Nimeikodi helikopta bila kushauriwa wala kuelekezwa na Jussa wala Hamad Rashid - Mtatiro

Jun 20, 2009
45
225
Helikopta tuliyoitumia kwenye uchaguzi wa Igunga nimeikodi mimi mwenyewe na wala haikumhusisha Jussa wala Hamad Rashid.
Haya masuala ya kuwa imetolewa na na ROSTAM AZIZ ni propaganda zinazopigiwa debe tu kama ilivyo ishu ya CUF IMEOLEWA NA CCM, CUF NI CCM B n.k.

Hizi ni propaganda zilezile za kuiumiza CUF lakini sie kama chama tutaendelea kuwa imara na kuwaelimisha wananchi juu ya propaganda hizi ambazo zinafanywa ili kuhakikisha CUF haiungwi mkono.

Nime-attach docs muhimu ambazo nilizi-process mimi mwenyewe kupata HELIKOPTA. Chama chetu kinapata ruzuku ya TZS 100m kwa mwezi, hatuwezi kushindwa kukodi helikopta kwa TZS 50m hadi tusubiri kufadhiliwa na makada wa CCM. Na tangu nimekuwa kiongozi wa CUF sikuwahi kuona tunafanya jambo lolote kwa pesa za kuletewa na matajiri.

Kinachoshangaza ni kuwa watanzania wakiandikiwa propaganda yoyote huanza kusihabikia na kuisambaza bila kujua nani aliyeileta na ana malengo gani na ikishafanya kazi itamnufaisha nani.

Pia, Baraza kuu la CUF halina mandate za kiutendaji, masuala yote ya kuidhinisha bajeti kubwa za chama au za dharura yanafanywa na KAMATI YA UTENDAJI YA TAIFA na baraza kuu litakagua taarifa kama kila kilichotumiwa na kufanywa na KUT ni sahihi na kilifuata masharti ya kibajeti ya chama.

Aliyeweka thread kuwa tumehongwa helikopta na CCM asome hizi docs and details na UONGO wake hataufanya siku zote.

Mtatiro.
 
sawa mkubwa!tuliza hasira!nguvu nyingi unaambulia asilimia 4!najua inauma but jipange kwa chaguzi zitakazojitokeza tena!
 
hongera sana kijana kwa mwenendo huo utaweza kuleta mabadiliko tanzania.usisahau na kuiponda chadema kwenye kila mahojiano yako ila nashangaa leo hujaitaja au kazi imeisha? jana pale kwa mkurugenzi ulikuwa kituko hongera sana
 
Julius Mtatiro ni miongoni mwa wanasiasa wachache sana nchi hii walio makini, wakweli na wanaoweza kutembea kwenye maneno yao.

Wanasiasa wengi tulio nao kwenye vyama vyoote ni wapiga domo tu wanaotafuta maisha kupitia siasa, kama tunataka tutoke hapa tulipo tunahitaji wanasiasa wengi zaidi wa aina ya Mtatiro, nakuunga mkono kijana...
 
Mtatiro

peleka justifications zako kwenye daily tabloids so as the bottomline tanzanian can reach, jf are too clever and it can unfold other things beneath and unexpectedly

as time goes cuf is running out of ideologies and you are now stand to defend what you call propaganda, trickly propagate propaganda to popularize your party and win support
 
inawezekana kabisa wewe ndio ulifanya maandalizi yote ila aliyetoa hela ya kukodisha ni mtu mwingine kabisa
Hili ndilo la msingi analotakiwas kulijibu. hakuna aliyehoji process ya kukodi choppa. Tunachotaka kujua fedha zilitoka wapi. Sidhani kusema tu kwua chama kinapata ruzuku ya Sh100 kwa mwezi haitoshelezi kuonyesha kuwa ruzuku ndiyo imelipia chopa
 
Sawa, Sio Sawa?Sawa sawa jamani kumbe tatizo ilikuwa ni jina refu mwisho linaishia na Rais na traffik mbele.
 
Next time msikodi helikopta tena.......madhara yake nadhani umeyaona kupata kura kiduchu....hayo madude yana wenyewe na si kila mtu anaweza kuyatumia
 
Ahsante sana Julius kwa kuuweka Uwazi na Ukweli hadharani kiasi hiki, huu ndio mwazo wa ushindi wa kweli wa kidemokrasia kwani ina hadi kuifikia ina mwendo mrefu na visiki vingi. Usivunjike moyo wewe na Chama Chako endeleeni na jipangeni na mwishowe mtafika.

CHADEMA ni Chama Kilichokosa fadhila na ihsani lau kama kingalikumbuka mchango wenu wa kuanzisha vugu vugu lakuitafuta Demokrasia Nchini Tanzania hadi kufikia kukata mbuga na milima na misitu na mapori yalioharimu damu na maisha ya Watanzania leo Wangalikuheshimuni kwa kuwa ni nyie ndio MABABA wa Demokrasia hapa Nchini lakini wapiiiii.

Watizame CHADEMA walivyotokwa na haya na Ulafi uliowajaa na zaidi UCHAGA na UDINI ulivyowazonga na waonea huruma mwisho wao hauko mbali ngoma ikivuma sana mwishowe hupasuka.

Sisi tunaothamini misingi ya Demokrasia tunajuwa nyie ni Wapinzani wa Kweli na subirini nasi tushaanza kujikusanya kwa pamoja na kwa kuwa nasi tupo Tanzania Nzima tunajipanga kisawa sawa Kuwashugulikia CHADEMA NA CCM Kuanzia katika vijiji, Kata, wilaya, mikoa yote ya TANZANIA Kuhakikisha 2015 hapa TANZANIA HAPANA CHADEMA WALA CCM
 
Na bado, hatuitaji siasa zenu uchwara za KUGAWANA MADARAKA. Kama hufahamu hiyo ndio ndoa yenyewe na nyinyi mnaita maridhiano. Endelea kupiga kelele ila ndoa yenu inaonekana na kila mtu na sio propaganda.
 
Mtatiro amepewa Chopa watu wazima wakachakachua Kura! tuna safari ndefu sana ya kuiona Tanganyika tuitakayo!
 
Jambo la kwanza kama chama tutakuchukulia hatua za kinidhamu kwa kuexpose document wakati zinajieleza wazi kuwa hairuhusiwi na hata mwenyekiti hana taarifa kama unazi-expose

Pili, hata nikitaka document za kuonesha Mtatiro ni mkimbizi nchi hii ninauhakika ndani ya masaa machache naweza kuzipata na ukatolewa Tanzania faster.....Kama kapuku mimi naweza ije kuwa ninyi ambao ni UBAVU wa kushoto wa CCM- Magamba? Ni rahisi sawa na mume kutoa posho ya matumizi kwa wifey wake

Piga tu mayowe na bandika document zote lakini NDOA YENU NA CCM HAIHITAJI CHETI CHA NDOA TOKA BAKWATA wala wapi kuthibitisha KUWA NYIE NI BI & BWANA CCM MAGAMBA
 
Kwani huwezi kufanya vitu kinyume, wewe ni msomi Bwn unaweza kutumia mbinu zozote kutimiza malengo yako. Mtaji wa kura 11,000 uliotamba nao umekwenda wapi????? Kweli CUF hamjauza hizo kura???????
 
Ahsante sana Julius kwa kuuweka Uwazi na Ukweli hadharani kiasi hiki, huu ndio mwazo wa ushindi wa kweli wa kidemokrasia kwani ina hadi kuifikia inamwendo mrefu na visiki vingi, usivunjike moyo wewe na Chama Chako endeleeni na jipangeni na mwishowe mtafika, CHADEMA ni Chama Kilichokosa fadhila na ihsani lau kama kingalikumbuka mchango wenu wa kuanzisha vugu vugu lakuitafuta Demokrasia Nchini Tanzania hadi kufikia kukata mbuga na milima na misitu na mapori yalioharimu damu na maisha ya Watanzania leo Wangalikuheshimuni kwa kuwa ni nyie ndio MABABA wa Demokrasia hapa Nchini lakini wapiiiii watizame CHADEMA walivyotokwa na haya na Ulafi uliowajaa na zaidi UCHAGA na UDINI ulivyowazonga na waonea huruma m,wisho wao hauko mbali ngoma ikivuma sana mwishowe hupasuka. Sisi tunaothamini misingi ya Demokrasia tunajuwa nyie ni Wapinzani wa Kweli na subirini nasi tushaanza kujikusanya kwa pamoja na kwa kuwa nasi tupo tanzania Nzima tunajipanga kiswa sawa Kuwashugulikia CHADEMA NA CCM Kuanzia katika vijiji, Kata, wilaya, mikoa yote ya TANZANIA Kuhakikisha 2015 hapa TANZANIA HAPANA CHADEMA WALA CCM


Yakhe jina lako nani vile?

Naona bado una hallucination za MV Spice


Any
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom