Nimesahau mzigo ndani ya basi

Allency

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
13,466
12,916
Habari wakuu.

Moja kwa moja kwenye mada, Jumapili iliyopita ya tarehe 05/06/2022 mida kama ya saa 1 usiku kuelekea saa mbili nikiwa natoka Dar kwenda Morogoro ndani ya bus mali ya kampuni ya Frester nikaamua kushukia Chalinze na kusahau begi langu lenye computer na vitu vingine. Nikatafuta usafiri mwingine kwenda Moro ili kufatilia begi langu lakini mpaka nafika Moro nikakuta bus limefika muda mrefu sana na abiria wote wameshashuka na bus limepaki kimya kabisa.

Ikabidi niende ofisini kuulizia maana ilikiwa usiku tayari mida kama ya saa saba. Ofisini sikukuta mtu zaidi ya abiria waliolala wakisubiri kusafiri kesho yake. Narudi nyuma kidogo, ni kuwa baada ya kujua nimesahau begi nilipiga zile namba za simu za kwenye tiketi kama nne ndipo nilipompata muhusika kwani wengi walisema wameshaacha kazi kampuni ile.

Muhusika alipokuja mida kama ya saa kumi tukaenda kwenye bus na kukuta dereva kalala kwenye bus na akajibu kupitia dirishani kuwa hajaona hilo begi. Nikapata wazo la kwenda Polis, nikaja na Polis wa kike na dereva akafungua mlango tukaingia ndani kukagua, kweli hakukuwa na begi ila mkoba tu wa kike uliosahaulika pamoja na demu wa dereva kumbe walilala humo.

Hisia zangu zinaniambia kuwa dereva, demu wake na kondakta ndiyo wamechukua mbegi langu. Naombeni msaada wa kipi cha kufanya kupata begi langu kwani ni muhimu sana na niko tayari kwa njia yoyote ile na kulipa gharama.

Ikumbukwe pia kuwa mzigo wa ndani ni dhamana yako/yangu.
 
Habari wakuu.
Moja kwa moja kwenye mada, jumapili iliyopita ya tarehe 05/06/2022 mida kama ya saa 1 usiku kuelekea saa mbili nikiwa natoka Dar kwenda Morogoro ndani ya bus mali ya kampuni ya Frester nikaamua kushukia chalinze na kusahau begi langu lenye computer na vitu vingine. Nikatafuta usafiri mwingine kwenda moro ili kufatilia begi langu lakini mpaka nafika moro
Pole mkuu
 
Kwanini uliposhuka tu chalinze na kugundua umesahau begi hukufanya taratibu ya kuwasiliana na wakala wa frester hapo chalinze akupe mawasiliano ya hilo basi lao lililoelekea Morogoro wakuangalizie begi lako? Pole huna wa kumlaumu ila ww mwenyewe
angepiga simu mapema ingesaidia sana...!! ila kwenda na abiria washashuka hapo ni ngumu mno na alielibeba amedhamiria kuliiba
 
Computer/laptop, simu, vitambulisho, kadi za Benki, nk,
Unakuwanavyo bega kwa bega,
i.e, ukikaa viko mapajani, ukiamka viko begani(bila shaka ndani ya begi).
Kamwe usiweke hata ndani ya sanduku. Kama kupotea viwe detached forcebly from your body(unyang'anywe kwa nguvu)
 
Chalinze Kuna kipi kinachoweza kukufanya usahau begi lenye kompyuta?
Wewe unataka kuharibu sifa nzuri za dereva wa Frester.
(Eti ana demu wake na walilala humo humo, unafikiri mke au watoto wa dereva wakisoma huu uongo watafurahi)
Kwa nini useme ni demu wake? Je Kama ni abiria Kama abiria wengine ameomba hifadhi kwa sababu Hana hela ya gesti?
Usipende kuharibu sifa za wengine kwa uchokoraa wako wa kuwahi vipusa vya Chalinze.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom