Nimegundua wenye magari aina moja (yanayofanana) na akili zao hufanana wakiwa barabarani

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Ni kama logic ya kipuuzi lakini ukweli ndo huo!
Wenye Gari zinazofanana wawapo barabarani hata akili zao hushabihiana na kufanana halafu Mara nyingi wao kwa wao wanapendana sana!
  1. Tazama kwa makini wanaomiliki harrier tako la nyani hawapendi kukaa nyuma, atapambana hadi akupite ndo furaha take
  2. Tazama wamiliki Wa IST wana viherehere vya kuchomekea halafu wabishi/viburi kama bodaboda (inferiority)
  3. Tazama wanaomiliki CAMI hawanaga makuu, halafu ni wapole na niwaelewa sana
  4. Tazama wanaomiliki Subaru wanavyopenda sifa sasa kama wahaya
  5. Tazama wanaomiliki land cruiser hawana mbwembwe barabarani they act matured
  6. Wanaomiliki Crown wanapenda kuzuga kama wakarimu kumbe kichwani mwao wanawaza ngono tupu
  7. wanaomiliki alteza mbio nyingi lakini hawana kitu mfukoni mda mwingi wanajaza mafuta ya ten ten n.k
Wenye Gari aina moja hata kuchomekeana kwenye foleni wao kwa wao hawabaniani!

Hii yote ni ishara kuwa wanaakili zinazofanana!
 
Magari n kama mitaa
ukiishi Masaki kuna tabia uta adopt na ukiishi Sinza kuna tabia za watu wa Sinza
uta adopt...hivohivyo ukiishi Tandale

Magari yana kawaida ya kumpa mtu tabia fulani
kama gari ni four wheel obviously hata kwenye rough road hutajali sana
kama wenye vigari vidogo...

Nyumba ikiwa kubwa kuna tabia inakupa na kama ikiwa ndogo kuna tabia
unajikuta nazo...na magari ni hivyo hivyo...
 
umenikumbusha wanaume Wa kinondoni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom