Nimehesabu, Polisi walimpiga Hamza risasi 19 baada ya kuwa ameanguka chini na sio tishio tena kwa usalama

Baadhi ya watu wanaoishi eneo la Upanga mkoani Dar es Salaam, jirani na nyumba aliyokuwa akiishi kijana aliyetekeleza mauaji ya askari polisi watatu na mwingine mmoja wa kampuni ya ulinzi ya SGA pembezoni mwa ubalozi wa Ufaransa mkoani Dar es Salaam wamesema, wanamfahamu kijana huyo kwa jina la Hamza na hawakuwahi kumshuhudia akifanya tukio lolote la uhalifu.

Wamedai kuwa kabla ya kutekeleza mauaji hayo, kijana huyo alisikika mtaani akisema anaenda Ubalozini kutafuta Viza ya kwenda nje ya nchi lakini baadaye wakamuona akiwa anarushiana risasi na polisi.

Kwa mujibu wa majirani hao, Hamza alikuwa kijana mpole na asiyependa kuongea, na wameshangaa waliposikia ndiye muhusika wa tukio hilo lililozusha taharuki.

Katika tukio hilo lililotokea tarehe 25 mwezi huu majira ya mchana, kijana huyo naye aliuawa katika majibizano ya risasi na polisi na watu wengine sita walijeruhiwa.

Jeshi la Polisi nchini linaendelea na upelelezi, ili kubaini chanzo cha kijana huyo kufanya tukio hilo.

TBC imefika katika nyumba hiyo aliyokuwa akiishi Hamza na familia yake na kushuhudia milango ikiwa imefungwa, na kulingana na maelezo ya majirani wa nyumba hiyo familia ilichukuliwa na polisi siku ya tukio majira ya jioni.
 
Police wa Tanzania hawajui kwamba habari ni muhimu zaidi.. ni kweli baada ya kuishiwa risasi alikuwa si threat tena....kulikuwa hamna haja tena ya kumtwanga ya kichwa.

Adui akishanyoosha mikono juu na kuweka silaha chini, huyo muda huo huo anageuka na kuwa shahidi mkubwa mno tena wa thamani kubwa!!

Kwa mfano sasa hivi wangeshajua why ali-target askari tu na si raia.
Hahaaa!!nimemsikia RC, anasema eti isingekuwa rahisi kumkamata akiwa hai kwani ilikuwa lazima auawe tu kwani alikuwa tishio kwa raia!!muda wote ule karibia saa nzima anatamba tu na hakuwa na shida na raia yoyote, hakuwa toshio sana, badaye ndio aje kuwa tishio kwa raia mbona hata baada ya kuanza kushambuliana na askari hakuweza hata kupiga risasi kwenye gari lolote lile pale!???waseme tu pale ndio ufundi wao uliishia, lakini yule alikuwa wa kumkamata akiwa hai kabisa kwani ilikuwa ni sehemu ya wazi kabisa anaonekana!!kwani hata kutuongopea ni ngumu, kuwa alikuwa na kiroba cha mabomu , na silaha za kibailojia!!!
 
Naangaliaga documentary za wenzetu walivyo sharp na wako well traiined,wanawakamata waharifu wazimawazima bila kuua.
Hizi mbulula za bongo zina rukaruka.
Zimezoea kukamata mateja, walevi na waandamanaji,hivyo tu wajuavyo.
Wenzetu wanatumia risasi za usingizi.. wakupiga tu mapema unaanguka na kulala kabisa na wanakuwa, ile kushtuka uko mikononi mwa Polisi
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
Wewe Kwa mfano ndo askari ,ungeaminije kuwa kaanguka Kwa kupigwa risasi na kama angejiangusha je,,bro kila kazi ni ngumu .kuna mtu ukimpa silaha anazimia papo hapo.kwa hiyo msifundishe watu kazi ....
Yaani mimi kwa mafunzo tu ya JKT najua mtu anakuwaje akipigwa risasi, Polisi wasijue, kwamba Polisi wetu vi vibaka wa mtaani wamepewa uniform na silaha kuwa askari?
 
Ulijuaje kama risasi ziliisha kwenye bunduki unazifahamu kanuni za umilikaji wa silaha? Kanuni inasema "muda wote amini silaha ina risasi",kitendo cha adui kunyoosha mikono juu ile ni fighting tactical yakumpumbaza unayepambana naye ndio maana polisi hawakutaka kuamini wakaendelea kumshambulia.Hivyo niwape rai musipende kuleta siasa kwenye mambo ambayo yanahatarisha uhai wa watu,ndugu zetu wamekufa aisee acheni use..

msiwafunze kazi polisi wetu wana mbinu zote za kimapigano ila pale ilikuwa ngumu sana kutumia mbinu ya 'close battle' na ndio maana wakamtanguliza yule askar aliyevalia kirai(mwenye pistol/aliyepigwa na adui).
Kama wewe ni askari basi ni mwuoga mno. Sijasema baada ya kuanguka Polisi walipaswa kumfuata kama kondoo anaenda kuchinjwa. Kama wana mafunzo wangejua, lakini tatizo Polisi wetu ni vibaka tu waliopewa silaha na uniform
 
Unajuaje kama amekufa au hakufa?
Vipi kama alikuwa na bomb?ambapo anasubiri umsogelee then anadetonate?
Au umsogelee then aanze tena kumimina risasi?

Kuna mamia ya possibilities sababu hii ni real life event na sio movie unasoma script.
Ukichangia huyu jamaa ameua wenzake wawili na bila shaka walipanick kwa uoga na hasira.
Pia ukichangia hiki kitu kina concern maisha yao na wao wana makundi ya watu wanaowategemea watoto na familia hivyo kufa kizembe sio option kabisa.

Mkuu narudia tena hii sio movie za james bond au crime shows unazoangalia weekend.
Hii kitu ni uhalisia mtu anamwaga risasi ikikupata wewe ni marehemu hivyo lazima upanic trust me ungekuwa wewe ungekuwa umeganda huku unatetemeka viungo vyote viko disabled na hujui cha kufanya.

Wewe ushawahi kuwa kwenye field yaani highly trained soldier au secret service agent kutoka CIA au MI6 au popote pale hivyo una uzoefu wa kutosha?

Au wewe ni mtu mmoja anayeangalia lots of crime shows na spy movies na hata siku moja hujawahi kusikia mlio wa risasi live zaidi ya kusikia kwenye spika hivyo anatoa opinions na perspectives zake kutokana na alichokiona kwenye tv?
 
Nimeangalia video juu ya tukio la huyu mtu anaetuhumiwa kuua askari, na kuangalia kilichotokea.

Baada ya kuwa amemaliza risazi katika SMG ya pili aliyokuwa nayo na kunyoosha mikono juu, polisi walimpiga risasi ambayo ilimfanya aanguke chini. Hakukuwa na haja tena kuendelea kumpiga risasi mtu ambaye amejeruhiwa kaanguka chini.

Alipokuwa amejeruhiwa na kuanguka chini, Polisi waliendelea kumpiga risasi akiwa amelala chini ambazo nimehesabu na kukuta walimpiga risasi 19. Ajabu ni kwamba kundi lote lile la Polisi walifanikiwa kumpiga pale tu alipoishiwa risasi na kuonyesha wazi alishaamua kufa - maana alijifanya target rahisi sana.

Sasa hili lina maana gani? Ni wazi kwamba polisi wetu hawana weledi katika matukio kama haya, kwa kuwa baada ya kuwa umeona ameishiwa risasi na si tishio tena, jambo la msingi inabidi kuwa ni kumkamata akiwa hai ili kuweza kupata habari zaidi atakapodhibitiwa.

Kwa hiyo Polisi walipaswa kumkaribia kwa umakini katika formation ambayo kunakuwa na askari wanamsogelea wakiwa na silaha tayari, na wengine waanawa-cover askari wanaomsogelea katika kitu tunaita "flanks".

Lakini pia, kuna upande wa pili, kwamba huenda kuna askari walikusudia kumuua ili huyu mtu asitoe taarifa juu ya ugomvi wake na askari, maana mfu haongei!

Kwahiyo kuna conclusion tatu tu hapa, kwamba polisi wetu wako very unprofessional, incompetent, na pia walikusudia huyu mtu asitoke kwenye hili tukio akiwa hai.


View attachment 1909036
Hii ndiyo Tanzagiza, Kila sehemu ni Dhuluma tu. Kumbe ndio maana polisi wetu wanavitambi visivyoeleweka, kitambi sio kitambi kiroba sio kiroba. Dhuluma tu mwanzo mwisho.
 
Hii thread inatia hasira na kusikitisha kuona raia wenye vitambi juu ya masofa na unene uliopitiliza wakijitia ujuaji kwenye field ambayo wanaiona kwenye tv na movie za james bond huku wakitumia google kama reference.
 
Bomu alitoe wapi wakati inasemekana silaha aliwapora polisi wenyewe
kupora silaha haimaanishi hawezi kuwa na bomu.
Hand grenade unaweza kuweka hata kwenye mfuko wa suruali.

Sasa utajuaje hana bomu?

Last question: una experience yoyote kwenye hii field?
 
Nyie maboya mnapenda kusifiwa tu mkiyatinganya hamtaki kukoselewa nawaamini mgambo 100% kuliko Polisi legelege
Amini unachoamini mkuu.Sasa nyie maboya msitake tutoe siri zenu close battle(cqb)hamuwezi kabisa kilichowakuta huko TANGA ulikisikia? au kilichowakuta nduguzo 'wakunya' pale west gate unakumbuka,polisi ndio walimaliza ile mishe.
 
Habari nyingine kubwa ni polisi kuzidiwa ujanja na teknolojia huru ya simu janja za watu binafsi.

Hakuna chombo rasmi cha habari kilichoweza kuwepo eneo la tukio. Hata skwadi la polisi liliwasili baadaye kidogo. Lakini wajanja tayari walikuwa wakishuhudia na kurekodi live.

Nafikiria isingekuwa hao mashuhuda polisi wetu wangetusimulia hadithi nyingine kabisa. Tungesikia mapambano makali ya piga nikupige kati ya polisi weledi na kikundi cha majambazi. Hata huyo Hamza si ajabu asingetajwa. Au mkuu wa CDM angetiliwa shaka kuhusika.
 
Police wa Tanzania hawajui kwamba habari ni muhimu zaidi.. ni kweli baada ya kuishiwa risasi alikuwa si threat tena....kulikuwa hamna haja tena ya kumtwanga ya kichwa.

Adui akishanyoosha mikono juu na kuweka silaha chini, huyo muda huo huo anageuka na kuwa shahidi mkubwa mno tena wa thamani kubwa!!

Kwa mfano sasa hivi wangeshajua why ali-target askari tu na si raia.
Unajuaje hawajui?
 
Back
Top Bottom