Nimehamia Tabata, tafadhali nipatieni fundi mzuri wa magari

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Nimesogea mitaa ya Bata, Tabata. Wadau gari yangu ni Toyota mbele chini inagonga. Nilikuwa naishi mitaa flani barabara mbaya sana inagonga kama watu wanapiga ngoma ya mdundiko.

Natafuta fundi mzuri wa kuondoa kelele zooooote za chini kwa bei nzuri, maana fundi wangu yupo Kimara, ni mbali na Tabata. Gari imekuwa haihitaji honi maana toka umbali wa mita 200 tu unaisikia ikipiga vingoma chini.

Tafadhali kama unamfahamu fundi mzuri wa kuondoa milio yote ya mbele chini mwenye bei nzuri tuwasiliane.
😁😁😁😁😁😁

Kawaida ya Watanzania uzi huu ndiyo watachangia na kufurahi sana kuwa maskini tupo wengi. But nikianza waelezea zile gari zangu za ukweli, tayari itakuwa nongwa.

Yaani Watanzania wanapenda sifa za kimaskini kama hizi.
 
Toyota gani? Nenda machinga complex pale wanazijua gari za japan na bei nafuu na spare unanunua hapo hapo mwenyewe.'
 
Ni Toyota model gani mkuu? Kuna dogo yupo tabata chama kuelekea Mawenzi, kuna garage inaitwa "Peter Gearbox", yupo vizuri kwa gari za Toyota.
Hahahaaaaa Mkuuuu umeniwahi maaaana mimi pia ndio Garage yangu happo kwa Peter ni uhakika ingawa vijana wake baadhi wamejitenga na kufungua vijiwe vyao.

All in all thats the best place kwa gari za Toyota. Ila tumshauri Peter awarudishe kundini Oscar na Mgabho ili kazi ionekane.
 
Hahahaaaaa Mkuuuu umeniwahi maaaana mimi pia ndio Garage yangu happo kwa Peter ni uhakika ingawa vijana wake baadhi wamejitenga na kufungua vijiwe vyao. All in all thats the best place kwa gari za Toyota. Ila tumshauri Peter awarudishe kundini Oscar na Mgabho ili kazi ionekane.
Hahaha, mkuu pale ndio kila kitu. Kuna dogo ni rafiki yangu sana anaitwa Ali, fundi mzuri sana...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom