Nimegundua kumbe kuna umuhimu wa kufunga CCTV camera sakafuni zimulike juu, maana za juu wakati mwingine zinafeli kunasa!

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,276
21,395
Nitawapa mfano;

Maeneo mengi sana siku hizi yamefungwa kamera!

Tembelea MALL zote hukosi idadi kubwa ya kamera!

Lakini ajabu, Pamoja na wingi wa kamera lakini bado ripoti za wizi na udokozi zinaendelea pasipo watuhumiwa kupatikana!

Mazingira ya matukio mengi yanayoripotiwa ukiangalia video (footage) zake zilivyo! Mwizi anaonekana anaingia mchana kweupe bila hata mask usoni lakini hajulikani kwa sura kamwe!

Wanachokifanya wezi kuanzia inje ya jengo, wanatembea wameinama kichwa chini bila kunyanyua kichwa, anaingia ndani katazama chini tu mwanzo mwisho, anatembea huku na kule kichwa chini, kama ni MALL anachukua SIMU, LAPTOP N.K Anaondoka na camera inamsindikiza hadi anatokomea!

Kwahiyo footage ya namna hii inachoambulia ni kumulika rangi za nguo tu! Sasa utamjuaje! Mtu katoka mbali wenye nguo kama zake wapo kibao! Kutambua ni vigumu mno.

Hivyo nadhani kuna umhimu wa kufunga pia CCTV CAMERA ZA CHINI CHINI (sakafuni) ili zimulike kwenda juu kama zipo!!
 
Hivi wale wanaovaliaga sijui ndio hijab/burqa kwani hawaingiagi Malls?

Maana ndio rahisi kuiba sehemu zenye ulinzi wa CCTV.

Kuna nchi zinakataza uvaaji wa hivyo sehemu za public kutokana na masuala ya kiusalama.
Hiyo inawezekana lakini kwa hili la mtu kuangalia chini huwezi kumhoji mtu anyanyue kichwa
 
𝙽𝚒𝚊 𝚢𝚊𝚔𝚘 𝚗𝚒 𝚔𝚞𝚘𝚗𝚊 🇺 🇨 🇭 🇮  𝚝𝚞𝚞
 
Nitawapa mfano;

Maeneo mengi sana siku hizi yamefungwa kamera!

Tembelea MALL zote hukosi idadi kubwa ya kamera!

Lakini ajabu, Pamoja na wingi wa kamera lakini bado ripoti za wizi na udokozi zinaendelea pasipo watuhumiwa kupatikana!

Mazingira ya matukio mengi yanayoripotiwa ukiangalia video (footage) zake zilivyo! Mwizi anaonekana anaingia mchana kweupe bila hata mask usoni lakini hajulikani kwa sura kamwe!

Wanachokifanya wezi kuanzia inje ya jengo, wanatembea wameinama kichwa chini bila kunyanyua kichwa, anaingia ndani katazama chini tu mwanzo mwisho, anatembea huku na kule kichwa chini, kama ni MALL anachukua SIMU, LAPTOP N.K Anaondoka na camera inamsindikiza hadi anatokomea!

Kwahiyo footage ya namna hii inachoambulia ni kumulika rangi za nguo tu! Sasa utamjuaje! Mtu katoka mbali wenye nguo kama zake wapo kibao! Kutambua ni vigumu mno.

Hivyo nadhani kuna umhimu wa kufunga pia CCTV CAMERA ZA CHINI CHINI (sakafuni) ili zimulike kwenda juu kama zipo!!
Rafiki usinge CCTV camera kwa ajili ya kumtambua mwizi, funga CCTV Camera kwa lengo la kukusaidia kugundua jaribio la wizi kabla halijatokea, ikiwa unafunga camera ili kumwona mwizi na kumjua sura utakuwa umepoteza hela zako. Unashauri zifungwe chini ili zianagalie juu na endapo mwizi ataingia akiwa naye kaangali juu je? Funga camera na kuwe na mtu wa kuingalia muda wote, hapo utaweza kuzuia wizi na itakuwezesha pia kumkamata baada ya kutekeleza tukio.
 
Unaifaham PTZ camera vizuri... BTW wizi mipango tu.. mnapanga na controller mnaiba..
Hakuna controller ambaye atakuwa na administrator password na endapo kuna kampuni itakuwa imefanya hivo basi security maneja, risk assessment na It wafukuzwe kazi mara moja , akiamua kuiba siyo kwamba hatoonekana, litakuwa ni suala la muda tu, natambua unataka kusema kuwa controller ataizungusha hiyo PTZ na kuipeleka upande mwingine, uko sahihi. Lakini endapo hilo litawezekana kutakuwa na shida upande wa uwekaji wa camera. Kimsingi maeneo yote ambayo ni high Risk lazima camera ilinde camera nyenzake.
 
Kujua yote hayo ndio mipango yenyewe...ukiiba bila mipango lazma udakwe
 
Nitawapa mfano;

Maeneo mengi sana siku hizi yamefungwa kamera!

Tembelea MALL zote hukosi idadi kubwa ya kamera!

Lakini ajabu, Pamoja na wingi wa kamera lakini bado ripoti za wizi na udokozi zinaendelea pasipo watuhumiwa kupatikana!

Mazingira ya matukio mengi yanayoripotiwa ukiangalia video (footage) zake zilivyo! Mwizi anaonekana anaingia mchana kweupe bila hata mask usoni lakini hajulikani kwa sura kamwe!

Wanachokifanya wezi kuanzia inje ya jengo, wanatembea wameinama kichwa chini bila kunyanyua kichwa, anaingia ndani katazama chini tu mwanzo mwisho, anatembea huku na kule kichwa chini, kama ni MALL anachukua SIMU, LAPTOP N.K Anaondoka na camera inamsindikiza hadi anatokomea!

Kwahiyo footage ya namna hii inachoambulia ni kumulika rangi za nguo tu! Sasa utamjuaje! Mtu katoka mbali wenye nguo kama zake wapo kibao! Kutambua ni vigumu mno.

Hivyo nadhani kuna umhimu wa kufunga pia CCTV CAMERA ZA CHINI CHINI (sakafuni) ili zimulike kwenda juu kama zipo!!
Kwani kukiwa na CCTV huko Malls si pia wanakuwapo "Auxilliary Police" (Walinzi)?

Mbona ukienda kutoa pesa katika ATMs unaombwa kuvua kofia?
 
Men being men loooh....!!

Mmechezesha mbavu zangu kisawasawa, ila na wale wanaume wanaovaa vikaptura tutaona mitulinga ikining’inia 🤣🤣🤣🤣🤣

cc: Leonardo Harold SACO
 
Mkuu zikiwekwa chini zitapigwa spray unaona ukungu tu

Bora kila mteja awe anapewa suma wake wakuzunguka nae akiwa mall
 
Back
Top Bottom