Nimegundua njia mpya ya kubana matumizi nchini

Seneta Wa Mtwiz

JF-Expert Member
Sep 23, 2013
3,622
4,138
Kwenye mada,

Wakuu nchi yetu ipo katika kipindi cha kubana matumizi ili kufanya tusiyumbe kiuchumi,ni jambo bora sana.

Sasa mimi nimegundua njia ya kubana matumizi zaidi,ni katika manunuzi ya baadhi ya mahitaji serikalini.

:Kipengele cha magari,

Badala ya kununua V8s na/au VXs,
Serikali ingeangalia uwezekano wa kununua zile Suzuki_Carry (Kirikuu) kama usafiri mbadala.

Faida ya kununua Kirikuu badala ya Ma_V8 & X ni:

a) Punguzo kubwa sana la bei,
(Bei ya V8 moja waweza kununua Kirikuu 10,
Wajuzi wanaweza kunirekebisha)

b)Utumiaji wa mafuta wa Kirikuu ni mdogo sana ukilinganishwa na wa V8,

c)Kirikuu hutumika kubebea vitu/vifaa vya shughuli mbalimbali na watu pia,
Wakati v8 haiwezi kubeba magunia bali ni watu tu.

Hivyo ningeshauri watu wa procurement serikalini walifikirie na hili,
Ili kupunguza gharama na kuimarisha uchumi wetu.

Ni kwa nia njema tu,
Na si vinginevyo.

Nawasilisha wakuu.
 
hapo unazunguka kama kweli wana nia ya kubana matumizi badala ya kununua magari wakodi magari hata wakilipa laki moja kwa siku kwa mwezi wana uwezo wa kulipa milioni 2 na nusu kwa mwaka milioni 30 kwa miaka mitano milioni 150 kulinganisha na vx 8 kununua milioni 300, mafuta kwa mwezi kiwango cha chini lita 200 mara 1800 laki 3 na 60 mara miezi 12 milioni 4 na laki 3 elfu 20 mara mika mitano milioni 21 na laki 6,mshahara wa dreva laki 2 kima cha chini mara 12 milioni 2 na laki 4 mara miaka mitano milioni 12 service milioni 10 kwa mwaka kima cha chini mara miaka 5 milioni 50 bado gharama nyingine ndogondogo kwa hiyo kukodi gari moja kwa miaka miatano unaokoa magari mawili
 
tunahitaji thread za namna hii ili tuweze kutimiza lengo la Tanzania yetu kujitegemea na kuwa donor country!
 
Back
Top Bottom