Nimeingia TRA nimeambiwa TIN laki na nusu. Je, wako sahihi?

Mzee wa kusawazisha

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
1,251
2,000
Leo nilikua na mlolongo mrefu nimeanza Tigo shop, Airtel shop, kisha TRA. Lengo nipate miongozo na hatua za kupata laini za wakala.

TRA sehemu ya mwisho kupita nimeambiwa kwanza nipate TIN mengine yatafuata, lakini mimi lengo nipate gharama za awali ili nianze na michakato maana bajeti ni muhimu, jamaa alilipa laki na nusu.

Najua humu kuna wazoefu wa hizi kazi na wapo wamepitia huko. Naombeni mnihakikishie bei sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
23,358
2,000
TIN NI BUREEEEEE....NO SINGLE CENT...
NENDA KWA INCHARGE HAO NI VISHOKA

Usiku Wa Shida Hauchelewi Kucha
Ukifika TRA Usikubali Mtu Akupokee Kwa Maneno Laini Nenda Hadi Ndani Ofisini


Hapo Huduma Huanza Taratibu
Hao Makanjanja Wapo Wengi Sana
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
26,630
2,000
Unalijua lile Tangazo ka TRA kwny TV yule msukuma amepigwa na vishoka sababu ya TIN?

Itakua nawe walikuona wa dizaini hio.
 

chuma cha reli

JF-Expert Member
Jul 2, 2012
2,554
2,000
Kipindi ile kupata TIN haraka haraka ndani ya dakika 5 pale samora ave ilikuwa ni elfu 10 ,mkono ukiwa mfupi unakaa wiki mbili tena kwa kuzungushwa zungushwa

Kipindi iyo watu individual walikuwa wanachukua TIN kwa ajili ya kulipia driving licence tu

Elimu ya kulipa kodi bado inahitajika sana watz wengi wanakwepa kodi sababu eiza hawajui au wanakutana na maafisa kodi vishoka au makanjanja

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom