Nimeguswa na tukio la Kanisa la Mtume na Nabii Mwamposa kuhusishwa na vifo vya waumini 20

Mwamposa ni mhuni kama kina Gwajima ambao wanawahadaa wajinga watoe sadaka lkn sadaka hiyo haiendi kufanya jambo lolote la ki Mungu ila inaishia kuliwa na hawa matapeli.
Tangu lini kiongozi wa dini akauza maji madhabahuni?
Nashangaa watu kama Mwamposa wanapewa kibali cha mkutano wa kuwaibia wananchi lkn Zito kabwe ananyimwa kibali cha kuongea na wananchi wake
Hayo ndio maajabu ya nchi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiacha mambo ya kibali na ulinzi, ipitishwe sheria kali kabisa kama rwanda, kama huna shahada ya theolojia katafute pa kufanya mikutano nje ya tanzania.
Wasalaam wanajamvi

Nimeguswa na tukio la Kanisa la Mtume na Nabii Mwamposa kuhusishwa na vifo vya waumini 20 katika viwanja vya Ushirika Moshi. Nimeguswa kwakua Mimi ni muumini wa waamini (wale wenye imani ya uwepo wa nguvu kubwa inayohitajika kuyaongoza maisha yao).

Aidha nimezisikia kauli mbili toka kwa Waziri mwenye dhamana ya Ulinzi wa Mambo ya Ndani, Mh. Ndugu George Simbachawene akipigilia msumari kwamba Mtume Mwamposa anayo kesi ya kujibu kwakua alitiroka baada ya ibada na kuacha msala (hili mheshimiwa sio kwamba alitiroka hii ndio staili yake ya kuondoka kwenye ibada)

Aliongeza kwamba hata kibali kiliruhusu kuanzia saa 6 hadi 12 ilihali tukio limetokea saa 1 kwenda 2 usiku.

Pia nikasikia kauli ya Mama Anna Mgwira akishutumu kwamba utaratibu huu si wa kiimani bali biashara kwakua kila huduma inayopatikana pale inauzwa iliwepo maji, mafuta na hata kiti unachokali unalipia na kuongeza kwamba anakwara na fungu la kumi pia na akatoa pendekezo ficho kwamba imani zilizo thabiti ROMAN CATHOLIC, KKKT, na zinazofanana zitoe aina ya masomo ya kuwaongoza hawa Viongozi wa Kiroho.

Aidha aligusia swala la wao kuwa na bodigadi as if ni Marais wa nchi Jambo hili litizamwe upya.

*********************

Kwanini napendekeza Jambo hilo BUSARA itumike.

Iman aina yeyote haikai akilini bali moyoni hivyo kuongozwa na hisia zaidi kuliko uhalisia ambao hupatikana katika akili pekee baada ya kuchanganua.

Wale makumi kwa maelfu wanaoenda kukanyaga mafuta hawazitumii akili zao kwa kua imani haikai huko.

Watahoji uko wapi Uhuru wao wa kuabudu. Labda unaweza kujiuliza tangu lini vifo ikawa sehemu ya ibada, tuwakumbushe ya Kibwetere.

Uhuru ambao ni haki yao kikatiba, na kwa hili la UHURU WA KUABUDU nilitwishe mzigo huu serikali na kulichukulia tukio hili kama ajali tu na ifikie Sasa makubaliano ya uwepo si wa kibali tu, bali na Ulinzi wa polisi wakati wa mikutano yao.

Wasalaam

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom