Nimegundua kuna hatari ya ongezeko la chuki nchini Tanzania

Chakwale

JF-Expert Member
May 17, 2015
1,068
1,542
Habari kwenu Wakuu wote

Kichwa cha habari hapo juu kinajieleza

Mimi si muanzishaji wa thread humu ndani bali nimejijengea tabia ya kuwa msomaji na mchangiaji wa Mada mbalimbali pale inapobidi.

Katika uzoefu wangu humu nimegundua ongezeko kubwa la chuki miongoni mwa Wachangiaji katika sehemu zifuatazo:
1.Chuki za Kidini
2.Chuki za Kisiasa na
3.Chuki za kikabila/Kikanda

Hapo namba moja Waislam na Wakristo wamekuwa wakitupiana maneno ya kejeli, dhihaka, dharau ikiwemo mpaka matusi katika kutetea Hoja na Dini zao kiasi cha kuonyesha chuki zao waziwazi dhidi ya dini nyingine kiasi Mtu unajiuliza hivi huyu ndie Mungu anayetaka watu wake wafanye katika kumtumikia?

Ni kheri hata wasio amini uwepo wa Mungu wamekuwa wastahamilivu dhidi ya Imani za wengine zaidi ya kuhoji uwepo wake basi. Hivi nyie Waislam na Wakristo kwanini mnachukiana kiasi hicho?

Hapo kwenye namba mbili ukiingia Jukwaa la Siasa utakubaliana na mimi kuhusu hiki ninachokizungumza. Mtaani tumeshuhudia watu wakitwangwa risasi mchana kweupe, wengine wakipotezwa na wasijulikane walipo na matukio mengine mengi kadha wa kadha.

La mwisho kumekuwa na kutambiana Uchagani, Uhayani, Usukumani, Udar, Wamikoani, nk nk hizi ni dalili mojawapo za kupanda na kupalilia ukabila Nchini kitu ambacho kitakuja kutugharimu mbeleni

Karibu kwa Hoja, Ushauri, Maoni nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa haya mambo tumerithi kwa nani,yametoka wp
,?
,,mbona waasisi wa taifa letu walitujenga kwenye umoja,amani na upendo,,,
,,,,,MWENYE JIBU ANISAIDIE WANDUGU,,,,,,,
mungu ibariki Africa mungu ibariki Tanzania
 
Fake id's ndo zinawapa watu ujasiri wa kuonyeshana chuki, trust me watu wanaotupiana matusi humu jf kisa dini,kabila au siasa huko mtaani hao watu ni maswahiba tu.
Kwasababu ya kutumia id fake na kutojulikana mtu anadiriki kusema mtuwe Muhammad(SAW) ni mbakaji akiwa na lengo la kuwakwaza waislamu lakini akiwa mtaani huyo mtu hawezi kuthubutu kutamka uduvi huo mbele ya wanajamii, the same to politics, the same to tribalism and regionalism.
Mkuu shusha net ulale there is nothing to fear.
 
Sijaona jipya hapo.. Hata ukisoma comments za miaka 10 nyuma zipo na ubaguzi hivyo hivyo., kikabila, vyama, dini.
Katika jamii haipo siku ambaye tutakubaliana katika hizo itikadi kutokana na asili ya binadamu (egoism).
Sasa sidhani kama ni sahihi sana kusema kuwa sasa kuna haya Mambo, mda mwingne keyboard za jf au mitandao ukisoma unaweza dhani nchi umesimama, kumbe ni maisha kama kawaida na mhaya anataniana na mkurya, msukuma na mkwere na Tanga, mhehe na Mrangi, mpare na mchaga, mnyakyusa, makonde, mgogo n.k.
Kikubwa mtu akilifanya hadharani ni kuendelea kukemea tu.
Na mtu mbaguzi Mimi namuona ni mtu 'primitive sana' kwa kuwa Dunia ya sasa inaishi bila mipaka (social diversity).
Ahsante!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fake id's ndo zinawapa watu ujasiri wa kuonyeshana chuki, trust me watu wanaotupiana matusi humu jf kisa dini,kabila au siasa huko mtaani hao watu ni maswahiba tu.
Kwasababu ya kutumia id fake na kutojulikana mtu anadiriki kusema mtuwe Muhammad(SAW) ni mbakaji akiwa na lengo la kuwakwaza waislamu lakini akiwa mtaani huyo mtu hawezi kuthubutu kutamka uduvi huo mbele ya wanajamii, the same to politics, the same to tribalism and regionalism.
Mkuu shusha net ulale there is nothing to fear.
Mkuu kwa paragraph na mstari wako wa mwisho huo wa "Shusha net ulale nothing to fear "angalau umenishusha presha na khofu juu ya mtazamo niliokuwa nao, lakini kwann tunaendekeza hii tabia? Ili iweje? Kwa faida ya nani? Kumbuka akisemacho Mtu ndicho kilichoujaza moyo wake yaan ndicho kilichomo moyoni mwake..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa haya mambo tumerithi kwa nani,yametoka wp
,?
,,mbona waasisi wa taifa letu walitujenga kwenye umoja,amani na upendo,,,
,,,,,MWENYE JIBU ANISAIDIE WANDUGU,,,,,,,
mungu ibariki Africa mungu ibariki Tanzania
Hakika Mkuu nimekaa na dukuduku hili kwa muda mrefu nimeona angalau Leo Nilitoe,Moyo wangu Unaumia sanaaa ninaposoma kauli za kibaguzi, dhihaka, dharau, Matusi, na kutoheshimiana miongoni mwetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rejea vizuri historia utakuta chuki Za kidini zilianza kujengwa toka huko nyuma
Sasa haya mambo tumerithi kwa nani,yametoka wp
,?
,,mbona waasisi wa taifa letu walitujenga kwenye umoja,amani na upendo,,,
,,,,,MWENYE JIBU ANISAIDIE WANDUGU,,,,,,,
mungu ibariki Africa mungu ibariki Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa paragraph na mstari wako wa mwisho huo wa "Shusha net ulale nothing to fear "angalau umenishusha presha na khofu juu ya mtazamo niliokuwa nao, lakini kwann tunaendekeza hii tabia? Ili iweje? Kwa faida ya nani? Kumbuka akisemacho Mtu ndicho kilichoujaza moyo wake yaan ndicho kilichomo moyoni mwake..

Sent using Jamii Forums mobile app
Binadamu akiwa haonekani anajifanya nunda,mbabe na anaweza kuzungumza chochote ambacho hakiendani na uhalisia wake, lengo ni kutisha watu au kutafuta sifa tu kwa wanamtandao.
Kwa mfano mtu anaweza kuandika hapa jukwaani akihamasisha watu wakachome makanisa na kuua wakristo lakini kiuhalisia unakuta huyo mtu ni muoga sana ambaye hawezi kuchoma hata kuchoma nyumba ya njiwa lakini akiwa hapa atajiita al shabaab wakati hajui hata bunduki inashikwaje.
Watu wengi mtandaoni ni fake 100%
 
Ulicho ongea ni sahihi chuki ujengwa taratibu mpaka inamuingia mtu hakitoka hapa anaenda kufanya vitu ambavyo si sahihi katika jamii
 
Ni matunda ya kukosa Uadilifu, hata katika familia ww km mzazi unapompendelea Mtoto m1 na kupuuza malalamiko ya mwingine bas watoto hao hawatokua na uhusiano mwema maishani.
 
Walivyoanza kufananisha Nairobi na dar nilijua tu watahamia Bukoba na Moshi.. Wakitoka hapo what next? Nini maana na faida zake? Nyerere alisema " SISI WA bara wao wa visiwani... Hii ni dhambi inashuka chini inatafuna. Mijadala ya kulinganisha maeneo kwa maeneo inajenga chuki, uhasama, wengine kujiona bora zaidi ya wengine hasa pale wanapotukanwa maeneo yao etc.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Mimi huwa ninajisikia vibaya lakini kwa Tz ni vigumu kuja kuuana kwa chuki za kidini kwa sababu familia nyingi za kitanzania zina mchanganyiko mkubwa wa dini. kwa mfano Mimi mama yangu ametoka kwenye familia ya kikirsito na kuolewa kwenye familia wa kiislam kwa hiyo kuanzia bibi ,babu,wajomba,mama wadogo zangu ni wakiristo lakini pia kuna mjomba alisha silimu kutokana ameoa kwenye familia ya kiislam lakini pia mama mdogo wangu mmoja naye ni muislam kwa sababu ameolewa kwenye familia ya waislamu.kwa upande wa baba na penyewe kuna mchanganyiko wa kidini baadhi ya baba mdogo zangu ni wakirsito .Lakini pia watoto wa wajomba na mama wadogo zangu wapo mchanganyiko wa kidini hali kadhalika upande wa baba.mchanganyiko wa familia yangu una hakisi familia nyingi za kitanzania ni familia chache mno ambazo hazina mchanganyiko wa kidini.kwa hiyo tuwe makini na maneno ambayo tuna kuwa tunayaandika.maana mnatuweka kwenye wakati mgumu sana sisi ambao familia zetu ni mchanganyiko.
 
Habari kwenu Wakuu wote

Kichwa cha habari hapo juu kinajieleza

Mimi si muanzishaji wa thread humu ndani bali nimejijengea tabia ya kuwa msomaji na mchangiaji wa Mada mbalimbali pale inapobidi.

Katika uzoefu wangu humu nimegundua ongezeko kubwa la chuki miongoni mwa Wachangiaji katika sehemu zifuatazo:
1.Chuki za Kidini
2.Chuki za Kisiasa na
3.Chuki za kikabila/Kikanda

Hapo namba moja Waislam na Wakristo wamekuwa wakitupiana maneno ya kejeli, dhihaka, dharau ikiwemo mpaka matusi katika kutetea Hoja na Dini zao kiasi cha kuonyesha chuki zao waziwazi dhidi ya dini nyingine kiasi Mtu unajiuliza hivi huyu ndie Mungu anayetaka watu wake wafanye katika kumtumikia?

Ni kheri hata wasio amini uwepo wa Mungu wamekuwa wastahamilivu dhidi ya Imani za wengine zaidi ya kuhoji uwepo wake basi. Hivi nyie Waislam na Wakristo kwanini mnachukiana kiasi hicho?

Karibu kwa Hoja, Ushauri, Maoni nk

Sent using Jamii Forums mobile app
Duu! Imenitokea juzi juzi tu. Nimetukanwa matusi ya nguoni na mjahidina mmoja, sitasahau kwa kweli. Kisa, dini!
Kwa kweli inabidi manabii wetu Jesus Christ na Muhamad warudi tu duniani wapigane weeeeee, atakayeibuka kidedea huyo ndiye tumfuate. Ni ujinga sisi wenyewe kupigana na kuuana eti kwa ajili ya Mudi na Jesus ilhali wenyewe wako na peace!
 
Naomba nianze direct na mada ya uzi. Tangu kuingia kwa Rais Joseph Pombe Magufuli madarakani mwaka 2015, nimefuatilia kwa umakini zaidi nimegundua kwa kadri siku zinavyo kwenda kabila la wasukuma limetokea kuwa linachukiwa na watu wengi kwa kadri siku zinavyosonga.

Nimejaribu kulinganisha na makabila mengine ambavyo Marais waliopita wametoka sijaona hata moja kuchukiwa kwa namna inavyotokea kwa wasukuma. Waangalie Wazanaki, Wamakuwa/wamakonde, Wakwere, sijui Mwinyi ni kabila gani?, yote hayo hakuna anaewajali au kuwa na husda nao, sasa kwa nini watanzania wanawaonaje wasukuma?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom