Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,907
3,261
MFANYABIASHARA MAARUFU MOHAMMED DEWJI APATIKANA AKIWA HAI

Amepatikana akiwa ametelekezwa kwenye viwanja vya Gymkhana

Baada ya kutekwa, Gari la watekaji liliendeshwa kwa kasi sana na kwenda kuwekwa kwenye chumba akiwa amefunikwa uso

Inasemakana watekaji walikuwa wakiongea lugha inayoonekana kuwa ni ya Afrika Kusini'

Tanzania, Mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ aliyetekwa Oktoba 11 na kupatikana leo Jumamosi Oktoba 20, 2018 saa nane usiku baada ya waliomteka kumtupa katika Viwanja vya Gymkhana katikati yajijini la Dar es Salaam.

Habari zaidi soma=>Dar: Mfanyabiashara Mohammed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay - JamiiForums

=======

“Namshukuru Mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani. Nawashukuru Watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao. Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo Jeshi la Polisi, zilizofanya kazi ya kuhakikisha narudi salama.” — Mohammed Dewji (Saa 9:15 alfajiri, Dar es Salaam)

“I thank Allah that I have returned home safely. I thank all my fellow Tanzanians, and everyone around the world for their prayers. I thank the authorities of Tanzania, including the Police Force for working for my safe return.”
— Mohammed Dewji (3:15AM, Dar es Salaam)



023B495A-4BC9-48B3-BF4E-7BC99ABE81DA.jpeg

6425F028-C539-4DD0-89D9-504E42942A17.jpeg




 
Wamebana wameachia, Jiwe siyo Mtu!.

Namshauri Mo asepe atulie zake huko Brunei au Kisiwa chochote cha Pasifiki ale bata miaka saba ipite kisha arudi tujenge nchi!, yeye bado kijana, kupumzika miaka saba siyo ishu!
Ameona tz itawaka moto ,kaamuru watu wasiojulikana wamurudise salami salimini, lakini namushauri hivyo hivyo ahame tz kabisa
 
Hii inaonyesha familia wamelipa ransom!

Moja ya masharti ya ransom ni kutozungumza kuhusu tukio lote!

Kama atazungumza kuhusu yaliyomsibu mpaka akarudi basi hiyo itaonyesha kuwa hakulipa ransom na hakuna makubaliano.

Hoja iliyopo mbele yetu kwa sasa, Je, kama amelipa ransom, nini kwa sasa nafasi ya matajiri nchini kuhusiana na usalama wao kwa sababu kulipa ransom ni kufungua mlango wa biashara ya kidnapping and ransom nchini kwa matajiri.

Kosa la kulipa ransom baada ya kutekwa ambalo nchi za kusini mwa Afrika kama Afrika Kusini na Msumbiji walilianza kwa matajiri ndilo kwa sasa linazidi kuwatafuta kwa kasi zaidi.

Je, kuna uwezekano na Tanzania tukaelekea ambako nchi za kusini mwa Afrika ziliko kwenye biashara ya kidnapping and ransom?
 
Back
Top Bottom