nimeibiwa simu yangu: nifanyeje?

minda

JF-Expert Member
Oct 2, 2009
1,068
67
wakuu,
jana nilikuwa kwenye sherehe ya bdau ya mtoto wa mtwasi wangu na wakati wa kwenda ku-tos na mtoto (cheers), simu yangu ilipotea katika mazingira ya kutatanisha kwani dakika chache baada mc kutangaza kupotelewa cm yangu haikupatikana tena baada ya kupiga kwa kutumia nyingine japo muda mfupi ilipatikana na betri ilikuwa imechajiwa mchana huo.


inavyoonekana "aliyepata" simu hiyo hakuwa na lengo la kunirudishia.

kwa bahati cm hiyo pamoja na kadi yake zote ni pin coded (zinafunguka kwa namba ya siri) na zimesajiliwa; je nifanyeje ili niweze kupata cm yangu?
 
Hahahahah kiongozi umesaidia kupunguza umasikini! Jamaa ataiuza kwa bei ya chini na kuipeleka kwa fundi Selemani pale Mjini itakuwa decoded. Pole sana tafuta simu nyingine rudishia namba kama ulivyoshauriwa na mdau hapo juu.
 
Au kwa mwesiga pale juu empresss wataichakachua huvwo vupini ni kama unandika na penseli katika karatasi!!wakati kifutio kina futa!!
 
Mkuu tafuta nyingine na simcard yako watakurudishia ukuwasiliana na customer care!
 
Pole sana. Nunua nyingine
Kama kampuni za simu tanzania zingeshirikiana u zingeshinikizwa na TCRA na polisi tatizo hili lingepungua.

Kimsingi ukireport polisi simu yako imebiwa na ukienda Povider anatkiwa Kuiblock ile IMEI No. Lakini Kampuni za simu hazifanyi hivyo. Na wala hakuna sheria hata inayowalzamisha kushare na ku block IMEI No za simu zote ziliolirpotiwa kuibiwa kwenye kampuni zote za simu.

Kama ungekuwa ni Mtoto wa JK au Mkurgenzi wa UWT ungeshangaa unaipata simu yako. Tatizo la tanzania kuna sheria mbili.
 
asanteni wakuu wote mlionishauri; nitazingatia.
 
Sasa lile zoezi tulilofanya la kusajili simu lilikuwa na faida gani? upuzi mtupu!
 
Sasa lile zoezi tulilofanya la kusajili simu lilikuwa na faida gani? upuzi mtupu!


nilikuwa nimepanga kwenda polisi kuchukua rb ili kama huyo jamaa akipatikana anitake radhi nikitegemea itakuwa rahisi kumpata akianza kutumia simu kwani imei yake ni muhimu; laklini naambiwa labda niwe mtoto wa jk labda ndipo hawa wajamaa wa mitandao watanifikiria.
 
Jaribu kwenda kwa service provider wako....ukiwa na ile IMEI....
Kuna mtu namfahamu alienda wakamsaidia....aliyenunua ile simu aliitwa kwa hila kidogo wakamkamata..then kataja mwizi...
Usiache kwenda kwa kuhisi hutasaidiwa...nenda kwanza....
BTW: Kama ukienda uje utoa ushuhuda wako hapa ili tuelimike zaidi.
 
ni makampuni ya simu ya Tanzaia pamoja na police kutofatilia hivyo vitu labda viwe sensitive sana,
kama simu imesajiliwa ama kama unaweza kukumbuka IMEI No, hata kama mtu akibadilisha SIM card, lakini akipiga simu ama kupokea, huwa inaonekana anatumia SIM card gani na hiyo IMEI no pia inaonekana, na vilevile ni raisi kujua huyo anayepiga ama kupokea anatumia minara gani (Radius ya nearest tower) hivyo ni raisi kumlocate
ugumu unakuja kwa police kupeleka hiyo taarifa kwa makampuni yote ya simu kuwa waifatilie hiyo handset (IMEI NO)
Lakini ni kitu ambacho kinawezekana mimi nilishuhudia mtu akikamatwa kwa kesi kama yako (sio Tanzania lakini ni hapahapa Africa)
 
Jaribu kwenda kwa service provider wako....ukiwa na ile IMEI....
Kuna mtu namfahamu alienda wakamsaidia....aliyenunua ile simu aliitwa kwa hila kidogo wakamkamata..then kataja mwizi...
Usiache kwenda kwa kuhisi hutasaidiwa...nenda kwanza....
BTW: Kama ukienda uje utoa ushuhuda wako hapa ili tuelimike zaidi.


umenipa motisha mkuu kwani nilishachoka!
 
Usiamini kampani yoyote unayokutana nayo kwenye sherehe yoyte usiyoifahamu..
Wadada flani waliibiwa viatu vyao baada ya kuviacha chini ya meza na kwenda kucheza ngoma kwenye harusi..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom