Nimefurahia maamuzi kesi ya Mbowe, Mungu mkubwa atatenda

Tulianza awamu ya tano tukapiga makofi wapinzani walipofilisiwa na kufunguliwa kesi tukiamini tunakijenga chama. Tulipomalizana nao tuliamia kwa wana CCM nakuwachapa kuanzia kwenye fikra Hadi kwenye akaunti zao. Leo Wana CCM wote waliokuwa na nguvu ya kiuchumi wamefilisika, au wamekufa kwa presha na baadhi wamepoteza madaraka.

Kwanini yamewapata hayo? Ni kwa sababu waliamua kuishi maisha ya Mwenye nchi badala ya kuishi maisha yao. Wapo watu kwa uzembe kabisa bila kujali elimu zao waliumizwa kisa tu wanamwelekeo na mawazo tofauti. Lakini pia wapo watu walitumia nguvu za kibinadamu na dola kutesa wengine wakiamini zamu yao itadumu Sana. Pole kwao maana Mungu alipangalo si la wanadamu.

Tukamaliza harakati za awamu ya tano, walioamini wapo salama wakageuziwa kibao nakuondolewa kwenye nafasi zao Kisha kukalishwa kimya. Kwa frastration wakanzisha Hadi madarasa ya uongozi na wengine kujifanya wataalamu wa afya kupinga chanjo ya COvID19 lakini leo wote wamenyamazishwa na wanatakiw kuongea lugha moja na waliyedhani Hana nguvu.

Lakini ni Jambo kubwa kwamba unapopanga kuwanyoosha na Mungu naye anapanga ratiba yake, unapotumika kuwanyoosha na Mungu naye anapanga ratiba yake. Akina Rwegamalila waliishi utumwani kwa uvumilivu wakiaminishwa kwamba hakuna namna wanaweza kurudi uraiani lakini Leo wale wote waliokuwa wanawakandamiza awapo kwenye nafasi zao na wengine hata Duniani awapo.

Wapo watu wachache Sana nimeona wanashangilia maamuzi ya kesi ya Mbowe, lakini madhara ya maamuzi haya Ni makubwa Sana kwa wanyonge wa nchi hii. Ninaposema wanyonge simaanishi kwamba watu wasio na fedha Bali namaanisha wale wote ambao maamuzi haya yanawaruhusu kuteswa na dola na bila kuhojiwa. Mfano mkubwa ni utata wa kifo Cha dreva wa kampuni ya Dangote ambapo maelezo ya Polisi yaliyotolewa kila mtu ameyatilia mashaka lakini kile walichotamka Polisi ndicho kinachoishi.

Siyo hayo, tumeshuhudia machinga wakijaribu kufanya fujo karikoo lakini uongozi wao leo wamejitokeza na kusema wale siyo machinga bali Ni wahuni na imepita hivyo. Usidhani Kiongozi wa machinga anappsema Yale aliyoyasema hajui ukweli wake Bali ndivyo amabvyo tunaishi. Kwamba Mwenye kusema hiki ni sawa na si sawa ni serikali.

Niseme wazi kwamba tunaposhangilia maamuzi ya Jaji ambayo hayana hata kifungu Cha sheria kinachoonyesha msingi wa maamuzi yake Basi tutambue kwamba hii siyo huku ya Mbowe. Ni hukumu yakuigwa na mahakama zetu nyingi nchini. Tukumbuke ipo siku Kama ilivyozoeleka kwa miaka mitano viongozi na watu wenye ushawishi ndani ya CCM ambao Sasa hivi wanaona dola na mahakama Wana ndoa nzuri ndoa hiyo itawaathiri wao na famililia zao.

Nimalizie, Makonda aliteuliwa na JK kabla yakuteuliwa kuwa RC na JPM. Lakini ni Makonda huyo huyo wakati anataka kuonyesha ana nguvu alisau mambo yote Jk na familia yake waliyomfanyia na kumtangaza Riz one kwenye skendo za madawa ya kulevya bila hata kutoa ushahidi wowote. Lakini pia wazee wa CCM wasiwe wepesi wa kusahau namna ambavyo wao na familia zao walinyanyasika, mateso waliyopata hayakuzongatia tuhuma zilizothibitika Bali yalijikita kukomoa.

Maamuzi ya Jaji Siyani ambayo yanafuatia uendeshaji wa kesi huku muda wa Azana kesi ikiwa inasimamishwa kumheshimu Mungu itufumbue macho kwamba hawa watu tunaowashangilia ndio hao hao wanaotafuta kututawala wanapokuwa mafichoni au sirini. Tufurahie maana tunamwona Mbowe akiwa anapita mateso lakini naamini vijana waliopo naye kwenye kesi wana wazazi kama ambavyo qatoa maamuzi Wana wazazi.

Tukumbuke Kama baba Riz alivyoumia mwanaye kutajwa kwenye madawa ndivyo wazazi, mke na watoto wa watuhumiwa wanavyoumia wanapogundua muda wakusubiri vijana wao wawahudumie watu wachache ambao Sasa hivi usiku huu wapo wanastarehe na familia zao, wanaitwa Dad na Mom, wanaulizia mshahara utatoka lini wameamua bila sababu yoyote kuakikisha kwamba vijana wale wanateseka na may be wanakufa ili wao malengo yao yatimie.

Mungu aishiye anaweza akanyamaza kwa machozi ya familia hizi kwa muda ila atonyamaza milele. Tunaposherekea ushindi uluotolewa na Jaji leo Ni vyema pia tukaandaa nafsi zetu kupokea maamuzi ya mwenyenzi Mungu dhidi ya watuhumiwa na waliosababisha wapate mateso wanayopitia Sasa.

Niwatakie sherehe njea, bia ziendelee kuwa tamu kwenu lakini pia muda wa majonzi utakapowadia tuwe tayari kuupokea. Hongera wote tunaofurahia ushindi mkuu.
Tulizana wembe una makali sehemu mbili, hata wewe kuna sehemu utaumizwa kufidia uwazayo moyoni mwako ya kishetani
Si.lazima yawe ya serikari hata yako katika maisha yako tu.
Ukihisi huna makosa hapa duniani basu ujue wewe sio binadamu
 
Mbowe aliajiri makomandoo waliofukuzwa na JWTZ kwa masuala ya nidhamu ili walipue vituo vya mafuta

Anastahili kunyongwa
Walivilupua hivyo vituo vya mafuta ?!. WaTz tuna hamu na ugaidi siyo ?!

Labda mahakama ya kuelekezwa ndiyo ihukumu kesi ya kufikirika hiyo. Siyo majaji waliosoma labda macombi
 
Kwani katika uamzi wa pingamizi juzi Jaji Siyani aliamua nin? Mbowwe ni gaidi
 
Tulianza awamu ya tano tukapiga makofi wapinzani walipofilisiwa na kufunguliwa kesi tukiamini tunakijenga chama. Tulipomalizana nao tuliamia kwa wana CCM nakuwachapa kuanzia kwenye fikra Hadi kwenye akaunti zao. Leo Wana CCM wote waliokuwa na nguvu ya kiuchumi wamefilisika, au wamekufa kwa presha na baadhi wamepoteza madaraka.

Kwanini yamewapata hayo? Ni kwa sababu waliamua kuishi maisha ya Mwenye nchi badala ya kuishi maisha yao. Wapo watu kwa uzembe kabisa bila kujali elimu zao waliumizwa kisa tu wanamwelekeo na mawazo tofauti. Lakini pia wapo watu walitumia nguvu za kibinadamu na dola kutesa wengine wakiamini zamu yao itadumu Sana. Pole kwao maana Mungu alipangalo si la wanadamu.

Tukamaliza harakati za awamu ya tano, walioamini wapo salama wakageuziwa kibao nakuondolewa kwenye nafasi zao Kisha kukalishwa kimya. Kwa frastration wakanzisha Hadi madarasa ya uongozi na wengine kujifanya wataalamu wa afya kupinga chanjo ya COvID19 lakini leo wote wamenyamazishwa na wanatakiw kuongea lugha moja na waliyedhani Hana nguvu.

Lakini ni Jambo kubwa kwamba unapopanga kuwanyoosha na Mungu naye anapanga ratiba yake, unapotumika kuwanyoosha na Mungu naye anapanga ratiba yake. Akina Rwegamalila waliishi utumwani kwa uvumilivu wakiaminishwa kwamba hakuna namna wanaweza kurudi uraiani lakini Leo wale wote waliokuwa wanawakandamiza awapo kwenye nafasi zao na wengine hata Duniani awapo.

Wapo watu wachache Sana nimeona wanashangilia maamuzi ya kesi ya Mbowe, lakini madhara ya maamuzi haya Ni makubwa Sana kwa wanyonge wa nchi hii. Ninaposema wanyonge simaanishi kwamba watu wasio na fedha Bali namaanisha wale wote ambao maamuzi haya yanawaruhusu kuteswa na dola na bila kuhojiwa. Mfano mkubwa ni utata wa kifo Cha dreva wa kampuni ya Dangote ambapo maelezo ya Polisi yaliyotolewa kila mtu ameyatilia mashaka lakini kile walichotamka Polisi ndicho kinachoishi.

Siyo hayo, tumeshuhudia machinga wakijaribu kufanya fujo karikoo lakini uongozi wao leo wamejitokeza na kusema wale siyo machinga bali Ni wahuni na imepita hivyo. Usidhani Kiongozi wa machinga anappsema Yale aliyoyasema hajui ukweli wake Bali ndivyo amabvyo tunaishi. Kwamba Mwenye kusema hiki ni sawa na si sawa ni serikali.

Niseme wazi kwamba tunaposhangilia maamuzi ya Jaji ambayo hayana hata kifungu Cha sheria kinachoonyesha msingi wa maamuzi yake Basi tutambue kwamba hii siyo huku ya Mbowe. Ni hukumu yakuigwa na mahakama zetu nyingi nchini. Tukumbuke ipo siku Kama ilivyozoeleka kwa miaka mitano viongozi na watu wenye ushawishi ndani ya CCM ambao Sasa hivi wanaona dola na mahakama Wana ndoa nzuri ndoa hiyo itawaathiri wao na famililia zao.

Nimalizie, Makonda aliteuliwa na JK kabla yakuteuliwa kuwa RC na JPM. Lakini ni Makonda huyo huyo wakati anataka kuonyesha ana nguvu alisau mambo yote Jk na familia yake waliyomfanyia na kumtangaza Riz one kwenye skendo za madawa ya kulevya bila hata kutoa ushahidi wowote. Lakini pia wazee wa CCM wasiwe wepesi wa kusahau namna ambavyo wao na familia zao walinyanyasika, mateso waliyopata hayakuzongatia tuhuma zilizothibitika Bali yalijikita kukomoa.

Maamuzi ya Jaji Siyani ambayo yanafuatia uendeshaji wa kesi huku muda wa Azana kesi ikiwa inasimamishwa kumheshimu Mungu itufumbue macho kwamba hawa watu tunaowashangilia ndio hao hao wanaotafuta kututawala wanapokuwa mafichoni au sirini. Tufurahie maana tunamwona Mbowe akiwa anapita mateso lakini naamini vijana waliopo naye kwenye kesi wana wazazi kama ambavyo qatoa maamuzi Wana wazazi.

Tukumbuke Kama baba Riz alivyoumia mwanaye kutajwa kwenye madawa ndivyo wazazi, mke na watoto wa watuhumiwa wanavyoumia wanapogundua muda wakusubiri vijana wao wawahudumie watu wachache ambao Sasa hivi usiku huu wapo wanastarehe na familia zao, wanaitwa Dad na Mom, wanaulizia mshahara utatoka lini wameamua bila sababu yoyote kuakikisha kwamba vijana wale wanateseka na may be wanakufa ili wao malengo yao yatimie.

Mungu aishiye anaweza akanyamaza kwa machozi ya familia hizi kwa muda ila atonyamaza milele. Tunaposherekea ushindi uluotolewa na Jaji leo Ni vyema pia tukaandaa nafsi zetu kupokea maamuzi ya mwenyenzi Mungu dhidi ya watuhumiwa na waliosababisha wapate mateso wanayopitia Sasa.

Niwatakie sherehe njea, bia ziendelee kuwa tamu kwenu lakini pia muda wa majonzi utakapowadia tuwe tayari kuupokea. Hongera wote tunaofurahia ushindi mkuu.
Kweli kabisa. Anayelia leo hucheka kesho, na kinyume chake.
 
Mbowe anakula miaka kimasihara hivi ukishangilia ya sabaya shangilia na ya mbowe

USSR
Mbowe atajiunga na mashujaa wengine Kama Nelson Mandela,Jomo Kenyatta,Haikande na wengine wengi. Ukombozi una gharama. MBOWE SIYO GAIDI.
 
Kwa Sabaya haki imetendeka na mahakama ni huru. Kwa Mbowe haki haijatendeka na mahakama siyo huru. What a double standard!

Wakiguswa wengine mnanyamaza, akiguswa gaidi mnataka sote tumpiganie eti wakimalizana nao watakuja na kwetu!
Kesi ya mbowe na kesi ya Sabaya havifanani, kesi ya Sabaya ipo wazi kila mmoja ni shahid wa maovu yake, lakini kesi ya mbowe ni kesi ya kubambikiwa mashahidi wa kutengeneza na jaji kapewa Rushwa ya cheo cha jaji kiongozi ili akatae ushahidi wa ukiukaji PGO na mateso kupigwa walikofanyiwa walinzi wa mbowe, endelea kuwahonga vyeo majaji wajitoe fahamu kupindisha Sheria lakini watambue mungu yupo na Albadiri haitawaacha salama
 
Ulichoandika hata hakieleweki. Wewe unajua sheria kuliko huyo hakimu aliyeshughulika na hii kesi ? CHADEMA mnaashngaza sana mwanzoni mwa utawala wa awmu ya tano mlitaka nchi isitawalike, ila mkdhibitiwa. Hivyo, acheni sheria ichukue mkondo wake na mjifunze kuwa watulivu wakati kesi ikiwa mahakamani.
Sheria ipi ichukue mkondo wake? Kwa kosa lipi ugaidi hewa wa kuwabambikia watu? PGO inaruhusu kuwatesa kuwapiga watu kuwafunga pingu saa 24 kila siku? Hakimu yupi anajua Sheria? Kuhongwa cheo cha ujaji kiongozi kisha kupindisha Sheria ndiyo kujua Sheria?
 
Subirini mahakama itende haki kama ilivyotenda kwa Sabaya.
Sabaya ni jambazi ni mbakaji kweli na kila Mtanzania ni shahid wa maovu yake ni tofauti na kesi ya mbowe ambayo ni kesi ya kubambikiwa huku PGO ikiwa imekiukwa kwa kiwango chakutisha
 
Kwa
Nyie mnayemlaumu Samia kwani hii kesi ilifunguliwa awamu yake? Yeye ndiye Polisi waliyefanya upelelezi na kuleta ushahidi mahakamani? Yeye ndiye mwendesha mashtaka aliyepeleka kesi Mahakamani? Yeye ni jaji anayeamuru hizi kesi? Siku zote si mmekuwa mnalilia serikali isiingilie mahakama? Sasa mbona mnafanya kinyume na kulazimisha Serikali iingilie hii kesi? Mbona hatujaona nguvu kama hii ikitumika kwenye kesi nyingine?

Subirini kesi ya msingi, ushahidi wote utawekwa hadharani! Kama Mwamba hana hatia ataachiwa, huu uoga wenu unatoka wapi? Mbona inaonekana kama inatumika nguvu kubwa sana kuhakikisha kesi kuu haisikilizwi? Nini kinafichwa? Au kuna ushahidi huko unamvua mtu nguo na njia pekee ya kuukwepa ni kuhakikisha kesi kuu haisikilizwi? Subira inahitajika, Muda utatoa majibu, hizi panicks sijui mnazitoa wapi
Kwani anashindwa kuifuta? Mbona ya Ruge ameifut??? Mbowe amekamatwa mwaka Huu mwez wa nane ilikuwa awamu ya nani
 
Hafuti yeye kesi, kesi zinafutwa na DPP na timu yake baada ya kuzichambua! And kumbuka kuna makesi mengi tu ya hovyohovyo wanayapitia kwa sasa, na zote zina umuhimu wake na wahusika wake wana haki pia ya kuwa free, itapofika zamu ya kesi ya Mbowe itachambuliwa pia kama waifute or not! Ulitaka warukie kesi ya Mbowe ya juzi tu hapa wakati kuna watu wamesota rumande miaka 5 sasa na ushahidi hakuna? And kesi ilishafunguliwa August 2020, lilikuwa ni suala la muda tu akamatwe! So utawala wa Samia usikamate mtu yeyote wa upinzani hata kama ameshtakiwa mahakamani? Kama ni hivyo basi majambazi yote yakimbilie upinzani, maana ukikamatwa ukiwa huko utatetewa na kila mtu
 
Nyie mnayemlaumu Samia kwani hii kesi ilifunguliwa awamu yake? Yeye ndiye Polisi waliyefanya upelelezi na kuleta ushahidi mahakamani? Yeye ndiye mwendesha mashtaka aliyepeleka kesi Mahakamani? Yeye ni jaji anayeamuru hizi kesi? Siku zote si mmekuwa mnalilia serikali isiingilie mahakama? Sasa mbona mnafanya kinyume na kulazimisha Serikali iingilie hii kesi? Mbona hatujaona nguvu kama hii ikitumika kwenye kesi nyingine?

Subirini kesi ya msingi, ushahidi wote utawekwa hadharani! Kama Mwamba hana hatia ataachiwa, huu uoga wenu unatoka wapi? Mbona inaonekana kama inatumika nguvu kubwa sana kuhakikisha kesi kuu haisikilizwi? Nini kinafichwa? Au kuna ushahidi huko unamvua mtu nguo na njia pekee ya kuukwepa ni kuhakikisha kesi kuu haisikilizwi? Subira inahitajika, Muda utatoa majibu, hizi panicks sijui mnazitoa wapi
Haki inapoporwa, inaonekana wazi sawasawa na doa jeusi kwenye karatasi nyeupe.Wooote wanaojua vifungu vya sheria wameliona hili.Wewe usiyejua sheria huwezi kuona.Ila kama ulikuwa ukienda kusikiliza kesi ilivyokuwa inaendeshwa ungejua.Hivi kweli alisema Wenzake waliotuhumiwa na Mbowe walishahukumiwa yeye Mbowe eti akatoroka.Hii unaionaje,imekaaje,
walipoletwa mahakamani kutoa ushahidi walishahukumiwa kifungo sio.Kwa hiyo walipokamatwa huko Moshi walitoroka magereza ndio wakaja kutafutwa wakakamatwa.Halafu kesi waliyokamatwa nayo ikaanza kusikilizwa kwa upya.

Ogopeni basi hata hiyo miungu yenu mnayoiabudu. Nchi yetu naihurumia sana,kwa sababu inateseka kwa kutendewa vitu vya ajabu,ndiyo maana imeshindwa kutoa mazao ili watu wake waneemeke kwa sababu ya udhalimu na uongo wa wanaoiongoza.Mtu mzima anasema uongo mwanzo mwisho hadharani bila aibu.

Kama sio kweli kumbukeni yule mwingine alisema uongo mpaka leo yupo wala hajatubu kwa aliyoyasema Eti kiongozi wenu ana afya njema anaendelea na kazi zake.Kumbe mtu anapumulia gesi. Tena mwingine alisema nimekwenda kumwona jana,ni mzima wa afya. Sawa endeleeni kudanganya,lazima lazima ipo siku mtaumbuka kama mlivyoumbuka.

Mimi naamini,Huyu aliyetuweka hai mpaka leo,hata hili atalimaliza salama.Haki huinua taifa.Bali dhambi ni aibu kwa taifa.
 
Back
Top Bottom