Nimegundua ya kuwa mimi ni mwendawazimu kwa kuamini kura yangu itaniletea maendeleo

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Ni kutokana na ufahamu wangu "potofu" sana kuwa kujiandikisha kupiga kura kwa matarajio ya kwamba eti kura yangu italeta mabadiliko.

Akili imekataa kuamini kama huu ni uchaguzi na sio maigizo ya uchaguzi.Kweli hapa najihisi nina wendawazimu

Kwanini ninajihisi nina wendawazimu?

Naam,hisia zangu kama si sahihi,basi kinyume chake kuna wendawazimu wengi sana wako kwenye siasa za upinzani.

Hivi ni kweli wapinzani waliamini kuna uchaguzi ambao wanaweza kushiriki na kushinda?

Baada ya yote yaliyotokea,bado kuna watu walikuwa wana imani kuwa mambo yako sawa tu?

Wanadhani wananchi wamesahau watu hawa walivyojitoa katika vyama vyao ili kuunga mkono juhudi?

Asee kama bado yupo mtu anaamini kuna mpinzani atatangazwa mshindi,basi imani hiyo ni kubwa kiasi cha kuhamisha 'milimA'

Na kama mi hivyo basi lile swali ya Yesu kuwa "mwana wa Adamu atakapokuja duniani ataikuta imani kweli?" Mi nasema ataikuta.
 
Huyu jamaa kuna kila dalili ya kutaka kupitisha agenda yake ya kuwa wa milele na milele.Kama umeelewa malizia amina.
 
Mfumo wa chama cha mapinduzi ulisukwa vizuri na Genious Nyerere kuhakikisha kua matakwa ya mfumo dunia Kwa maana ya vyama vingi na demokrasia havitakiathiri chama CCM.

Hata hivo Kura yako ni muhimu Sana kuhadaa dunia kua kuna Demokrasia.

Ni muhimu kiihadaa dunia kwakua Demokrasia ya kweli haiwezi kwamua mataifa machanga bali kuyadidimiza,
Lakini tusipokaa ndani ya mfumo dunia madhara ni makubwa Sana.
Rejea matokeo ya 20/80 ya w.p wananchi kuhusu vyama vingi lakini Mwalimu akaamua minority vote ya kuruhusu vyama vingi nchini tznia

Hivo usishangae yanayotokea si Kwa bahati mbaya ni Kwa maslahi mapana ya taifa letu pendwa,Kulikinga na wanyanganyi (mabeberu) wanaoweza tumia mianya ya Demokrasia kutuamlia mifumo Kwa malengo ya unyonyaji kutokana na uchanga wa mataifa yetu,

Hata hivo siungi mkono brutal means. Kwani naamini 'Humanity first'

*Haya ni mawazo na mtazamo binafsi
 
Sio wewe tu kuanzia mbowe ,zito sipunda na wanachama wote ambao vyama vyao vimejitoa ni watagundua kuwa ni wendawazimu tu.


State agent
Wendawazimu ni wewe na mama zako waliokata majina ya wapinzani uku wanajua wao kushinda kwao ni zaidi ya lazima
 
Huyu jamaa kuna kila dalili ya kutaka kupitisha agenda yake ya kuwa wa milele na milele.Kama umeelewa malizia amina.
Siwezi sema amina kwa sababu ni mwanadamu na ana kifo kinamsubiri atakufa tu.hana umilele wowote.
 
Back
Top Bottom