Nimeingia kwenye uhusiano naye kama mwezi 1 hivi lakini tayari anataka nimkopeshe pesa milioni 2

Kopesha tu mkuu, na pia Jiandae kudai Deni.

kama una moyo wa Sufi achana kabisa na hiyo habari baki na pesa zako.
 
Jiulize kwanza kwa nini ulikibaliwa! Ulionesha uwezo wako kifedha? We mpe tu ila habari ya kurudisha haipo. We kazana kumfukunyua tu ijifidie
 
Umeshasema ni mtumishi kwanini asiende kukopa bank?za kuambiwa changanya na zako unless kama umeamua kutoa hiyo pesa kama sadaka
 
Nadau nimeingia kwenye uhusiano naye kama mwezi mmoja hivi lakini tayari sasa hivi anataka nimkopeshe pesa shilingi milioni mbili

Yeye ni mtumishi wa umma ila wasiwasi wangu nikimpatia hiyo pesa atarudisha kweli au ndio nitacheza karata tatu kuliwa maana ni mapema

Wale wazoefu waniambie nikitoa hii pesa atarudisha kweli?
Kama wewe ni mwanaume jua mwanamke hakopeshwi pesa, anapewa!! Ukijiloga kumkopesha imekula kwako.
 
Duh! Kwanza wewe ni Me au Ke?
Pili, kama kweli unataka kumsaidia, chukua hiyo pesa, alafu umpe mtu anayejua kudai. Mwambie huyo mpenzi wako kuwa huna, ila utamdhamini akakopeshwe na mtu fulani. Unaenda naye kwa yule mtu alafu wanaandikishana. Chochote kitakachotokea, watadaiana wao kwa wao. Wewe utaweza kuipata pesa yako kwa mgongo wa nyuma.
Otherwise, hiyo milioni mbili iwe ni pesa ndogo kwako. Yani isiwe imezidi asilimia 20% ya pesa yote unayomiliki. Ikizidi hapo utakuja kushika kichwa....
Mleta mada fwata huu ushauri.
 
Hakuna majaribu kwenye ela hata siku moja mkuu,na tambua pesa ndo kila kitu
 
Mpenzi huwa hakopeshwi kama unampa mpe tu mkuu ila usitegemee kurudishiwa
 
Back
Top Bottom