Nimegundua ameni-cheat kwa miaka 3 mfululizo, nifanyaje?

Poleni na majukuu ya ujenzi wa taifa letu.

Nipo kwenye mahusiano na mwanamke kwa muda wa miaka 5 sasa, tumeishi nae vema na tumejaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume hadi sasa japo sijamuoa wala sijamlipia mahari.

Kabla hajawa na mimi kwenye mahusiano, alikuwa ametoka na mshkaji mmoja waliyesoma wote japo mahusiano yao ndio kama yalikua mapya vile, akaja kwangu, nimekaa nae kwenye mahusiano kama miezi miwili, yule first boyfriend wake niliemkuta naye alianza kumsaka tena.

Akarudi kwa boyfriend wake na mm kuniacha, baada ya wiki 2, nikashindwa kuvumilia na nikaanza kumrudisha kwangu na akakubali kurudi kwangu mazima, nikabaki zangu na kinyongo cha kusalitiwa naye kwa kurudi kwa jamaa yake.

Muda wote huo wa mahusiano yetu tulikua nae chuo, nikiwa ya likizo ya semister, nikatongoza mtumishi mmoja wa umma kwa lengo la kulipizia yeye alivorudi kwa jamaa yake, nilimdanganya yule mtumishi wa umma hadi akakubali na akaanzisha mahusiano na mm,

Mahusiano yalidumu kwa kipindi cha miezi miwili ya likizo na siku naondoka akaniambia kuwa anahisi ana mimba, bila kubisha nikajua ile mimba itakuwa yangu, nikaikubali kuilea na kuitunza na wakati huo wote nilikua nimeshamjulisha kuhusu girfriend wangu wa chuo na akakubaliana na hali.

Nipo chuo naendelea na huyu wa chuo wakati kule mtaani kuna mimba inakua na huyu wa chuo hata mimba hana, yule wa mimba akajifungua na muda wote huo sikumwambia huyu wa chuo kua kuna mimba wala mtoto huko.

Baada ya kumaliza chuo, nilisepa na yule girfriend wangu alikua nyuma yangu, kwahiyo akabaki chuo na masomo, nikapata kazi hapa jijini Dar. Yule wa chuo akaja Dar kunisalimia likizo, alipokuja ndipo ilipopatikana mimba ya huyu mtoto wangu niliezaa na mwanachuo.

Aliponipa taarifa ya mimba, nilimuita Dar na nikaona haina haja ya kumficha kuhusu mtoto wa mtaani niliezaa naye, nikamwambia ukweli na kumuomba msamaha, alilia sanaaaa sanaaa na baadae akaniuliza kua mwelekeo wako ni upi, nikamwambia mwelekeo wangu ni kudumu na wewe, tukakubaliana na maisha yakaendelea.

Mimi sina hili wala lile, nakomaa na maisha na kumtunza zaidi mana gharama za maisha zilipanda sana alipopata mimba na kujiandaa kwa ajili ya kujifungua, nikawa nakomaa kidume adi alipojifungua na maisha yakawa poa sana.

Hawa watoto wangu wawili wamefanana sana kama wametoka kwa mama mmoja mana wote wamechukua msura wangu, ukiwaona huwezi hata kuuliza ni wa nani mana wanajionesha kabisa.

Maisha yakaenda, nikawa nakomaa na maisha na binti akamaliza chuo naye akapata kazi dar ila tulikua hatukai pamoja kutokana na mazingira yetu ya kikazi na sababu zilizokua nje ya uwezo wetu ila tulikua tunaonana mara nyingi sanaaaa na kila wikend tulikua pamoja adi wikend inaisha au katikati ya wiki kama tukipata nafasi.

Miezi miwili iliyopita, nilianza kuona kama anabadilika vile, yaaani ile romantic atmosphere ni kama inapungua vile, nkaona kama love inaanza kupwaya vile, nilipanic sana na kuanza kutumia nguvu za pesa na out nyingi ili kurejesha tena, mambo yakagoma.

Nikaanza kufatilia simu yake, nikagundua kuna namba anawasiliana nayo kimaficho sana na kuna siku SMS iliingia nkaisoma tuu kwa juu ila sikufungua. SMS haikua na shida ila alivochukua simu yake na kuirudisha kwangu, ile SMS sikuikuta na kwenye recent calls kulikuwa na missed call za ile namba ila nazo nikakuta kafuta.

Nilizidi kupanick aiseee, ikabidi niichukue ile namba kwa siri na kubaki nayo, niliporudi kwangu, nilianza kuchat na yule jamaa na kumuuliza kama anatoka na mama mtoto wangu, alikataa kata kata na kusema wao ni marafiki sanaaaa na akijua nimemuuliza hivo basi mama watoto wangu hatafurahia.

Jina la yule jamaa nimelisikia sana kwa mwanamke wangu katika matukio ya hapa na pale kwahiyo hata aliposema ni rafiki yake, mie haikunipa shida sana, nikaamini ivo na kuendelea na maisha.

Kile kitendo cha kuchati na jamaa kumbe kilimpa shida sana, wiki mbili baadae alinitafuta tena nilikua nipo kwa mama mtoto palepale, akatuma SMS kuwa najua upo nyumbani muda huu, naomba utoke nje ili flani asisikie ninachokwambia.

Nikatoka moyo ukienda mbio sana, tukaongea kwa simu na jamaa kwa kirefu sana, ikabidi tuonane asubuhi hiyo hiyo na jamaa, tuliongea nae man to man.

Nilijipa moyo wa ujasiri ili nisilie wala nisitetemeka mbele ya jamaa, yule jamaa alimipa stori zote na alikiri kua ni kweli anatoka na mama mtoto wangu.

Akasema walianza kama marafiki na baadaye wakajikuta kwenye mahusiano. Mahusiano yao yameanza mwanamke akiwa na mimba ya wiki chache, maana yake umri wa mwanangu kuanzia mimba ndo umri wa mahusiano yao.

Akasema mama watoto alikuwa amejeruhika kwa sababu mimi nilim-cheat na kuzaa nje, kwahiyo alianza kunitoa moyoni mwake ndiyo mana akaanzisha mahusiano mengine kama kulipiza vile, but mimi ndo nimechangia sana yeye kuanzisha mahusiano mengine.

Kwa hiyo kila nilipokuwa nakutana na mwanamke wangu, jamaa alikuwa anapewa taarifa kuwa mhusika yupo, kwahiyo jamaa anatulia kimya bila kutuma SMS wala kupiga simu hadi nikiondoka ndiyo wanaendeleza tena. Maisha yakawa hivo kwa kipindi chote cha miaka mitatu yao.

Mzigo wa mama mtoto wangu ukawa unaliwa hivo na mapenzi yao bila shaka yamekolea sana mana wamekula out nyingi, nimedanganywa mara nyingi kuwa anaenda kazini kumbe anaenda kwa mshkaji, nimedanganywa kuwa kalala ndani kumbe kalala kwa mshkaji.

Niliumia sana siku ile, jamaa akasema wamejaribu kuachana ila wanashindwa kwa sababu mwanamke wangu ana huruma sana na jamaa akasema njia pekee ya kuvunja mahusiano yale ni kwa kukiri wazi bila kuficha mbele yangu na mbele ya mwanamke wangu. Akaomba turudi kwangu ili akakiri hii dhambi na waiache rasmi.

LAKINI JAMAA AKAJA NA HABARI MPYA TENA, akasema mwanamke wako ameanzisha mahusiano tena na yule boyfriend wake wa kwanza ambae alini-cheat naye tukiwa chuo, hii iliniuma zaidi.

Kufupisha stori, kumbe muda huo tulikua watatu ndani ya mwanamke mmoja.

Nikakubali twende kwa mwanamke, tulipofika jamaa alizungumza na mwanamke na alikiri kuwa ni kweli japo lile la boyfriend wake wa kwanza alilikataa. Baada ya jamaa kusepa, nikambana sana, alilia sana na akakiri kuwa ni kweli alianzisha hayo mahusiano miezi miwili nyuma na ameshalala naye usiku mmoja hadi asubuhi.

Akaomba msamaha na kusema ananitaka mimi, mana alikuwa kwenye utaratibu wa kuachana na jamaa zote ili abaki kwangu.

Nampenda huyu mwanamke, nampenda sana hadi nashindwa kuamua. Je, niendelee naye au nibaki naye? Nipo katikati, lolote linaweza kutokea kutegemeana na ushauri wenu.

Kwa sasa wale wawili kawabwaga, nimebaki mwenyewe kwake, japo nikikumbuka moyo unapasuka ndani yangu.

Sorry kwa urefu wa habari, karibuni kwa ushauri, hata PM pia kama utaona itafaa.


Sent using Jamii Forums mobile app
Potezea km unampenda na umwambie ulijua kinachoendelea.lkn kwa sababu unampenda.
Sasa unaogopa kulea watoto wa kambo. Na umri unasonga unataka zaa!
Aamini nakwambia utakufa nae.angalizo usifanye kazi yako kizembe kunako sita kwa sita bila kumfikisha ngazi zote.

MApesa uwe nayo pia, na mpinzani usimsahau mkali kuliko yeye. Mwaga mavitu mazuri mazuri nyumbani kwako kuanzia jikoni sebureni mpaka unapoweka mbavu zako.
 
Kama hukukuta bikra hayo ndio matokeo.

Usimlaumu kwa kukucheat wakati hukukuta bikra. Hiyo ndio tabia yake.

Ungemkuta na bikra usingeumia sana. Bali ungejua ni bahati mbaya. Lakini huyo hata akiomba msamaha. Amini nakuambia atarudia tena na tena
Tena hiyo tabia hata acha kamwe,mwanamke akicheat amechit huyu bwana atamgegeda Tena na Tena ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Potezea km unampenda na umwambie ulijua kinachoendelea.lkn kwa sababu unampenda.
Sasa unaogopa kulea watoto wa kambo. Na umri unasonga unataka zaa!
Aamini nakwambia utakufa nae.angalizo usifanye kazi yako kizembe kunako sita kwa sita bila kumfikisha ngazi zote.
MApesa uwe nayo pia, na mpinzani usimsahau mkali kuliko yeye. Mwaga mavitu mazuri mazuri nyumbani kwako kuanzia jikoni sebureni mpaka unapoweka mbavu zako.
Live vinginevyo atawali mpaka uzeeni mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jamaa bado unampenda Sana huyo mwanamke,,,,kifo chako kitatokea kwa huyo mwanamke ucpokua makini.

Kuna wanawake hata aki cheat na ukajua uwezo wa kumuacha huna...kunakua na chemistry ya ajabu sana...

Mm Kuna manz kitaa Ni kicheche na ninajua wanaomgonga ila huwez amini namm nimo tu...uzuri nikimwambia wkend hakuna kutoka utakua namm tu anakubali...Yuko vzr sana kitandan ila cjui anatumia na dawa maana nashndwa kumuacha kbs.....

Yuko mkoan kwa mama yake ila nimemtumia nauli arudi mjini aendelee kunipa faraja kwa wakati wangu japo najua fika tuko wengi na wengine ni wafanyakaz wenzangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mijitu mingine sijui mna laana au ubongo wenu una mapovu
Kama hukukuta bikra hayo ndio matokeo.

Usimlaumu kwa kukucheat wakati hukukuta bikra. Hiyo ndio tabia yake.

Ungemkuta na bikra usingeumia sana. Bali ungejua ni bahati mbaya. Lakini huyo hata akiomba msamaha. Amini nakuambia atarudia tena na tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I'm not that old (29 years) but in my few years here on earth, I have learnt that a woman cannot respect a man who is fully aware of her past whoring history yet still chooses to settle with her. Hata umnunulie state house.

In her eyes, you are communicating that you are unable to find a higher quality mate or one who is not yet 'tampered' with.

She will reciprocate this in kind by cheating with another man, with or without your knowledge. She knows deep down that she is doing you a favor by staying with you.

Don't be a bozo, cut your losses and bounce.
 
aisee.Mungu nisaidie mm.
pole sana mkuu mm sina cha kukushauri.Umeyataka mwenyewe ,pambana na uhalisia.Usinge cheat mpaka ujisahau na kutia mimba nje, yamkin haya yote yasingetokea. Au pia yangetokea tu kutegemeana na hulka ya mtu.
pole sanaa

NB
Lyrics za NEY WA MITEGO
.....Kudadadeki mapenzi hayashauriki,
kama kweili unampenda, mpende tu maradufu,
ila huku kitaa ,wanamgonga hata kwa buku,
huyo sio demu, ni demu wa kitaa,

huyo sio demu, ni demu wa masela,

aahh ,,nasema huyo sio deeeeeem.

Nyimbo: huyo sio demu
Abdu kiba ft Neybar & Ney wa mitego
 
bro, ilifika kipindi nikataka niende kwao kujitambulisha but alionesha hana bashasha na ile habari, na kusema unakimbilia nini kwani, jipange vzr kwanza, hadi nikashangaa, miez miwili baadae ndo nagundua mali inaliwa nje

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii stor ndio naisoma leo vp bado upo nae? Piga chini malaya huyo
 
Niliichogundua wanawake huwa wanasaidiana sana mmoja wao anapoharibu,Mwanaume unapokuwa na matatizo na mwenzi wako usiombe ushauri uamuzi uko juu yako,Mjinga sana wewe jamaa
 
Msamehe Sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo ndo wazo zuri. Kwanza huyu mwanamke anampenda sana sana kiasi kwamba alikuwa kamficha hao wengine. Tena aliwaratibu vizuri ka ndo ya kiislamu. Akawapa time yao kila mmoja. Nimempenda sana huyu mwanamke.
Hakutaka wakutane ila aliwapa haki yao kila mmoja ila mzalishaji ni mmoja tu. Nimempenda saana
 
" In every action there is equal and opposite reaction "

Hivi hii ni "Newton's law" ya ngapi hii.

Forgive and forget
 
Back
Top Bottom