Nimehuzunishwa: Msome Mwandishi Athumani Hamisi kisha Chukua Hatua Kumsaidia

mwaJ

JF-Expert Member
Sep 27, 2007
4,074
2,947
Habari ni ndefu lakini naomba msome mpaka mwisho. Si maneno yangu bali nimeileta kama ilivyo. Ninatumaini watakaoguswa watamsaidia.
ATHUMANI HAMIS AONGELEA MUSTAKABALIWA MAISHA YAKE NA AOMBA MSAADA

Athuman Hamis.jpg

ATHUMAN HAMIS alikuwa ni mpiga picha katika vyombo vya habari tofauti na alipata ajaliya gari iliyopelekea kushindwa kufanya kufanya kazi na bado anaugua anaishi kwa kulala na kukaa kwenye kiti chake maalum sababu anasumbuliwa na Uti wa mgongo(Spinal Cord).

Athuman Hamis 2.jpg

Mimi Athumani Hamisi Awali ya yote, napenda kuwasalimia wote, wakubwa na vijana wenzangu Hii itakuwa mara ya pili kuongea nanyi waandishi wenzangu, ndani ya miaka minne tokea nipate ajali Septemba 12, 2008 eneo la Kibiti Mkoani Pwani nikiwa na wenzangu Herry Makange ambaye kwa sasa ni marehemu na Anthony Siyame, tukiwa njiani kwenda Kilwa mkoani Lindi kikazi. Mara ya kwanza niliongea nanyi 2010 baada ya kurejea kutoka Afrika Kusini nilikopelekwa na Serikali kwa matibabu.

Shukrani zangu za awali, zimwendee Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete aliyenitembelea katika Hospitali ya Muhimbili nilikolazwa na kuagiza nilipelekwe nje kwa matibabu zaidi. Katika ajali ile, nilivunjika shingo na ku-damage spinal cord iliyopelekea kupooza mwili wote kuanzia shingoni. Katika operesheni iliyofanywa na madaktari wa hospitali ya Mil Park, Afrika Kusini walilazimika kuunganisha shingo kwa nyuma.

Shukrani za pili ni kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kampuni ninayofanyia kazi ya magazeti ya serikali, wachapishaji wa Daily News, Sunday news, Habari Leo Jumapili na Spoti leo, familia yangu iliyokuwa katika wakati mgumu wakati huo hadi sasa watanzania wote waumini wa dini zote waliokuwa wakiombea Pamoja na marafiki zangu waliokuwa wakihangaika huku na kule kwa namna moja ama nyingine.

Niko mbele yenu leo kuwaomba mnifikishie ujumbe kwa jamii kwa maelezo yafuatayo:-

Ofisi yangu ya TSN ilinipangia nyumba ninayokaa Sinza Vatican, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mei 2010-2011 na mkataba ulikukwa kati ya mwenye nyumba na TSN ambao mimi sikuwahi kuuona hadi ninavyoongea na nyie leo. Mkataba uliishatena Mei 2011, mwenye nyumba alikwenda TSN kuomba kusaini mkataba mpya. Badala yake aliandikiwa mkataba mpya wenye jina langu na kupewa aniletee mimi nisaini. Nilipomuuliza mkataba wa kwanza uliingia na nani na ni nani alisaini. Alisemani TSN walisaini wakamwambia wana mgonjwa ambaye ni Staff wake atakuja kuishi pale akitokea Afrika Kusini alikokwenda kwa matibabu.

Mwenye nyumba akasema walimwambia gharama za nyumba ni za TSN, sasa nashangaa leo wameandika jina lako na mkataba ni kati yangu na wewe.

Nikamwambia kaka, mimi sikutarajia kufikia hapa kwani mwaka 1999 ilipangwa mimi nifikie katika nyumba ya kampuni Upanga kuepusha gharama na ukaribu wa huduma za kitabibu, mpaka masuala yangu yatakapothibitishwa na Daktrari kama hali yangu itaruhusu mimi kuweza kufanya kazi ama vinginevyo. Rudi ofisini mkasaini kama mlivyofanya awali. Na umwambie kwa hali ya Athumani hawezi kusaini mkataba na mimi kulingana na hali yake. Isitoshe mi nilitiliana saini mkataba wa awali na TSN.

Ukweli nilikataa kusaini zaidi ya mara tatu, mpaka Meneja Mwajiri (siyo huyo wa sasa) alipoingilia kati na kunithibitishia kuwa kampuni italipa nyumba mpaka uamuziwa madaktari utakapotoka, saini mimi nitakulinda.

Niliporejea nyumbani nikawekwa wino katika dole gumba wakaweka saini. Mpaka yalipojitokeza ya sasa.

Ndugu waandishi wa habari, hali yangu japo imeimarika zaidi kuliko awali, leo nimekuja na jambo ambalo litahusisha jamii na nyie ndiye wahusika Wakuu katika suala hili.

KIKUBWA ZAIDI LEO NI SHUKRANI NAOMBI

Ukweli ulio wazi, nashukuru kwa Mungu na kujivunia kuwa TSN. Nimelelewa na TSN kwa miaka sita sasa. Imenilea nikiwa mgonjwa kwa miaka mine, nikiwa bado niko ndani ya ajira jambo ambalo ni gumu sana sehemu nyingine. Imelipa nyumba kwa miaka miwili na imesitisha kulipa kodi ya 2012-2013 kwa barua ya Februari 3, 2012 na kutoa maelezo kwenye barua kuwa imefikia hatua hiyo kutokana na kuwapa wafanyakazi wake asilimia 15 ya mishahara yao kulipa nyumba.

Nyumba walionipangia ni ya vyumba viwili na kodi iliyolipwa kwenye mkataba wa mwaka jana ni Milioni 4.8 Nilipatwa na mshutuko kidogo, nafsi ikanishauri niite menejiment nyumbani tushauriane katika hili.

Walikuja Machi 28, na wakanipa pole ya kampuni tokea nirudi 2010 Shs 50,000. Lakini mazungumzo hayakuisha kutokana na muda na kuahidi kurudi wiki inayofuata kwa mazungumzo zaidi. Nimepewa notisi na mwenye nyumba April 23, 2010. Nadhani kutokana na kubanwa na kazi, hawakupata nafasi ya kurudi tena kumalizia mazungumzo. Kwa mtazamo wa kifikira ni wazi msimamo ulibaki palepale. Barua ya kusitisha kulipa kodi haikuja kwangu tu bali pia mwenye nyumba alipata.

UFAFANUZI

Kabla ya kuruhusiwa kurejea nyumbani Tanzania, Netcare Rehabilitation Hospital, wana utaratibu mzuri sana. Kabla ya kuwa discharged wanakuruhusu ukae nje ya hospital kwa miezi mitatu, kama una mke au mume na kama huna utatafutiwa nurse awe wa kike ama wa kiume mimi nilipata nurse. Baada ya hapo una hudhuria mazoezi na vipimo kadhaa kwa miezi mitatu. Ukifaulu kumaliza miezi mitatu wewe na mwangalizi wako hasa wewe mgonjwa bila kupata matatizo, hapo wanaku-discharge.

Nilipiga simu kwa Katibu Kiongozi Ikulu wakati huo, Philemon Luhanjo na kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii anahitajika nurse kuja kukaa nami nje ya hospital kwa miezi mitatu, je mtanisaidiaje? Kwa kweli jibu lao lilikuwa moja tu hatutatuma nurse kutoka huku, tafuta huko huko, fedha za kumlipa, nyumba ya kulala, chakula na usafiri, andika budget itume haraka tutalipa na wasiliana na ubalozi waje kujua unakaa wapi na fedha zitatumwa ubalozini watakuwa wanakuletea.

Nilipata nurse na miezi mitatu ilipokaribia kwisha nilifanya mawasiliano kujua kama kutatumwa mtu wa kunifuata, wakanijibu njoo naye huyo huyo watanzania waliofanikiwa kuangalia vyombo vya habari wengi walimuona kwani nilirudi Mei 28, 2010.

Baada ya mwezi alimaliza mkataba na kutakiwa kutafuta nurse wa kukaa naye kwa saa 24. Akapatikana na akafundishwa na M-South Africa jinsi ya kukaa na mgonjwa wa Spinal Cord. TSN, wakamlipa nurse wa South Africa Rand 12,500 alizokuwa anadai na palepale nikauliza vipi kuhusu malipo ya nurse mpya ambaye ataachwa na mimi? Kwa sababu serikali imemaliza jukumu lake na waliniambia kwa kuwa wewe bado ni mwajiriwa wa TSN, jukumu lote sasa utakuwa chini yao na ndiyo mmepewa pia jukumu la kumlipa kama mlivyofanya leo. TSN walinijibu palepale kuwa suala la kumlipa nurse ni lako na familia yako ila nyumba tutalipa.

Vodacom walijitokeza kubeba gharama za tiketi nilipopata ajali kwenda Afrika Kusini na wasindikizaji wote, tiketi ya nurse niliyekuja naye. Pia wakalipa tiketi yangu na nurse Desemba 8, 2010 kwenda na kurudi Afrika Kusini kwa ajili ya check up.

Baada ya TSN kulipa nurse yule msouth afrika, nikawapigia Vodacom Foundation kuwa nurse amemaliza mkataba na ameshalipwa fedha naomba mumkatie tiketi. Hivyo ilikuwa Juni 25 na kesho yake Juni 26 2010 jioni wakaja watu wawili kutoka Vodacom Foundation na mmoja kutoka TSN waliniambia wamekuja na vitu vitatu. Wakamshukuru nurse kwa kazi nzuri, lakini wakamwambia, sisi ni kutoka Vodacom. Vodacom Foundation inakuomba uendelee kumhudumia Athumani. Na Vodacom watakulipa mshahara lakini tunaomba upunguze kiwango.

Yule nurse akakubali akapunguza nusu ya mshahara aliokuwa akilipwa na serikali. Wakamwambia sasa Vodacom Foundation inakata tiketi ya kwenda nyumbani Afrika Kusini kuaga. Akaomba siku 15, mkataba wa mdomo ukakubaliwa na yule nurse na mshahara wa kwanza ukawa Julai 2010 kuendelea na kazi chini ya Vodacom. Julai 2010 wakamlipa. Kilichoendela naomba nisiseme.

Muda wa checkup ulifika Desemba 2010, nikaitaarifu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Wakakubali wakaandika barua kwa kugawa majukumu. Afya wakasema watalipa gharamaza matibabu, Vodacom tiketi za kwenda na kurudi na TSN waliagizwa kulipa allowance kwa mgonjwa na nurse. Tukasafiri Desemba 8, 2010 na tukarudi Februari 28, 2011. Malipo yaliyofanywa na TSN kidogo ni aibu naomba nisiseme. Hali hiyo ilinionyesha kuwa Vodacom Foundation walikuwa wanatambua uwepo wa yule nurse. Lakini hadi nurse anaondoka alilipwa mshahara mmoja tu na hata tiketi ya nurse kurudi Afrika Kusini Vodacom hawakulipa.

Nililipa tiketi ya Business Class. Nikampa Rand 4,500 akakataa akachukua Rand 2,500 tu, akaniambia, Athumani nakuacha katika hali mbaya sana. Fuatilia haki zangu na zako, ukifanikiwa utaniambia na Account ya benki, First bank nakuachia utaniwekea. Vodacom Foundation hawajawahi kupokea simu yangu na Mkurugenzi wake hajawahi kupokea simu yangu wala kuongea na mimi tokea nipate ajali.

Suala lingine waliniuliza nichague kitu kimoja, kujengewa nyumba au kusomeshewa watoto. Mimi nilichagua kujengewa nyumba. Walichukua chaguo langu. Tukamaliza mazungumzo. Baada ya mwezi waliniambia suala lako limekubaliwa ila tumepata Mkurugenzi mpya, lakini usijali. Mpaka hapa ninavyoongea danadana ziliendelea mpaka ninavyoendelea kwenye nyumba, sijawahi tena kupata jibu kutoka Vodacom. La mwisho nilijibiwa na mmoja wa watu wa Vodacom Foundation aliniambia wewe uliingia mkataba na kampuni ya One Plus na si Vodacom Foundation.

SIKU YA LEO Nimekuja kuutangazia umma hali ilivyo. Ukweli kwa sasa Account ya CRDB ilikuwa maalumu kwa ajili ya kusomeshea watoto, imekauka ya Postal bank ambayo ya mshahara haina kitu. Pesa ya mshahara inayoingia benki ni 450,000 Nawalipa nurse, msaidizi wake na mfanyakazi 370,000. Maisha ya ulemavu ni ghali sikutarajia. Nina wanangu watatu, wa kwanza anamaliza darasala saba mwaka huu, wa pili yuko la nne na wa mwisho yuko la pili. Hawa wanasoma primary za kulipia wote hawa nawalipia 200,000 kila mmoja kwa term jumla 400,000 hizo shule zina term nne kwa mwaka. Gharama chakula, vifaa vya wanafunzi, gharama zao ndogondogo na za kifamilia Pamoja na chakula kwa mwezi, inakwenda kati ya 750,000 mpaka 900,000 kwa mwezi.

Nimekuwa ombaomba mpaka watu kadhaa siwalaumu, wamechoka hawapokei simu wala kujibu sms. Siyo siri ndugu wote wamekimbia waliobaki ni marafiki wa kweli wameniingiza katika familia zao. Hali yangu ni mbaya sana kiuchumi. Sina uwezo wa kulipa nyumba kwa gharama zozote zile.

Mimi Athumani Hamisi, naomba watanzania watakaoguswa wanisaidie. Kubwa nyumba na ushauri wa madaktari walinishauri nisiishi mbali na mazingira ya hospitali kulingana na hali yangu. Makampuni, mashirika, wizara yoyote, shirikala nyumba la Taifa NHC, watu binafsi, serikali na Taasisi yoyote watakaoguswa na kilio changu nawaomba wanisaidie kwa njia yoyote. kwa waliotayari naomba misaada ipitie katika account No 01J2027048800 ya CRDB na Account No 010-00090488 ya Postal Bank Kwa wanaotumia mitandao ya simu, wanaweza kutumia M-pesa 0757 825 737, Tigopesa 0655 531 188 na Airtel Money 0784 531118; M-Pesa 0767 298 888 ya Chris Mahundi na Airtel Money 0686 710 977 ya Ephraim Mafuru.

Habari kwahisani ya <data:blog.pageTitle/>

Pole sana Athumani. Hivi nini kilitokea mpaka baadhi ya watu wa jf kutiwa kwenye msukosuko?

Pole sana Athumani ndo maana watu wanaamua kuwa mafisadi kwa sababu kama hizo.Asiye kuwepo na lake halipo ndo wanachokifanya hao watu manake wamekusahau kabisa ina uuma kwa kweli

Nimeharibu siku yangu, any way I'll do what is possible :confused2:

Nimeharibu siku yangu, any way I'll do what is possible :confused2:

Pole Ezan hicho ndicho kilichonipata mie lakini nikaona nisiishie kuhuzunika tu nikaamua kuileta huku nanyi muisome na kusaidia panapowezekana.

Last edited by a moderator:
Jambo moja najifunza hapa. Kama kuna mambo muhimu katika maisha, nadhani ni kujiandaa mapema kabisa kimaisha. Matatizo yanayompata Athuman sote tunapaswa kuyatambua na kuajiandaa. Kama kijana una uwezo, jenga nyumba sasa. Usisubiri kesho. Kama athumani angekuwa kajenga, hakika leo angekuwa anahangaikia suala la ada, chakula na matibabu. Hapa kinachotatiza zaidi ni namna ya kulipia kodi ya pango. Vijana amkeni sasa!! Angalizo: Msijiandalie maisha kwa kuwa mafisadi. Tafuteni maisha kwa haki.

Jambo moja najifunza hapa. Kama kuna mambo muhimu katika maisha, nadhani ni kujiandaa mapema kabisa kimaisha. Matatizo yanayompata Athuman sote tunapaswa kuyatambua na kuajiandaa. Kama kijana una uwezo, jenga nyumba sasa. Usisubiri kesho. Kama athumani angekuwa kajenga, hakika leo angekuwa anahangaikia suala la ada, chakula na matibabu. Hapa kinachotatiza zaidi ni namna ya kulipia kodi ya pango. Vijana amkeni sasa!! Angalizo: Msijiandalie maisha kwa kuwa mafisadi. Tafuteni maisha kwa haki.
Mwitongo ushauri wako ni mzuri lakini ni muhimu kufahamu kuwa ajali inaweza kumpata mtu wakati wowote. Athuman alipata ajali kabla hajajenga na wala hilo si kosa lake maana kujenga mtu anajenga akiwa na uwezo wa kufanya hivyo. Tuyaache hayo, je Athuman anasaidiwaje? Hilo ndio suala la msingi kwa sasa. Jaribu kujiweka katika viatu vyake.

Last edited by a moderator:
Mwitongo ushauri wako ni mzuri lakini ni muhimu kufahamu kuwa ajali inaweza kumpata mtu wakati wowote. Athuman alipata ajali kabla hajajenga na wala hilo si kosa lake maana kujenga mtu anajenga akiwa na uwezo wa kufanya hivyo. Tuyaache hayo, je Athuman anasaidiwaje? Hilo ndio suala la msingi kwa sasa. Jaribu kujiweka katika viatu vyake.

Ni kweli, ajali ni ajali, lakini ndugu zangu kuna mipango katika maisha. Bahati mbaya wengi wetu tunadhani kwamba maisha ni kesho, na si leo. Kifo kipo, ajali ipo. Ukilitambua hilo, huwezi kubaki hivi hivi bila kufanya maandalizi. Angalia Kanumba, alikuwa na fedha na jina nene sana, lakini pengine alidhani kuwa angeishi miaka 70. Mungu hakutaka iwe hivyo. Muhimu hapa ni kuanza kujenga palepale unapokutana na fedha. usisubiri kuwa na milioni 200, la hasha! Anza na hizo hizo za kudunduliza. Maisha ni sasa (hapo ulipo sasa), na si kesho!

Last edited by a moderator:
Ni kweli, ajali ni ajali, lakini ndugu zangu kuna mipango katika maisha. Bahati mbaya wengi wetu tunadhani kwamba maisha ni kesho, na si leo. Kifo kipo, ajali ipo. Ukilitambua hilo, huwezi kubaki hivi hivi bila kufanya maandalizi. Angalia Kanumba, alikuwa na fedha na jina nene sana, lakini pengine alidhani kuwa angeishi miaka 70. Mungu hakutaka iwe hivyo. Muhimu hapa ni kuanza kujenga palepale unapokutana na fedha. usisubiri kuwa na milioni 200, la hasha! Anza na hizo hizo za kudunduliza. Maisha ni sasa (hapo ulipo sasa), na si kesho!

Ni kweli unayosema kaka lakini kumbuka ajali haina kinga na kujenga ni majaaliwa pia.

Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD

mwaJ honestly nimehuzunishwa pia!

Seems like complicated issue ... ! I will do something!

Mtu yeyote anaweza kujikuta kwneye situation close realated na hizo and the rest ...!

Last edited by a moderator:
Jambo moja najifunza hapa. Kama kuna mambo muhimu katika maisha, nadhani ni kujiandaa mapema kabisa kimaisha. Matatizo yanayompata Athuman sote tunapaswa kuyatambua na kuajiandaa. Kama kijana una uwezo, jenga nyumba sasa. Usisubiri kesho. Kama athumani angekuwa kajenga, hakika leo angekuwa anahangaikia suala la ada, chakula na matibabu. Hapa kinachotatiza zaidi ni namna ya kulipia kodi ya pango. Vijana amkeni sasa!! Angalizo: Msijiandalie maisha kwa kuwa mafisadi. Tafuteni maisha kwa haki.

Kama si fisadi, ajenge kwa mshahara upi?

Pole sana mpiganaji,nina hakika TSN wamesikia na watajadili kupata muafaka wa kukusaidia zaidi ama la wakuite mshauriane nini hatma yako!!
Na sheria inasemaje!

Pole sana mpiganaji,nina hakika TSN wamesikia na watajadili kupata muafaka wa kukusaidia zaidi ama la wakuite mshauriane nini hatma yako!! Na sheria inasemaje!
Pia nimewaza kuhusu swla la sheria!Pili! Hivi in real sense mtu kama huyo anasaidiwaje ili ilete maana? kumchangia kila siku kwa kumrushia kwenye simu? AU ipi ni njia concrete ya kumsaaidia kwa hali ilivyo sasa?

Pia nimewaza kuhusu swla la sheria!Pili! Hivi in real sense mtu kama huyo anasaidiwaje ili ilete maana? kumchangia kila siku kwa kumrushia kwenye simu? AU ipi ni njia concrete ya kumsaaidia kwa hali ilivyo sasa?
Azimio Jipya ukiliangalia hili suala kisheria utajiuliza maswali mengi sana kuanzia kwenye malipo ya bima - ajali iliyosababisha kupoteza uwezo wa kufanya kazi, suala la kuumia kazini, je? bado yupo kwenye ajira ya TSN? Kama jibu ni ndio je, mwajiri wake anajukumu gani katika kumhudumia mfanyakazi wa aina yake in terms of accommodation (kumbuka amezungumzia nyumba za staff) n.k.

Njia za kumsaidia zaweza kuwa pamoja na hiyo aliyoomba mwenyewe yaani kumchangia pesa. Lakini hii kwa maoni yangu haitakuwa endelevu maana watu hawataweza kuchangia kila mara anapopungukiwa na ndio maana amesema baadhi ya watu aliowategemea wamechoka na hawapokei hata simu zake.

Lengo la kuileta hii habari JF ni kupata michango ya wana JF ya hali, mali na mawazo pia namna huyu ndugu atakavyoweza kutoka katika hali aliyomo. Watu wanaweza kuchangia pesa na hizo pesa badala ya kuzitumia zote ashauriwe namna ya kuzifanyia mradi ambapo pia atashauriwa namna ya kupata wasimamizi wa huo mradi maana yeye katika hali yake hataweza kusimamia na mawazo mengine ya kumsaidia ili mradi aondokane na huu utegemezi mkubwa aliyotumbukia baada ya ajali.

Najaribu tu kufikiria wako wapi wadada na akina kaka wa JF akina Bishanga Saint Ivuga Bujibuji Mtambuzi Pasco Senetor Mwali Preta sweetlady Kipipi kisukari Smile Michelle charminglady BADILI TABIA na wengineo waje wasaidie mawazo yao katika hili.

Huyu amekuwa ni mpiga picha wa muda mrefu wa magazeti ya chama na serikali.
Iweje leo wale waliokuwa wana pozi mbele ya kamera yake wamemtupa?
Ndani ya CCM hakuna urafiki ila kuna unafiki.
Wito kwa Wazalendo wenzangu wote, tusiangalie nyuma, kama tulivyo fanya kwa Sajuki, tufanye leo tena, Tumchangie huyu mwenzetu

@Azimio Jipya ukiliangalia hili suala kisheria kutajiuliza maswali mengi sana kuanzia kwenye malipo ya bima - ajali iliyosababisha kupoteza uwezo wa kufanya kazi, suala la kuumia kazini, je? bado yupo kwenye ajira ya TSN? Kama jibu ni ndio je, mwajiri wake anajukumu gani katika kumhudumia mfanyakazi wa aina yake in terms of accommodation (kumbuka amezungumzia nyumba za staff) n.k.

Njia za kumsaidia zaweza kuwa pamoja na hiyo aliyoomba mwenyewe yaani kumchangia pesa. Lakini hii kwa maoni yangu haitakuwa endelevu maana watu hawataweza kuchangia kila mara anapopungukiwa na ndio maana amesema baadhi ya watu aliowategemea wamechoka na hawapokei hata simu zake.

Lengo la kuileta hii habari JF ni kupata michango ya wana JF ya hali, mali na mawazo pia namna huyu ndugu atakavyoweza kutoka katika hali aliyomo. Watu wanaweza kuchangia pesa na hizo pesa badala ya kuzitumia zote ashauriwe namna ya kuzifanyia mradi ambapo pia atashauriwa namna ya kupata wasimamizi wa huo mradi maana yeye katika hali yake hataweza kusimamia na mawazo mengine ya kumsaidia ili mradi aondokane na huu utegemezi mkubwa aliyotumbukia baada ya ajali.

Najaribu tu kufikiria wako wapi wadada na akina kaka wa JF akina Bishanga Saint Ivuga Bujibuji @Yo Yo Mtambuzi Pasco Senetor p Mwali Preta sweetlady Kipipi kisukari Smile @Ashadii Michelle charminglady BADILI TABIA na wengineo waje wasaidie mawazo yao katika hili.

Najaribu tu kufikiria wako wapi wadada na akina kaka wa JF akina Bishanga Saint Ivuga Bujibuji Mtambuzi Pasco Senetor Mwali Preta sweetlady Kipipi kisukari Smile Michelle charminglady BADILI TABIA na wengineo waje wasaidie mawazo yao katika hili.
Ndio nimeiona hii habari, naninakumbuka kwa usahihi kabisa juu ya ajali hiyo iliyompata mwenzetu.
Mimi sipendi unafiki, ninachoweza kumshauri ndugu yangu huyu ni kujaribu kupunguza bajeti yake......... ingawa wazo hili limechelewa, lakini hata hivyo anaweza kuangalia bajeti yake na kuipunguza.
Kitu cha kwanza ilitakiwa atafute nyumba za bei rahisi kidogo, Kukaa sinza kuna gharama kubwa sana, kwa mfano angeweza kuhamia Mwananyamala karibu na hospitali kwani pale anaweza kupata nyumba nzuri kwa bei nafuu kidogo, pili gharama za shule za watoto nazo zinamkamua sana, najua alikuwa na lengo la kuwasomesha wanae shule nzuri za English Medium, lakini kwa hali yake kwa sasa inabidi ageukie shule za akina Kayumba...... (najua utakuwa ni uamuzi mgumu),
tatu, ajishughulishe na shughuli za kiuchumi, kuna namna nyingi za kujiongezea kipato, kwa mfano kwa kuwa taaluma yake ni mpiga pisha wa magazeti, basi angejifunza uandishi wa makala hata kwa njia ya mtandao na angekuwa anafanya kazi akiwa nyumbani....
kingine labda angetafuta ujuzi wowote wa kazi za mikono, sidhani kama angetangaza kupitia vyombo vya habari kwamba anatafuta mwalimu wa kumfundisha kazi za mikono angekosa.... Naamini angepata na hata gharama za kumlipa wangejitokeza wafadhili....... Kutegemea wafadhili kwa misaada ya kila siku huku ukiwa na maisha ghali ni shida kidogo.....
Naamini kamaatafuata ushauri wangu anaweza kuvuka mtihani huu mgumu.....
Nakumbuka wakati fualni niliwahi kuandika makala kuhusu tajiri mmoja wa kule Colorado nchini Marekani, yeye alimudu kusimama na kuwa tajiri mkubwa nchini humo pamoja na misukosuko ajali alizowahi kupana na kuwa mlemavu kama alivyo Athumani.

Ukitaka kusoma habari hiyo unaweza kubofya hapa:

https://www.jamiiforums.com/jf-chit...dia-zaidi-wale-waliokata-tamaa-ya-maisha.html

Back
Top Bottom