nyumba kubwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2010
- 10,309
- 8,369
- Thread starter
- #81
Hizo sanaa za kulazimisha ndio za wale wanaotulazimisha tucheke wakati hawachekeshi. Sanaa kipaji.
Sasa na wenzangu na mie ambao wanaona sanaa ndio short cut ya maisha ndio wanaishia kushika magitaa mitaani; tena wamesomea miziki lakini hawana uasilia wa usanii.
Sasa na wenzangu na mie ambao wanaona sanaa ndio short cut ya maisha ndio wanaishia kushika magitaa mitaani; tena wamesomea miziki lakini hawana uasilia wa usanii.
Ni kweli sanaa ina uhusiano na uhuru. Kama nilivyosema kwenye posts zangu za juu ni kwamba wengi wa hao vijana wanachukua mengi kwa mama zao ikiwa ni pamoja na mwelekeo wa sanaa. Hawa wanakuwa wamechagua sana kwa uhuru wao; huo ndo mwelekeo wao kutoka ndani ya moyo wao.
Lakini lazima tukubali pia kwamba wapo wanaoweza kwenda kwenye sanaa kama chaguo la pili baada ya kukosa kile walichokitaka katika maisha yao. Na hili si jambo geni, ni jambo la kawaida popte duniani. Mtu unapanga maishani kufanya hiki, lakini unajikuta huna uwezo: wa kifedha, qualification, nk unaamua kuingia kwenye fani nyingine. Hapo hakuna cha ajabu wala cha kushangaa. Kwa hiyo using'ang'anie sana kusema sanaa ni uhuru ukaishia hapo. Wakati mwingine mtu anaweza akaingia huko kutokana na kukosa njia nyingine ya kusonga mbele.