Nimeikodi helikopta bila kushauriwa wala kuelekezwa na Jussa wala Hamad Rashid - Mtatiro

MAALIMSEIF ni mpuuzi as ameshindwa kuonesha uwajibikaji kwa waziri tena wa chama chake kuzembea mpaka meli ikazama
Seif angemlazimisha waziri ajiuzulu au angeitumia CUF kumshinikiza waziri ajiuzulu

Maria
Kama ukiangalia huyo jamaa na wengine wengi CUF walitaka tu kupata ulaji Zanzibar kwa kupewa shavu na CCM, wamesababisha watu wengi wamekufa bure, angalia sasa walivyo, wanavimba mashavu tu na matumbo kwa safari za nje, ona wenzao wanavyoumbuka huku Bara, yaani aibu tupu!!
Lakini ndio hivyo, ukikubali kuolewa, usilale na ch***pi!
 
Mtatiro kwani umefungwa kamanda? CUF wameiharibu wao wewe shida yako nini sepa na sio wewe tu, na wengind jamani tuunganishe nguvu kuwang'oa hawa wanyonyaji kina magamba A na Magamba B. Njoo CDM tuipiganie nchi yetu.
 
Na bado, hatuitaji siasa zenu uchwara za KUGAWANA MADARAKA. Kama hufahamu hiyo ndio ndoa yenyewe na nyinyi mnaita maridhiano. Endelea kupiga kelele ila ndoa yenu inaonekana na kila mtu na sio propaganda.

ndoa ya mkeka!
 
Mkuu nimekusoma lakini hata sikuelewa hii mada inahusu kitu gani na unataka kuthibitisha kitu gani... Naona umeweka barua za kukodisha na mafuta zingine zikiwa na maandishi confidential lakini umepuuza na kuziweka hapa - ili iwe nini?.. Kama kuna madai ya kwamba fedha za kukodisha Helikopta zimetolewa na Rostam, barua hizi zinathibitisha nini? Ya kwamba CUF ndio wamekodisha sio Rostam! kwa taarifa yako hakuna barua hata moja inayothibitisha lolote. Haya ni mawasiliano ya kukodisha hakuna hati, hundi wala cashbook kuonyesha fedha za michango mlopokea kwa ajili ya uchaguzi wa Igunga.

Mkuu wangu, sasa CUF kimekuwa chama cha kihuni, na mara zote pinga kitu chenye maana kwa sababu hata kama Rostam aliwapa fedha, mkitaka tusijue, hatuwezi kujua na wala huyo Rostam hawezi kuongeza wala kupunguza imani ya watu akiwapa fedha au kutowapa. Chama kimeshapoteza mwelekeo toka siku mlokubali MUAFAKA na CCM, toka siku mlobadilisha kauli zenu na kuitaka Zanzibar huru, kuvunja muungano na kadhalika ili mradi mpate kuibana CCM mpate kuongoza nao ktk serikali ya Zanzibar tena kabla hata ya kusubiri matokeo ya uchaguzi mkuu. CUF mlipoteza dira yenu kama walivyopoteza CCM na sii swala la kuwaelimisha wananchi kama unavyodai.

Ila Kazi kubwa ni nyie wenyewe KUELIMIKA na kufahamu ya kwamba wananchi wamechoka na hizi hadithi za Utajirisho ili hali mnatumikia ilani ya chama CCM, halafu mkiambiwa nyie ni CCM - B mnakuja juu. Kama CUF sio CCM - B inakuwaje mnatumikia Ilani ya CCM ktk utawala wa mseto mlofunga na CCM, si bora mngebakia chama cha Upinzani!...Unaweza kunijibu ktk hilo?
Mkuu Mkandara, pamoja na maneno yako mazuri kwa Mtatiro' lakini sizani kama atajitokeza hapa kujibu hichi ulichomuuliza. Mtatiro hana tofauti
na Nape Nnauye linapokuja swala la kuitetea hoja hapa jamvini. Yaani hawa jamaa mchezo wao ni kutupia post hapa jamvini alafu haooo wanai
ngia mitini.....ila kidogo huyu Mtatiro anabusara na hekima kuliko Nape Nnauye na pia bado anamvuto fulani machoni mwa watanzania. Binafsi ningefurahi sana kama angekuwa kila akipost hoja fulani basi ingekuwa anaisimamia mpaka mwisho kama wafanyavyo wanasiasa wengine hapa
jamvini.
 
Mtatiro kwani umefungwa kamanda? CUF wameiharibu wao wewe shida yako nini sepa na sio wewe tu, na wengind jamani tuunganishe nguvu kuwang'oa hawa wanyonyaji kina magamba A na Magamba B. Njoo CDM tuipiganie nchi yetu.
Well said mkuu! yampasa aangalie na kutambua alama za nyakati
 
Mdogo wangu Mtatiro
we ni mwanasiasa Mzuri sana, lakini kwa nini unapoteza nguvu na muda kufanya siasa za hovyohovyo, siasa uchwara?

Hivi unafikiri kuna Siri katika siasa?

Bora ubaki huna chama kuliko siasa unazozifanya
 
Tatizo ndoa ndoa ndoa ndoa! Lakini msikonde maana mme akishinda na nyie mmeshinda.
 
Ahsante sana Julius kwa kuuweka Uwazi na Ukweli hadharani kiasi hiki, huu ndio mwazo wa ushindi wa kweli wa kidemokrasia kwani ina hadi kuifikia ina mwendo mrefu na visiki vingi. Usivunjike moyo wewe na Chama Chako endeleeni na jipangeni na mwishowe mtafika.

CHADEMA ni Chama Kilichokosa fadhila na ihsani lau kama kingalikumbuka mchango wenu wa kuanzisha vugu vugu lakuitafuta Demokrasia Nchini Tanzania hadi kufikia kukata mbuga na milima na misitu na mapori yalioharimu damu na maisha ya Watanzania leo Wangalikuheshimuni kwa kuwa ni nyie ndio MABABA wa Demokrasia hapa Nchini lakini wapiiiii.

Watizame CHADEMA walivyotokwa na haya na Ulafi uliowajaa na zaidi UCHAGA na UDINI ulivyowazonga na waonea huruma mwisho wao hauko mbali ngoma ikivuma sana mwishowe hupasuka.

Sisi tunaothamini misingi ya Demokrasia tunajuwa nyie ni Wapinzani wa Kweli na subirini nasi tushaanza kujikusanya kwa pamoja na kwa kuwa nasi tupo Tanzania Nzima tunajipanga kisawa sawa Kuwashugulikia CHADEMA NA CCM Kuanzia katika vijiji, Kata, wilaya, mikoa yote ya TANZANIA Kuhakikisha 2015 hapa TANZANIA HAPANA CHADEMA WALA CCM

Kweli wewe ni Kiberenge sishangai subiri utiwe mizigo
 
Mtatiro hauhitaji somo jingine lolote kuamini kuwa CUF imekwisha! uamuzi wa kutumia Helkopta na pesa nyingi na kuambulia 4% unajitosheleza kuwa uko wrong side, ungetumia magari peke yake ingekuwaje? kama unaweza jipange upya ama kwenda CCM au CHADEMA, otherwise karibu watanzania wote watakuchoka na kukudharau, pia acha kutapatapa na CDM, unabwabwaja sana hadi unakera, CDM inazidi kupokelewa na kukubarika, be careful man! you are destroying your own future man! na utafutika kama Tambwe... etc. Ni ushauri tu, CUF na CCM ni Watawala wanaotakiwa kuondoka madarakani! kwa sasa hauna mvuto kama wenzako, unaonekana unapiga kelele tu man!
Kalia Mbwata!
 
Helikopta tuliyoitumia kwenye uchaguzi wa Igunga nimeikodi mimi mwenyewe ...hatuwezi kushindwa kukodi helikopta kwa TZS 50m
Kwa hiyo wewe mtu mmoja una mamlaka ya kujiamulia kivyako ku spend milioni 50 za taasisi ya kitaifa?

 
Mdogo wangu Mtatiro
we ni mwanasiasa Mzuri sana, lakini kwa nini unapoteza nguvu na muda kufanya siasa za hovyohovyo, siasa uchwara?

Hivi unafikiri kuna Siri katika siasa?

Bora ubaki huna chama kuliko siasa unazozifanya

mtatiro ni mganga njaa kama seif hafai kujoin team makini kama cdm
 
Kama ni kujibu tuhuma, Bw. Mtatiro naona kama hujajibu hizo tuhuma. Umeweka barua ya kuomba kibali cha hiyo helikopta ku-operate Igunga lakini hujaelezea process au risiti mlizotumia kupata hiyo chopa. Inawezekana chopa ikalipiwa na mtu mwingine na mtumiaji akawa mwingine.

Kitu kingine; kwenye headed paper ya chama chenu, inakuwaje mnaweka personal emails za Maalim Seif pamoja na ya kwako wakati mna domain tayari? Hata kama mngekuwa hamna domain, ni vipi anuani zingine ziwe za chama lakini emails ziwe personals? Je hayo masanduku ya barua nayo ni personal? Je nini tofauti ya kati ya Makao Makuu na Ofisi Kuu?

Nafikiri mnahitaji kufanya marekebisho kidogo kwenye headed paper yenu, mkitumia Grid naamini itawasaidia. Ninaweza kutoa huo msaada Free of Charge kama mtahitaji. Unaweza kuni PM
 
ni vigumu sana kufuatilia malipo kupitia bank je kama malipo yalifanyika kwa fedha tasilimu italuwaje
 
Kutafuta risiti Tanzania sio ishu kabisa..mihuri ndio acha kabisa,watu wanayompaka ya ikulu..Ushauri wangu kwako Mtatiro,achana na CUF tafuta chama chenye mashiko kwa wananchi!
 
Back
Top Bottom