hizo kwa jumla ili nikifanikisha kupata pesa nisiangaike kutafuta mzigo unapopatikana.

Badaye niliamua kuuza kiwanja changu kwa shilingi 2,000,000/= baada ya makato ya dalali na wakili (wakili tulichangia na mnunuzi) nikabakiwa na 1.9 ku-cut story short, nilikwenda kununua mzigo baada ya kulipia chumba, nauli, nilifanikiwa kuanza na mzigo wa 900,000+

Baada ya kufungua biashara nilianza kwa taabu maana wanasema mwanzo mgumu, lakini nilipambana nikawa kila shilingi ninayouza naagiza mzigo Dar, hivyo hivyo baada ya siku kadhaa mahitaji ya wateja (wanaoulizia) bidhaa fulani ikawa kubwa ikabidi nitafute sehemu nikope pesa niongezee mtaji nikapata 800,000 nikaongeza mtaji dukani.

Ikumbukwe kwamba hapa dukani sitoi matumizi zaidi ya matumizi ya kulihudumia duka kama umeme, mlinzi nk.

Hivyo mpaka leo siku tisini nimeingiza faida ya 1,092,600/= .

Swali langu kwenu: Je, ninakwenda vizuri na biashara hii au napiga mark time tu?
Tatizo hujasema unauza nini mkuu
 
300k kwa mwez, 10k kwa siku..
Kweli kuna watu mnatafuta hela kwa shida sana.
Ungeweka wazi basi ni biashara gani?
Huishi tz!
Unafanya biashara au umeajiriwa?
Kwa biashara yenye miezi mitatu huo Ni uelekeo mzuri bila kujali Ni biashara gan
 
Huu uzi umeuweka kwa makusudio gani ndgu yangu?

Kwakweli umefupisha mpaka umezidisha!!
Hujasema ni biashara gani, uko wapi! Hiyo ni faida kweli??

Haya nikupongeze kwa kuanzisha biashara.
 
UPDATE

From JANUARY TO MARCH

Hiki ndicho nilichokivuna 747,050/=

Habarini wana jamvi wengi walitamani kusikia mambo yapoje baada ya miezi mitatu mingine. Kiukweli biashara ni ngumu lakini Mungu ni mwema hicho ndicho nilichovuna
Najua wapo watakao beza Karibuni

Picha naleta soon
Dah imepungua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biashara imekupa promotion usigande ukizan graph inaganda hvy muda wote .... Muda na mabadiliko havizuiliki😁
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom