Nimegombana na rafiki yangu kwa kuniita "MKURYA" mbele za watu

Amani ya bwana itawale kwenu wapendwa,

tujikumbushe kidogo enzi za mwalimu JK Nyerere,Mwalimu alikuwa mstari wa mbele kupinga ukabira pia kumuita mtu kwa kabira lake kama ndo jina lake,mfano we "msukuma njoo hapa" wakati mtu anajua jina lako kamili,

leo hii nikiwa matembezini kwa mbari rafiki yangu ariniita kwa kabila langu mbele za watu,"we mkurya njoo hapa",kwa kweli jambo hiri rinikera sana ukizingatia niko mikoa ya watu ambapo mtu akisikia neno mkurya picha inayomjia kichwani mwake ni mapanga na mishare,pia mimi nilishajitamburisha kwa watu kama msukuma,na watu wote wanajua mimi msukuma ,kwa kweri sikupenda na hivyo nirimkanya jamaa asirudie jambo hiri,kwani rilipelekea kuzua tafrani na watu wote kuanza kuniangaria mimi,

je wapendwa wangu nirikuwa sahihi au nimawazo yangu tu ndo yamepelekea kujinyanyapaa?
Wewe !!! wakati watu wengine kutoka mkoa wa Mara ambao sio Wakurya wakijitambulisha kama Wakurya na kujiita "Poti" ili waheshimiwe na wasionewe ovyo. wewe ndo unajificha na kubadili kabisa mpaka na mkoa !! Haya, ole wako endelea kujificha halafu uone namna utakavyodharauliwa na kuporwa haki yako. Nakwambia mtu yeyote hata awe Polisi akishajua kuwa wewe ni wa asili ya Mara hata kama sio Mkurya, huwa anajongea kwako heshima ikiwa mbele. Mimi kuna siku nilikuwa na-drive, Mrs wangu hajafunga mkanda kwa kuwa alikuwa preg., Polisi akanisimamisha, akazunguka zunguka gari, mimi sikufungua kio, gari iko tinted, Polisi alipokuja dirishani akagonga gonga kio kwa kidole, nikafungua akaniuliza mbona abiria wako hajafunga mkanda ? Nikamuuliza tofauti na hilo, umeona kosa gani lingine ? akasema sijaona lingine, nikamwuliza, sasa umenisimamisha kwa kosa gani maana hilo mpaka nilipofungua kio ndo umeliona hata hivyo, kama unavyomwona huyu hawezi kufunga mkanda, lakini nilijua ni kosa na nilikuwa tayari kwa adhabu yake, akaniomba leseni, akaitazama na kusema kumbe ndo wale wale, nenda bwana akanirudishia leseni. Nikajiuliza, ameona nini ? maana cheo changu hakipo kwenye leseni labda kama ningempa ID, hata hivyo, sipendi kutumia cheo kupinga sheria kuchukua mkondo wake, lakini pia sipendi mimi binafsi au mtu mwingine kuonewa bila kosa, nikajua labda kaona jina ambalo halitaki uonevu ingawa mimi ni wale wa mjini waoga hata wa kuchinja njiwa !!
 
Kuna makabila ukiitwa na mtu mbele ya watu ni aibu.

Kuna makabila ukiitwa mbele za watu unajivunia.

Wale wanao ona aibu ndo hai utawaskia ukimuuliza kabila anakwambia Nyerere alikataa,huyo huyo akiomba Passport,cheti cha kuzaliwa ,Kitambulisho cha Taifa anaulizwa kabila na anataja kwa furaha .

Kweli Mungu tusaidie tujiamini na ubin wetu
 
Naomba kujua ww mleta uzi huu, ni mkurya wa sehem gan, na ni tabaka gan na ni mlango gan, na kama umetahiriwa kwel wewe rika(saiga) lako ni jina gani? ukijibu utakuwa mkurya kwel ila hiyo tabia yakukimbia jina ukurya utakuwa umeambukizwa tu
Tatighana na akalisya kayo ghataghacha kaghotwi mutwe kwansa ghatana isaigha nsibhitali ghasarwe.
 
Nikiitwa muhaya wa BK tena Mulangila nafurahi saaaaanaaaaaah. Hata mtaani wanaponiita wee muhaya naona fahari kubwa sana.
Sasa wewe mtani wangu mkurya wa Tarime sijui Sirari nini kinakusibu mpaka unamwaga magumi ili ukane kabila lako!!!! au unapenda uitwe msukuma uonekane ni wa ukoo uliopo mitaa ya Magogoni hapa Dar????????????????? Acha Ushamba MRAAAAAAAAAAAAAHHH
 
wakurya hatunaga asili ya kukataa/kukana kabila letu coz ni ngumu kukuta mkurya akijiitia majina yote ya mkoloni na mostly huwa tuko proud na ukurya wetu mfano mm kazini kwangu wananijua wafanyakazi wenzangu wote kutokana na kuwa mkurya hvyo huyu ni limbukeni mmoja aliyekaririshwa kwamba kuwa mkurya ni kutokuwa na letter 'L' na yeye kwa kushikiwa akili akakimbia kuja kupost hvyo hvyo humu jf.
 
sijawai ona mkurya anae ikana asili yake isee... chunguza vzr ndugu huenda kuna mistake ilitokea wewe sio wa ukuriyani
 
Jivunie kabila lako acha ujinga wa kumnukuu nyerere vibaya plz usirudie ujinga huo. Nakuita mjinga sio kukutukana maana utasema nimekudhalilisha hapana, mjinga ni mtu ambae hujui anachosema ila akipate Elimu dunia tu atakuwa mwelewa hivyo basi mjinga sio mpumbavu maana mpumbavu hana ajifunzalo. Mi mwenzio mhehe na popote nafahamika hivyo na ukiniita am so proud
 
Amani ya bwana itawale kwenu wapendwa,

tujikumbushe kidogo enzi za mwalimu JK Nyerere,Mwalimu alikuwa mstari wa mbele kupinga ukabira pia kumuita mtu kwa kabira lake kama ndo jina lake,mfano we "msukuma njoo hapa" wakati mtu anajua jina lako kamili,

leo hii nikiwa matembezini kwa mbari rafiki yangu ariniita kwa kabila langu mbele za watu,"we mkurya njoo hapa",kwa kweli jambo hiri rinikera sana ukizingatia niko mikoa ya watu ambapo mtu akisikia neno mkurya picha inayomjia kichwani mwake ni mapanga na mishare,pia mimi nilishajitamburisha kwa watu kama msukuma,na watu wote wanajua mimi msukuma ,kwa kweri sikupenda na hivyo nirimkanya jamaa asirudie jambo hiri,kwani rilipelekea kuzua tafrani na watu wote kuanza kuniangaria mimi,

je wapendwa wangu nirikuwa sahihi au nimawazo yangu tu ndo yamepelekea kujinyanyapaa?
Nahisi ubongo wako unashida
 
Back
Top Bottom