Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,196
- 25,515
Jumapili ijayo, klabu za Simba na Yanga zinapambana kwenye mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho almaarufu kama Azam Conf. Cup. Mchezo huo kabambe ambao unabeba tukio kubwa la kisoka nchini utapigwa kwenye uwanja wa Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma.
Katika kuchagiza na kusherehesha mechi hiyo ya watani wa jadi, Shirika la Reli nchini (TRC) imeandaa safari ya treni kwa ajili ya mashabiki wa Simba na Yanga kuanzia Dar es Salaam hadi Kigoma na kurudi katika hali ya ubunifu. Safari husika itafanyika leo (?) na kurudi ni Jumapili baada ya mechi.
Ndani ya treni husika kutakuwa na michezo ya aina mbalimbali kama drafti huku watanzania wapenda furaha wakijumuika kubadilishana mawazo na 'kusahau' shida zao wakati wa kwenda na kurudi. Kitu pekee kinachppaswa kuzingatiwa safarini ni hatua za tahadhari dhidi ya maambukizi ya UVIKO.
Kwa moyo wangu wa dhati, nawapongeza TRC. Nawaomba na kuwahamasisha kubuni mambo mengine mazuri kwa ajili ya watanzania na maendeleo ya Shirika la Reli kwa ujumla.