Nimeibiwa hela za ofisi na wallet mazingira tatanishi ofisini

Yna aika

JF-Expert Member
Aug 29, 2017
349
1,010
Habari za wakati huu wana jamvi. Nmeona nije uku niandike nitoe machungu ya moyoni maana nahisi kuzidiwa na maumivu.

Nmeibiwa leo asubuhi kazini, hela za ofisi pamoja na wallet yangu iliyokuwa na vitambulisho na hela pia na zimeibwa kwenye hali ambayo nikikueleza ata haieleweki.

Ilikuwa asubuhi ya leo nimefika kazini huwa tuna utaratibu wa kunywa chai kabla ya muda wa kazi kuanza.

Mlinzi wetu aliniomba ruhusa ya kwenda hospitali maana alikuwa anaumwa sana, nikamruhusu mimi nikajumuika na wengine kunywa chai.

Baada ya kama dk 5 au 10 za kunywa chai narudi kwenye meza yangu nakuta droo zipo wazi,nafungua hela hazipo na wallet haipo, kutoka nje kuulizia tunaambiwa wamemuona mtu ameingia na kutoka akiwa amevaa kofia iliofunika sura.

Nikawa nimeibiwa kwa namna io.
 
Najenga picha iyo ofisi ipoje ipoje mtu anaingia, mpaka kwa drawer na kutokomea na vitu
 
Karoge tu bro, haiwezekani mtu akaiba na wameona mtu kaingia na kutoka. Karoge Hali ngumu sana
 
Habari za wakati huu wana jamvi.
Nmeona nije uku niandike nitoe machungu ya moyoni maana nahisi kuzidiwa na maumivu.

Nmeibiwa leo asubuhi kazini, hela za ofisi pamoja na wallet yangu iliyokuwa na vitambulisho na hela pia na zimeibwa kwenye hali ambayo nikikueleza ata
Hujaibiwa na mlinzi aliyekuomba ruhusa ya kwenda hospitali; umeibiwa na mtu ambaye alijua kuwa leo mlinzi ataomba ruhusa kwako ya kwenda hiospitalini. Mtu huyo ni mwenyeji wa mazingira ya ofisini.

Unachoweza kufanya ni kuongea na mlinzi ili uweze kujua ni akina nani alifanya nao maongezi yanayohusiana na yeye kutaka kuja kuomba ruhusa kwako, hasa kwa siku mbili zinazofuatana, yaani jana na leo. Pole sana
 
Mlinzi.. mlinziii ! Mlinziii kuondoka tu mwiz kaja.. ofis inq mazingira rafiki kuingia mtu yoyote!?
Hapana mazingira ya ofisi ni mazingira salama adi sasa sielewi imekuaje maana ni kwa mda mchache tukio limetokea.na watu tulikuwepo ofisini.
Ujasiri alioupata mwizi ndo unanishangaza
 
Dàhhh!mpk kujifunika Uso kajipanga huyo aseehh!pole sana ila maofisini mwetu uaminifu ni sifuri kabisa.ulikosea kuacha droo wazi.natumai utakua umejifunza kitu!

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Hujaibiwa na mlinzi aliyekuomba ruhusa ya kwenda hospitali; umeibiwa na mtu ambaye alijua kuwa leo mlinzi ataomba ruhusa kwako ya kwenda hiospitalini. Mtu huyo ni mwenyeji wa mazingira ya ofisini. Unachoweza kufanya ni kuongea na mlinzi ili uweze kujua ni akina nani alifanya nao maongezi yanayohusiana na yeye kutaka kuja kuomba ruhusa kwako, hasa kwa siku mbili zinazofuatana, yaani jana na leo. Pole sana
Ahsante sana mkuu.
Inawezekana pia ni wake wa karibu waliomuona au aliowaaga kua anatoka
 
Habari za wakati huu wana jamvi.
Nmeona nije uku niandike nitoe machungu ya moyoni maana nahisi kuzidiwa na maumivu.

Nmeibiwa leo asubuhi kazini, hela za ofisi pamoja na wallet yangu iliyokuwa na vitambulisho na hela pia na zimeibwa kwenye hali ambayo nikikueleza ata haieleweki.

Ilikuwa asubuhi ya leo nimefika kazini huwa tuna utaratibu wa kunywa chai kabla ya muda wa kazi kuanza.
Umeibiwa shilingi ngapi nikusaidie kupunguza deni!?
 
Pole Sana Kuanzia leo uache kunywa chai.
Ofsi yako hauna sehem salama Zaid ya kutunza hela aisee?
 
Back
Top Bottom