Nimegundua zilikotumika zile trioni walizoiba mawaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimegundua zilikotumika zile trioni walizoiba mawaziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by QUALITY, Apr 27, 2012.

 1. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wana JF
  baada ya gazeti la Mwananchi la Alhamisi iliyopita kuanika kiasi cha fedha zilizoibwa na mawaziri wa JK, nilianza uchunguzi wa chini kwa chini kujua kiasi hicho kikubwa cha fedha kinaweza kuwa kimetumika namna gani.

  Nimegundua kuwa fedha ziliibwa mwaka wa uchaguzi ambapo tarifa za ndani zinasema kuwa zimetumika kwa:-

  1. Kuchapa T-shirt zilizogawiwa nchi nzima
  2. Kuchapisha Kofia za CCM
  3. Kutengeneza skaf walizogawiwa akina mama nchi nzima
  4. kutengeneza vitenge na Kanga za CCM
  5. Kuweka mabango makubwa na madogo nchi nzima
  6. kutengeneza viatu na soksi za CCM kwa wapiga kampeni katika uchaguzi wa 2010
  7. Kutengeneza opener za soda na bia kwa ajili ya kusherehekea ushindi wa kishindo wa Kikwete
  8. Kuhonga wapiga kura katika maeneo mengi ya nchi hii.
  Na ruzuku ilikuwa haitoshi.

  nawasilisha
  Ni mimi Quality
  :A S-heart-2:
   
 2. Ngoromiko

  Ngoromiko JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 559
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Acha kuhangaika na upepo ambao ulishapita.
   
 3. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu, upepo haujapita. Bado wananyukana. Subili jasho la damu!! :crying:
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  sio upepo bali watanzania wanasahau haraka jambo muhimu!hiyo ndio tafsiri ya kikwete
   
 5. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Teteteteteeeeeeee! Umenikumbusha ile kauli ya Nape kwamba siasa inahitaji timing. Sikuamini macho na masikio yangu, yaani karne ya 21 mtu bado ana mawazo ya kuendesha nchi kwa timing badala ya akili ya kisayansi, na kweli jasho la damu liko karibu kuvuja!
   
 6. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Uchaguzi wa 2010 CCM ilitumia fedha nyingi sana katika kampeni na hakika ilikuwa ni gharika ya matumizi,kwa sisi wataalamu wa mambo ya fedha na uchumi ni wazi CCM vyanzo vyake vya mapato sehemu kubwa ilikuwa wizi serikali na ndio maana hata leo nchi imeongeza deni la taifa kwa 38% hadi trilion 14 na ufisadi wa wazi katika idara na wizara za serikali.Kama JK aliweza kupata fedha kwa ajili ya uchaguzi kihalali kwa nini leo ashindwe kupata fedha kama hizo kuendeshea serikali yake ambayo hivi sasa iko taabani kibajeti.
  1.Umepunguza nafasi za ajira na promotion za watumishi.
  2.Halmashauri ziko hoi na madiwani hawalipwi posho zao.
  3.Inakopa fedha kwenye mabenki ya kibiashara badala ya kuuza dhamana zake maana hazina tija sasa kwa taasisi za fedha(low interest rate and no demand at all.
  4.Wakandarasi wa miradi ya ujenzi wamegoma kuendelea na ujenzi wa miradi ya barabara kama Kahama-Rusumo,Namtumbo na deni la Bilion 400
   
Loading...