Nimeguswa na ubunifu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), nawapongeza na kuwataka waongeze ubunifu

Naona ni bata mwanzo mwisho🤣
20210723_214457.jpg
20210723_214508.jpg
20210723_214511.jpg
20210723_214500.jpg
 
Jumapili ijayo, klabu za Simba na Yanga zinapambana kwenye mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho almaarufu kama Azam Conf. Cup. Mchezo huo kabambe ambao unabeba tukio kubwa la kisoka nchini utapigwa kwenye uwanja wa Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma.

Katika kuchagiza na kusherehesha mechi hiyo ya watani wa jadi, Shirika la Reli nchini (TRC) imeandaa safari ya treni kwa ajili ya mashabiki wa Simba na Yanga kuanzia Dar es Salaam hadi Kigoma na kurudi katika hali ya ubunifu. Safari husika itafanyika leo (?) na kurudi ni Jumapili baada ya mechi.

Ndani ya treni husika kutakuwa na michezo ya aina mbalimbali kama drafti huku watanzania wapenda furaha wakijumuika kubadilishana mawazo na 'kusahau' shida zao wakati wa kwenda na kurudi. Kitu pekee kinachppaswa kuzingatiwa safarini ni hatua za tahadhari dhidi ya maambukizi ya UVIKO.

Kwa moyo wangu wa dhati, nawapongeza TRC. Nawaomba na kuwahamasisha kubuni mambo mengine mazuri kwa ajili ya watanzania na maendeleo ya Shirika la Reli kwa ujumla.
Wasafi tulishafanya hii kitu na hatukuwa na kelele kama hizi
 
Baada ya dakika 90 za mchezo na matokeo kujulikana, washabiki wa Simba na Yanga watasafiri katika treni hiyo moja yenye mabehewa kadhaa ya timu moja yakitenganishwa na yale ya timu nyigine au zitakuwa treni mbili za Simba na Yanga?.
 
Huo ubunifu umetoka kwa Joseph Kusaga wa Clouds media
TRC miaka yote hawajui usafi wala fummigation ya mabehewa ila Kusaga anajua kutumia fursa na kampuni yake kuwa sehemu ya mradi huu
Yeah ubunifu mzuri,ila sio vyote anafanya kusaga,Kuna watu wapo pale clouds na hawana umaarufu sana
 
Jumapili ijayo, klabu za Simba na Yanga zinapambana kwenye mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho almaarufu kama Azam Conf. Cup. Mchezo huo kabambe ambao unabeba tukio kubwa la kisoka nchini utapigwa kwenye uwanja wa Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma.

Katika kuchagiza na kusherehesha mechi hiyo ya watani wa jadi, Shirika la Reli nchini (TRC) imeandaa safari ya treni kwa ajili ya mashabiki wa Simba na Yanga kuanzia Dar es Salaam hadi Kigoma na kurudi katika hali ya ubunifu. Safari husika itafanyika leo (?) na kurudi ni Jumapili baada ya mechi.

Ndani ya treni husika kutakuwa na michezo ya aina mbalimbali kama drafti huku watanzania wapenda furaha wakijumuika kubadilishana mawazo na 'kusahau' shida zao wakati wa kwenda na kurudi. Kitu pekee kinachppaswa kuzingatiwa safarini ni hatua za tahadhari dhidi ya maambukizi ya UVIKO.

Kwa moyo wangu wa dhati, nawapongeza TRC. Nawaomba na kuwahamasisha kubuni mambo mengine mazuri kwa ajili ya watanzania na maendeleo ya Shirika la Reli kwa ujumla.
Mikusanyiko isiyo ya lazima

Mbaya zaidi na pombe juu

Pale ni covod spreading agents Tu
 
Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba Officials Wa TRC waliohusika kwenye huu mchongo wamelamba kwanza 10% kabla hawajaridhia.

Trust me, hii ni akili ya Clouds Kwa asilimia 99.9. TRC wamekuwa watekelezaji tu.
Na usambazaji wa covod pia clouds wanahusika vizuri Sana

Sijui kama.tunaliangalia hilo
 
Mi nina hamu ya kutoooo

Ndani ya behewa
 
Attachments

  • VID-20210724-WA0041.mp4
    2.7 MB
Watanzania ni nai alituloga? Hili nalo ndilo linaitwa ubunifu? Kusafirisha washabiki wa mpira kwenda kwenye mechi ndiyo ubunifu? Hakika nchi yangu inaangamia kwa kukosa watu weledi
Sidhani kama utaelewa ubunifu uliofanyika hapo. Endelea kunywa double kick
 
Back
Top Bottom