joshydama
JF-Expert Member
- May 10, 2016
- 4,623
- 5,037
Habari za asubuhi wakuu. Ni matumaini yangu kwamba hamjambo humu ndani.
Wakuu bila kupoteza muda ni kwamba leo asubuhi nikiwa tumelala, mpenzi wangu ambaye tunatarajia kufunga ndoa mwezi wa tano aliniomba nimsaidie kutengeneza simu yake kwa sababu ilikuwa na matatizo katika upande wa WHATSAPP.
Katika kuitengeneza nimekutana na meseji mbaya sana ambazo zilisababisha nitetemeke mithili ya mtu aliyepigwa na shoti ya umeme. Kiukweli nimejikaza kama mwanaume ili asigundue chochote.
Nikawa nimepiga picha zile meseji kwa camera ya mbele(screenshot) na kujitumia. Ni meseji ambazo zinaonesha few days ago alikuwa guest House na mwanaume. So yule mwanaume alikuwa anaomba wakutane tena pamoja na anakumbushia walivyofanya siku hiyo na kumsifia shemeji yenu kuwa anajua mambo sana.
Kwa muktadha huo hapo juu wakuu. Nipo nae hapa ndani natamani nimmalize kabisa ila roho inasita ingawa hajui kama nishajua usaliti alioufanya. Kiukweli imefikia muda nafsi yangu haitaki kumuona kabisa. Tangu saa tatu nipo tu nimelala naugulia maumivu wakuu.
Je nimpe taarifa au nisubiri mpaka siku ya send off yake nije nimuwekee zile picha za screenshot kama zawadi yake na hapo ndipo utakuwa mwisho wa mahusiano yetu na uchumba wetu?
Je nimtumie meseji hizi ili ajue kwamba nimegundua uchafu wake au nizitume kwa wazazi wake ili wajue matendo machafu ya mtoto wao?
Naomba tupeane uzoefu na mawazo wakuu. Najua wapo ambao watakuja kunikejeli ila it hurts a lot when you do really love someone halafu ana-cheat.
Ahsanteni na karibuni kwa ushauri pamoja na michango yenu wakuu maana nipo katika njia panda japo bado nipo imara sana.