Chakwale
JF-Expert Member
- May 17, 2015
- 1,068
- 1,542
Habari kwenu Wakuu wote
Kichwa cha habari hapo juu kinajieleza
Mimi si muanzishaji wa thread humu ndani bali nimejijengea tabia ya kuwa msomaji na mchangiaji wa Mada mbalimbali pale inapobidi.
Katika uzoefu wangu humu nimegundua ongezeko kubwa la chuki miongoni mwa Wachangiaji katika sehemu zifuatazo:
1.Chuki za Kidini
2.Chuki za Kisiasa na
3.Chuki za kikabila/Kikanda
Hapo namba moja Waislam na Wakristo wamekuwa wakitupiana maneno ya kejeli, dhihaka, dharau ikiwemo mpaka matusi katika kutetea Hoja na Dini zao kiasi cha kuonyesha chuki zao waziwazi dhidi ya dini nyingine kiasi Mtu unajiuliza hivi huyu ndie Mungu anayetaka watu wake wafanye katika kumtumikia?
Ni kheri hata wasio amini uwepo wa Mungu wamekuwa wastahamilivu dhidi ya Imani za wengine zaidi ya kuhoji uwepo wake basi. Hivi nyie Waislam na Wakristo kwanini mnachukiana kiasi hicho?
Hapo kwenye namba mbili ukiingia Jukwaa la Siasa utakubaliana na mimi kuhusu hiki ninachokizungumza. Mtaani tumeshuhudia watu wakitwangwa risasi mchana kweupe, wengine wakipotezwa na wasijulikane walipo na matukio mengine mengi kadha wa kadha.
La mwisho kumekuwa na kutambiana Uchagani, Uhayani, Usukumani, Udar, Wamikoani, nk nk hizi ni dalili mojawapo za kupanda na kupalilia ukabila Nchini kitu ambacho kitakuja kutugharimu mbeleni
Karibu kwa Hoja, Ushauri, Maoni nk
Sent using Jamii Forums mobile app