Nimeingia kwenye maombi ya kufunga ili bei ya mafuta ifike 150USD kwa pipa

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,318
8,228
Mafuta ni bidhaa inayoendesha uchumi wa nchi.
Bila mafuta uchumi unayumba na kusimama.

Lakini pia bei ya mafuta ikipanda inapandisha gharama za maisha kwasababu bei ya mafuta ndio inayoaksi bei za bidhaa zinazotegemea chombo kinachotumia mafuta ili kumfikia mtumiaji.

Kwanini mafuta, mafuta yanatumika kwenye vyombo vya usafiri kama vile magari, ndege, matreni, meli n.k.

Vyombo vya usafiri vinafanya kazi ya kusafirisha watu na bidhaa mbalimbali kutoka sehemu moja Hadi nyingine.

Pia mafuta yanatumika kwenye mitambo inayofanya kazi nzito kama vile kuchimba madini, ujenzi miundombinu n.k.

Mafuta yakikosekana au kupanda bei yanatufundisha nini?
Mafuta yakikosekana au kupanda bei sana yanatufundisha somo la kuweka mikakati endelevu ya kujitegemea kiuchumi. Kutafuta mafuta yetu wenyewe ili siku yakikosekana kabisa uchumi wetu usiathirike.

Yanatufundisha somo la energy security, kwa kununua mafuta ya kutosha kipindi yakiwa na bei ndogo na kuyahifadhi ili kipindi yanapopanda bei au kukosekana taifa liweze kupunguza bei za mafuta nchini.

Sasa kwanini nimeamua kufanya maombi ya haya ili bei ipande zaidi. Nataka taifa letu lijifunze kuchukua hatua endelevu za kuleta matokeo ya muda mrefu ili kutatua tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta ndani ya taifa letu.

Juzi marekani wenzetu baada ya bei kupanda. Wamechukua mafuta waliyohifadhi ili kudhibiti bei isipande sana.

Tuungane kwenye maombi jamani.
 
Kwa hiyo ulitaka na sisi tufanye kama Marekani ? Hapo si sawa na kutegemea sisimizi aangushe miti kama tembo afanyavyo.
 
Back
Top Bottom