Nimegundua ameni-cheat kwa miaka 3 mfululizo, nifanyaje?

Poleni na majukuu ya ujenzi wa taifa letu.

Nipo kwenye mahusiano na mwanamke kwa muda wa miaka 5 sasa, tumeishi nae vema na tumejaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume hadi sasa japo sijamuoa wala sijamlipia mahari.

Kabla hajawa na mimi kwenye mahusiano, alikuwa ametoka na mshkaji mmoja waliyesoma wote japo mahusiano yao ndio kama yalikua mapya vile, akaja kwangu, nimekaa nae kwenye mahusiano kama miezi miwili, yule first boyfriend wake niliemkuta naye alianza kumsaka tena.

Akarudi kwa boyfriend wake na mm kuniacha, baada ya wiki 2, nikashindwa kuvumilia na nikaanza kumrudisha kwangu na akakubali kurudi kwangu mazima, nikabaki zangu na kinyongo cha kusalitiwa naye kwa kurudi kwa jamaa yake.

Muda wote huo wa mahusiano yetu tulikua nae chuo, nikiwa ya likizo ya semister, nikatongoza mtumishi mmoja wa umma kwa lengo la kulipizia yeye alivorudi kwa jamaa yake, nilimdanganya yule mtumishi wa umma hadi akakubali na akaanzisha mahusiano na mm,

Mahusiano yalidumu kwa kipindi cha miezi miwili ya likizo na siku naondoka akaniambia kuwa anahisi ana mimba, bila kubisha nikajua ile mimba itakuwa yangu, nikaikubali kuilea na kuitunza na wakati huo wote nilikua nimeshamjulisha kuhusu girfriend wangu wa chuo na akakubaliana na hali.

Nipo chuo naendelea na huyu wa chuo wakati kule mtaani kuna mimba inakua na huyu wa chuo hata mimba hana, yule wa mimba akajifungua na muda wote huo sikumwambia huyu wa chuo kua kuna mimba wala mtoto huko.

Baada ya kumaliza chuo, nilisepa na yule girfriend wangu alikua nyuma yangu, kwahiyo akabaki chuo na masomo, nikapata kazi hapa jijini Dar. Yule wa chuo akaja Dar kunisalimia likizo, alipokuja ndipo ilipopatikana mimba ya huyu mtoto wangu niliezaa na mwanachuo.

Aliponipa taarifa ya mimba, nilimuita Dar na nikaona haina haja ya kumficha kuhusu mtoto wa mtaani niliezaa naye, nikamwambia ukweli na kumuomba msamaha, alilia sanaaaa sanaaa na baadae akaniuliza kua mwelekeo wako ni upi, nikamwambia mwelekeo wangu ni kudumu na wewe, tukakubaliana na maisha yakaendelea.

Mimi sina hili wala lile, nakomaa na maisha na kumtunza zaidi mana gharama za maisha zilipanda sana alipopata mimba na kujiandaa kwa ajili ya kujifungua, nikawa nakomaa kidume adi alipojifungua na maisha yakawa poa sana.

Hawa watoto wangu wawili wamefanana sana kama wametoka kwa mama mmoja mana wote wamechukua msura wangu, ukiwaona huwezi hata kuuliza ni wa nani mana wanajionesha kabisa.

Maisha yakaenda, nikawa nakomaa na maisha na binti akamaliza chuo naye akapata kazi dar ila tulikua hatukai pamoja kutokana na mazingira yetu ya kikazi na sababu zilizokua nje ya uwezo wetu ila tulikua tunaonana mara nyingi sanaaaa na kila wikend tulikua pamoja adi wikend inaisha au katikati ya wiki kama tukipata nafasi.

Miezi miwili iliyopita, nilianza kuona kama anabadilika vile, yaaani ile romantic atmosphere ni kama inapungua vile, nkaona kama love inaanza kupwaya vile, nilipanic sana na kuanza kutumia nguvu za pesa na out nyingi ili kurejesha tena, mambo yakagoma.

Nikaanza kufatilia simu yake, nikagundua kuna namba anawasiliana nayo kimaficho sana na kuna siku SMS iliingia nkaisoma tuu kwa juu ila sikufungua. SMS haikua na shida ila alivochukua simu yake na kuirudisha kwangu, ile SMS sikuikuta na kwenye recent calls kulikuwa na missed call za ile namba ila nazo nikakuta kafuta.

Nilizidi kupanick aiseee, ikabidi niichukue ile namba kwa siri na kubaki nayo, niliporudi kwangu, nilianza kuchat na yule jamaa na kumuuliza kama anatoka na mama mtoto wangu, alikataa kata kata na kusema wao ni marafiki sanaaaa na akijua nimemuuliza hivo basi mama watoto wangu hatafurahia.

Jina la yule jamaa nimelisikia sana kwa mwanamke wangu katika matukio ya hapa na pale kwahiyo hata aliposema ni rafiki yake, mie haikunipa shida sana, nikaamini ivo na kuendelea na maisha.

Kile kitendo cha kuchati na jamaa kumbe kilimpa shida sana, wiki mbili baadae alinitafuta tena nilikua nipo kwa mama mtoto palepale, akatuma SMS kuwa najua upo nyumbani muda huu, naomba utoke nje ili flani asisikie ninachokwambia.

Nikatoka moyo ukienda mbio sana, tukaongea kwa simu na jamaa kwa kirefu sana, ikabidi tuonane asubuhi hiyo hiyo na jamaa, tuliongea nae man to man.

Nilijipa moyo wa ujasiri ili nisilie wala nisitetemeka mbele ya jamaa, yule jamaa alimipa stori zote na alikiri kua ni kweli anatoka na mama mtoto wangu.

Akasema walianza kama marafiki na baadaye wakajikuta kwenye mahusiano. Mahusiano yao yameanza mwanamke akiwa na mimba ya wiki chache, maana yake umri wa mwanangu kuanzia mimba ndo umri wa mahusiano yao.

Akasema mama watoto alikuwa amejeruhika kwa sababu mimi nilim-cheat na kuzaa nje, kwahiyo alianza kunitoa moyoni mwake ndiyo mana akaanzisha mahusiano mengine kama kulipiza vile, but mimi ndo nimechangia sana yeye kuanzisha mahusiano mengine.

Kwa hiyo kila nilipokuwa nakutana na mwanamke wangu, jamaa alikuwa anapewa taarifa kuwa mhusika yupo, kwahiyo jamaa anatulia kimya bila kutuma SMS wala kupiga simu hadi nikiondoka ndiyo wanaendeleza tena. Maisha yakawa hivo kwa kipindi chote cha miaka mitatu yao.

Mzigo wa mama mtoto wangu ukawa unaliwa hivo na mapenzi yao bila shaka yamekolea sana mana wamekula out nyingi, nimedanganywa mara nyingi kuwa anaenda kazini kumbe anaenda kwa mshkaji, nimedanganywa kuwa kalala ndani kumbe kalala kwa mshkaji.

Niliumia sana siku ile, jamaa akasema wamejaribu kuachana ila wanashindwa kwa sababu mwanamke wangu ana huruma sana na jamaa akasema njia pekee ya kuvunja mahusiano yale ni kwa kukiri wazi bila kuficha mbele yangu na mbele ya mwanamke wangu. Akaomba turudi kwangu ili akakiri hii dhambi na waiache rasmi.

LAKINI JAMAA AKAJA NA HABARI MPYA TENA, akasema mwanamke wako ameanzisha mahusiano tena na yule boyfriend wake wa kwanza ambae alini-cheat naye tukiwa chuo, hii iliniuma zaidi.

Kufupisha stori, kumbe muda huo tulikua watatu ndani ya mwanamke mmoja.

Nikakubali twende kwa mwanamke, tulipofika jamaa alizungumza na mwanamke na alikiri kuwa ni kweli japo lile la boyfriend wake wa kwanza alilikataa. Baada ya jamaa kusepa, nikambana sana, alilia sana na akakiri kuwa ni kweli alianzisha hayo mahusiano miezi miwili nyuma na ameshalala naye usiku mmoja hadi asubuhi.

Akaomba msamaha na kusema ananitaka mimi, mana alikuwa kwenye utaratibu wa kuachana na jamaa zote ili abaki kwangu.

Nampenda huyu mwanamke, nampenda sana hadi nashindwa kuamua. Je, niendelee naye au nibaki naye? Nipo katikati, lolote linaweza kutokea kutegemeana na ushauri wenu.

Kwa sasa wale wawili kawabwaga, nimebaki mwenyewe kwake, japo nikikumbuka moyo unapasuka ndani yangu.

Sorry kwa urefu wa habari, karibuni kwa ushauri, hata PM pia kama utaona itafaa.


Sent using Jamii Forums mobile app
Kwakweli nashindwa kukushauri..ila ngoja nijaribu..
Kwa uzoefu wangu, naona ndoa yenu haitakua na furaha kabisa..maamuzi magumu inabidi yachukuliwe for the sake of amani ya mioyo yenu..jambo kubwa kabisa linaloletaga mpasuko kwenye ndoa hua ni kukosekana uaminifu halaf ndio na mengine hua yanafuata..cheating katika ndoa huleta machungu na majuto..
So..nashauri KAMA itawezekana mkae chini mkubali kua wote mlikosea na mko tayari kuanza upya katika usafi wa ndoa au mahusiano yenu..halaf pia sijui upendo wenu ni genuine kiasi gani..i mean msingi wa mahusiano yenu..kama kuna ile strong feelings mtasurvive through hii hard time.
 
Hapo wote mlifanya utoto. The best thing you could do ni kumwacha the very first time alipoku cheat. Ungeachana nae tu mangi then ungetafuta mtu mpya ukaanza nae esp. huyo mtumishi kama ulimpenda ungeendeleza nae gurudumu.

"Once a cheater, always a cheater"

Huu ni msemo ambao unaishi na ni halisia kabisa. Guess what, huyo mwanamke unaeona unampenda hastahili huo upendo unaompa maana alishaharibu na lile kosa halifutiki.
 
Its high time mubariki ndoa na muishi kihalali kama mme na mke,yaliyopita sindwele.
Kuchapiwa ni siri ya ndani.
Wake za watu wanachapwa sana walio wengi,sio wakwako ndio anaanza.
 
Back
Top Bottom