Nimefurahishwa kwa nilicho kutana nacho kwa askari wa barabarani

Konte

Member
Jul 26, 2017
86
130
Habari zenu na hongereni kwa majukumu!

Siku tatu zilizopita (Ijumaa ya Eid) nilipata safari ya kutoka Mwanza kwenda Musoma na baadaye Tarime, siku mbili baadaye (Jumapili) nilirudi kwa njia hiyo hiyo nikiwa na gari binafsi.

Wakati wa kwenda baada ya kupita Magu nilipigwa mkono na traffic na kuambiwa pamoja na kuoneshwa speed niliyokua nakimbia nayo, nilikua nimezidi 50Km/h kama inavyotakiwa kutembea eneo hilo kutokana na vibao vinavyoelekeza. Sikuandikiwa faini badala yake alinipa onyo la hiyo speed na kukagua kama gari ina madeni ya nyuma na kunitakia safari njema.

Nikaendelea na safari na nilipofika maeneo ya Kalemela ikawa vivyo hivyo kama ilivyokua hapo nyuma. Nikapewa onyo na kukaguliwa madeni ya nyuma na kutakiwa safari njema.

Wakati wa kurudi Mwanza nilipofika Lamadi niliovertake lori moja sehemu ambayo haikua sahihi kufanya hivyo, askari walikua kama mita 200 mbele waliona na nikapigwa mkono na kupewa onyo na kutakiwa safari njema.

Kimsingi makosa yote yalikua ni sahihi kwa maana ya kwamba hakuna niliposingiziwa. Safari nyingine ambazo huwa nasafiri njia hiyo sijawahi kupewa onyo badala yake ni kuandikwa faini tu.

Kwa uzoefu wangu mdogo wa highway ni nadra sana kupata onyo zaidi ya moja kwenye njia moja bila kupewa adhabu ya faini.

Sijajua kama huo ndiyo utaratibu mpya au ni wiki tu ya elimu na huruma

Nimefurahishwa sana na ninatoa pongezi kwa mamlaka husika kwa hicho nilichokutana nacho.

Kila la kheri.
 
hapo wamekusamehe kutokana na aina ya gari uliloliendesha na namba pia
unafikiri ungekuwa na T100 AAX wangekuacha pesa ya kubrush viatu
wao kukaa juani kuna maana yake
sisi hatukatizi mpaka tutakapoendesha mapya
 
Mkuu askari wamekuwa tofauti na wewe kuwa tofauti.

kwanini baada ya kupewa onyo usiwe mwelewa? kwanini upewe onyo 3times? Unakiri kabisa uli overtake kwenye dangerous area kwanini unaatarisha maisha yako?

Tuache lawama tubadilike
 
Sidhani kama gari ni sababu ya kutokuandikiwa faini, ndani ya hii miezi miwili nimepita hiyo njia na gari hilo hilo mara tatu go and return hii ya juzi ni ya nne. Sikuwahi kupewa onyo huwa ni faini tu
 
Mkuu nilitereza tu, sijalaumu na nimekubali kubadilika. Nilichojaribu kushare ni huo utofauti wa askari wa kuelimisha na kutoa onyo na si kuadhibu moja kwa moja.
 
Mkuu huoni kwamba comment zako mbili zina kinzana?
Unaonekana ww ni dereva usiyejielewa na the way kukueleimisha lazima upigwe fine tu. Badilika mkuu kama una safari na sio emergency panga muda wako vizuri
 
Unawakumbusha ili wa-develop software ya ku-track hata warnings? Wana click, "show warning history in the past 6 months" halafu inaleta history inasema "two warnings within the past 2 hours". Tunaelekea huko!

Sikulifikiria hilo, ni idea nzuri japo faini ya ambaye ameshaonywa itakuwa ni kubwa kuliko ambaye anaadhibiwa kwa mara ya kwanza
 
Mkuu huoni kwamba comment zako mbili zina kinzana?
Unaonekana ww ni dereva usiyejielewa na the way kukueleimisha lazima upigwe fine tu. Badilika mkuu kama una safari na sio emergency panga muda wako vizuri

Awali nilikua na mtazamo tofauti kwa hawa askari, hizi warnings zimenibadilisha.
NIMEBADILIKA
 
Askari huwa hawasimamishagi wakiona Vieite,Mkonga au Range Vogue!! Wakiona una screpa linaolotembea lazima upigwe mkono.
 
Askari huwa hawasimamishagi wakiona Vieite,Mkonga au Range Vogue!! Wakiona una screpa linaolotembea lazima upigwe mkono.
tunamwambia Konte anatubishia kuna baadhi ya gari hawajisumbui nazo tunamuuliza ni gari aina gani anayotumia?
Vi Hiace na Coaster utamuona konda anashuka bila shuruti anamfuata Traffic hizi gari za abiria hazikamatwi pia
 
Nikisema ni gari gani nadhani aibu itazidi kuwa kubwa acha tusubiri kuwashiana tu taa barabarani
 
Wewe inaelekea ni dereva mkorofi..Maonyo matatu kwenye bara bara moja....?

Inaeleka miezi mitatu baadae, utaonywa na IGP..

IGP anakwambia nyumba nyingi DAR hazina Mapanga au Mashoka ya kujilinda yaani ndani utakuta makochi,TV na "SABUFA".
 
Imani yao ya huruma moyoni itakuwa ilizidi siku hiyo.
Sidhani kama inawezekana kwa askari mmoja mmoja waingiwe na huruma ya kufanana kwa kipindi kimoja. Pengine ilikua ni huruma ya askari mmoja kutoka juu hao niliokutana nao wakawa wanaideliver tu.
 
Sikulifikiria hilo, ni idea nzuri japo faini ya ambaye ameshaonywa itakuwa ni kubwa kuliko ambaye anaadhibiwa kwa mara ya kwanza
Actually Askari waliofuatia waliokuwa wanamsamehe, ukiacha yule wa kwanza (baada ya yule wa kwanza), wote walikuwa wanadhani kuwa amefanya kosa kwa mara ya kwanza siku hiyo, na kwamba hakuna kosa jingine alilofanya siku hiyo kabla ya wao kuwa wamemkamata. Ni kwa sababu hawana software ya ku-detect frequency za warnings mtu alizowahi kupata ndani ya kipindi fulani. Wanayo software ya ku-track faini tu ambazo mtu anaweza kuwa ameshapigwa na hakuwahi kuzilipa. Kwa hiyo kwa thread hii, huyu mtu anawakumbusha wafanye marekebisho kidogo tu kwenye ile application software ya ku-track fine alizopigwa mtu, watengeneze auxilliary application nyingine ya ku-track warnings na kutunza warning history.

Nachelea kusema kuwa mwaka huu unaweza usiishe kabla hawajaitengeneza application hiyo. Huyu mtu aliyeanzisha thread hii, anaweza kuwa ni Askari ambaye ameamua anonymously kutoa ushauri kwa mamlaka za juu za Trafifc Police
 
Mkuu askari wamekuwa tofauti na wewe kuwa tofauti.

kwanini baada ya kupewa onyo usiwe mwelewa? kwanini upewe onyo 3times? Unakiri kabisa uli overtake kwenye dangerous area kwanini unaatarisha maisha yako?

Tuache lawama tubadilike
Good, kupewa onyo zaidi ya mara moja ni wazi na wewe hufuati sheria, wao wakiamua kuifuata inakua shida tena
 
Back
Top Bottom