Nimeibiwa gari na majambazi nyumbani, msaada tafadhali

smarte_r

JF-Expert Member
Nov 8, 2013
2,668
2,000
Sasa usilazimishe kila mtu awe na primitive na immature mind kama yako. Mtu kakua toka kwao magari yapo mengi tu ya kutosha, ko gari kitu cha kawaida sana yani. mimi mtu mzima sahv namiliki gari zangu still ntakua na hio akili ya kijinga ya kupiga picha gari? Prestige my foot. Hayo mambo ya kupiga picha na magari ni mambo yenu nyie wasukuma na wamasai baada ya kununha gari.
.
giphy.gif
 

babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
8,549
2,000
Kama ni gari ndogo ndogo tunaweka begani tunaondoka nayo .

Anyway, tukirudi kwenye mada kwanza nampa pole madau aliyeibiwa. Inauma sana jasho lako la miaka kadhaa kupotea ndani ya dakika kadhaa.
Chakufanya: Omba msaada kwa jiirani wa karibu ambae amefunga cctv camera kwenye njia zinazoeelekea kwako. Hii itakupa picha kuwa ilielekea upande gani. Kisha anza kufuatikia upande huo ukiwaulizia walinzi wa magetini wa usiku. Kama ulikuwa na simu ndani ya gari au kama waliiba simu, ni starting point nzuri sana kujua ilipo au wahusika.
Kama walikuja na funguo zao, itakuwa walichongesha copy ya funguo zako na hao watakuwa ni watu wa gereji au carwash iliyo maeneo ya karibu na kwako(wanaofahamu unapoishi).
Kama una mlizi au kuna kijana alikuwa mfanyakazi wako na ukamfukuza au akaacha kazi kamata huyo abanwe vizuri.
Kama hujuwepo nyumbani wakati tukio linatokea, chunguza uliokuwa nao au anayefahamu ulikuwa wapi, inawezekana aliuza ramani.
Ashasema alitoa funguo in gun point kuwapa majambazi.
 

bravocharlie

JF-Expert Member
Feb 1, 2020
485
500
Hata usijisumbue na huyo mzee anaekwambia huwa anazima switch ya mafuta ukiwekewa pipe kichwan unanyoosha maelezo had ulipoficha kadi yako ya clinic ukiwa mdogo
hii ni hatari sana,unaona kuna uhitaji wa kujipendekeza kwa kaka jambazi
 

mtozatozo

Member
Sep 25, 2021
49
125
Duh aiseee pole sana. I hope umeshatoa taarifa kitu cha polisi na tayari wameshaweka macho maeneo yyote ambayo gari inaweza pitishwa ndani ya muda huu.....

Unaweza tupatia details zaidi kuwa gari ulipaki wapi katika hilo eneo, wewe ulikuwa wapi na ilichukua muda gani kugundua umeibiwa.

Ufunguo uliweka wapi?!

Ndani ya hizi siku kadhaa nyuma ni maeneo gani uliachia ufungua kwa mtu yaani funguo hukuwa nazo mikononi mwako ?!

Haya maswali yatatoa mwanga tujue namna ya kukushauri cha kufanya.
Wezi original wa magari hawasubiri funguo yako wakatoe copy
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom