Nimeijaribu hii series kumbe ni ya kipuuzi hivi, watu wameipendea nini?

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,961
Nimeona kwenye matangazo mengi hii serires ikipewa promo kubwa sana, hadi watu wengi wanaweka zile mask za wale robbers kwenye dp zao.

Nikaona niitafute bana. Dah Money Heist ni series ya hovyo, haipo level moja kabisa ya kuitwa series kali na inaboa kuitazama.
Nimejaribu kuitazama kwa kujilazimisha hadi nikafikia episode ya 9 naona imenishinda kabisa.

Japo story yao imetungwa kwa kufanana kidogo na Prison Break, hii imekosa msisimko kwani imebase upande mmoja, yaani mtungaji wa story kamfanya yule kiongozi wa robbers (Professor) kuwa ana akili sana na polisi akawafanya ni wajinga sana, mpango wa Profesa unafanikiwa na kila mpango wa polisi unafeli kiasi kwamba haijabalance hata kidogo.

Eti Profesa anatabiri polisi watafanya hivi kisha wanafanya, watafanya vile kisha wanafanya, watafanya vile tena wanafanya pia, yaani ndio mtiririko ulivyo.

99% ya mipango anayopanga Profesosor inafanikiwa huku mipango karibia yote ya polisi dhidi yao inafeli, yaani haina msisimko kama mechi ya Taifa Stars na Ujerumani.

Prison Break ilikuwa na msisimko sana sababu Michael mipango yake ilikuwa haiendi kama alivyokuwa amepanga na hivyo kuleta msisimko kwa mtazamaji kuwa jamaa atafanyaje au atakamatwa au vipi.
 
Hebu tajeni series kali za kuanzia 2016 mpaka sasa. Ziwe na mkono wa kutosha, maswala ya ujasusi ya kumwaga, akili nyingi na misheni za nguvu zitakazo niacha moyo ukidunda

Achana na za sayansi na supernatural powers na zile za kina game of throne
 
Mkuu Lacasa dë papel nnayo nimeishia kwenye kipande cha kumi kama sikosei. Ilisifiwa mno na watu kibao. Nikajua watunzi walitumia akili kumbe ujinga mtupu. Tokea mwanzo tu walivovamia benki sijui bullion limekaa kama museum. Haliko secure na eti kuna mlango mmoja tu. Wale jamaa sijui walikula nini siku zote na prof alikuwa daredevil sana kitu ambacho hakina uhalisia. Ilinishinda
 
Police mipango yao inaweza kuwa inafeli sababu hawakujua majambazi watavamia. Ile ni mojawapo ya series nzuri. Sema unaikubali prison break sababu ndo ilianza. Hata mimi bongo freva za mwanzo mwanzo naziona tamu kuliko hizi za sasa.
mtu anatabiri polisi waafanya hivi, kisha wanafanya kweli, kila tukio, haina uhalisia. kingine wale wezi alikuwa akiwapa bahati zote ziwaangukie huku polisi gundu ziwe upande wao. Very predictable and very boring, boring,boring
 
Back
Top Bottom