Nimefurahia maamuzi kesi ya Mbowe, Mungu mkubwa atatenda

Mleta mada poleni MaCHADEMA hiyo ni wembe kuwili.
Ila pigeni domo tu kuondoa machungu.
 
Jamani, ugaidi siyo wa kukumbatia hata kidogo. Tuache tu mahakama ifanye kazi yake.
 
hii nchi kuna watu wanafiki nyinyiahhh.

sabaya kala mvua,watu wamechinja mbuzi na kuisifu mahakama,mbowe hata hajafungwa siku moja.tayari kelele.
 
Tulianza awamu ya tano tukapiga makofi wapinzani walipofilisiwa na kufunguliwa kesi tukiamini tunakijenga chama. Tulipomalizana nao tuliamia kwa wana CCM nakuwachapa kuanzia kwenye fikra Hadi kwenye akaunti zao. Leo Wana CCM wote waliokuwa na nguvu ya kiuchumi wamefilisika, au wamekufa kwa presha na baadhi wamepoteza madaraka. Kwanini yamewapata hayo? Ni kwa sababu waliamua kuishi maisha ya Mwenye nchi badala ya kuishi maisha yao. Wapo watu kwa uzembe kabisa bila kujali elimu zao waliumizwa kisa tu wanamwelekeo na mawazo tofauti. Lakini pia wapo watu walitumia nguvu za kibinadamu na dola kutesa wengine wakiamini zamu yao itadumu Sana. Pole kwao maana Mungu alipangalo si la wanadamu.

Tukamaliza harakati za awamu ya tano, walioamini wapo salama wakageuziwa kibao nakuondolewa kwenye nafasi zao Kisha kukalishwa kimya. Kwa frastration wakanzisha Hadi madarasa ya uongozi na wengine kujifanya wataalamu wa afya kupinga chanjo ya COvID19 lakini leo wote wamenyamazishwa na wanatakiw kuongea lugha moja na waliyedhani Hana nguvu.

Lakini ni Jambo kubwa kwamba unapopanga kuwanyoosha na Mungu naye anapanga ratiba yake, unapotumika kuwanyoosha na Mungu naye anapanga ratiba yake. Akina Rwegamalila waliishi utumwani kwa uvumilivu wakiaminishwa kwamba hakuna namna wanaweza kurudi uraiani lakini Leo wale wote waliokuwa wanawakandamiza awapo kwenye nafasi zao na wengine hata Duniani awapo.

Wapo watu wachache Sana nimeona wanashangilia maamuzi ya kesi ya Mbowe, lakini madhara ya maamuzi haya Ni makubwa Sana kwa wanyonge wa nchi hii. Ninaposema wanyonge simaanishi kwamba watu wasio na fedha Bali namaanisha wale wote ambao maamuzi haya yanawaruhusu kuteswa na dola na bila kuhojiwa. Mfano mkubwa ni utata wa kifo Cha dreva wa kampuni ya Dangote ambapo maelezo ya Polisi yaliyotolewa kila mtu ameyatilia mashaka lakini kile walichotamka Polisi ndicho kinachoishi.

Siyo hayo, tumeshuhudia machinga wakijaribu kufanya fujo karikoo lakini uongozi wao leo wamejitokeza na kusema wale siyo machinga bali Ni wahuni na imepita hivyo. Usidhani Kiongozi wa machinga anappsema Yale aliyoyasema hajui ukweli wake Bali ndivyo amabvyo tunaishi. Kwamba Mwenye kusema hiki ni sawa na si sawa ni serikali.

Niseme wazi kwamba tunaposhangilia maamuzi ya Jaji ambayo hayana hata kifungu Cha sheria kinachoonyesha msingi wa maamuzi yake Basi tutambue kwamba hii siyo huku ya Mbowe. Ni hukumu yakuigwa na mahakama zetu nyingi nchini. Tukumbuke ipo siku Kama ilivyozoeleka kwa miaka mitano viongozi na watu wenye ushawishi ndani ya CCM ambao Sasa hivi wanaona dola na mahakama Wana ndoa nzuri ndoa hiyo itawaathiri wao na famililia zao.

Nimalizie, Makonda aliteuliwa na JK kabla yakuteuliwa kuwa RC na JPM. Lakini ni Makonda huyo huyo wakati anataka kuonyesha ana nguvu alisau mambo yote Jk na familia yake waliyomfanyia na kumtangaza Riz one kwenye skendo za madawa ya kulevya bila hata kutoa ushahidi wowote. Lakini pia wazee wa CCM wasiwe wepesi wa kusahau namna ambavyo wao na familia zao walinyanyasika, mateso waliyopata hayakuzongatia tuhuma zilizothibitika Bali yalijikita kukomoa. Maamuzi ya Jaji siani ambayo yanafuatia uendeshaji wa kesi huku muda wa Azana kesi ikiwa inasimamishwa kumheshimu Mungu itufumbue macho kwamba hawa watu tunaowashangilia ndio hao hao wanaotafuta kututawala wanapokuwa mafichoni au sirini. Tufurahie maana tunamwona Mbowe akiwa anapita mateso lakini naamini vijana waliopo naye kwenye kesi wana wazazi kama ambavyo qatoa maamuzi Wana wazazi. Tukumbuke Kama baba Riz alivyoumia mwanaye kutajwa kwenye madawa ndivyo wazazi, mke na watoto wa watuhumiwa wanavyoumia wanapogundua muda wakusubiri vijana wao wawahudumie watu wachache ambao Sasa hivi usiku huu wapo wanastarehe na familia zao, wanaitwa Dad na Mom, wanaulizia mshahara utatoka lini wameamua bila sababu yoyote kuakikisha kwamba vijana wale wanateseka na may be wanakufa ili wao malengo yao yatimie.

Mungu aishiye anaweza akanyamaza kwa machozi ya familia hizi kwa muda ila atonyamaza milele. Tunaposherekea ushindi uluotolewa na Jaji leo Ni vyema pia tukaandaa nafsi zetu kupokea maamuzi ya mwenyenzi Mungu dhidi ya watuhumiwa na waliosababisha wapate mateso wanayopitia Sasa.

Niwatakie sherehe njea, bia ziendelee kuwa tamu kwenu lakini pia muda wa majonzi utakapowadia tuwe tayari kuupokea. Hongera wote tunaofurahia ushindi mkuu.
Umenena vyema. Walio na Roho wa Mungu watakuelewa, na nafsini mwao watanena na Mungu.

Nao waishio na shetani mioyoni mwao watafurahia, sawa na watawala wetu hawa wenye ndoa ya kudumu na yule mwovu, shetani. Lakini wasichojua ni kuwa Shetani wanayeishi naye hana ndoa na mwanadamu. Amewapa nafasi ya muda mfupi kufurahia ili waangamie milele kwa ujinga wao.
 
Kwa Sabaya haki imetendeka na mahakama ni huru. Kwa Mbowe haki haijatendeka na mahakama siyo huru. What a double standard!

Wakiguswa wengine mnanyamaza, akiguswa gaidi mnataka sote tumpiganie eti wakimalizana nao watakuja na kwetu!

Pathetic fools.
Sabaya alikiri, je, Mbowe nae amekiri makosa?
 
Inaumiza sana kuona mtu anayejifanya mchamungu na kuvaa ushungi masaa 24 anafanya ushetani kama huu.

Bora Mbowe ana watoto wakubwa na wana maisha yao. Sasa hao vijana watatu wana wake zao na watoto wanateseka kisa tu walitaka kumlinda Mbowe.

Mchengelwa mshauri vizuri mkweo. Malipo ni hapa hapa duniani.
Kwa ushetani huu ambao huyu Mama anaufanya, hakika atawafanya Watanzania, hasa wa bara wauone hata Muungano ni sehemu ya ushetani.

Mtu hawezi kutoka kwenye visiwa nukta kuja kuwaumiza wananchi wa Taifa mlima. Hapa naikumbuka kauli ya marehemu Mtikila, "kama huu unyama unapendwa huko kwao, wamwambie huyo TX akaufanyie huko kwao Mchambawima"
 
Kuna jambo baya sana Wakubwa wanalijenga katika mioyo ya Watanzania. Na si kwamba hawajui, wanajua. Katika vikao vyao huwa wanaambizana. Lkn mwisho wanakubaliana kwamba Watanzania hawana ujasiri huo. Wanaamini Nchi zingine wana mioyo tofauti na Watanzania.

Lkn, siku Ujenzi huu ukikamilika, watambue kwamba wakubwa huonekana kirahisi kuliko wanyonge..hivyo madhara yakakuwa makubwa zaidi kwao.
 
Kwa ushetani huu ambao huyu Mama anaufanya, hakika atawafanya Watanzania, hasa wa bara wauone hata Muungano ni sehemu ya ushetani.

Mtu hawezi kutoka kwenye visiwa nukta kuja kuwaumiza wananchi wa Taifa mlima. Hapa naikumbuka kauli ya marehemu Mtikila, "kama huu unyama unapendwa huko kwao, wamwambie huyo TX akaufanyie huko kwaa Mchambawima"
Uvunjwe huu muungano fake unaotuletea madikteta kama hili
 
Huezi amini Jaji ametoka kuadhimisha Siku ya kuzaliwa mtume (SAW) akaja na hili...
Hatujali watu waliteswa,walinyimwa chakula,walitiwa madawa,sheria haikufatwa kuwakamata,walitishwa kuuawa nk. Wanachotizama ni cheo nakuzidi kumfraisha muungu wao mtoa vyeo.
Mpaka vijana watakaposema sasa inatosha tunataka katiba safi na ifuatwe basi amiini nisemayo watu weeengi watakuwa wamedhulumiwa na taasisi vibogoyo,vipofu,viguru,viziwi tulizo nazo!!!

Eeh Mwenyezi Mungu wadondoshe woote walinyimao taifa lako haki,
aamini.
Huu utawala wa kishetani lazima tuukatae mkuu
 
Nyie mnayemlaumu Samia kwani hii kesi ilifunguliwa awamu yake? Yeye ndiye Polisi waliyefanya upelelezi na kuleta ushahidi mahakamani? Yeye ndiye mwendesha mashtaka aliyepeleka kesi Mahakamani? Yeye ni jaji anayeamuru hizi kesi? Siku zote si mmekuwa mnalilia serikali isiingilie mahakama? Sasa mbona mnafanya kinyume na kulazimisha Serikali iingilie hii kesi? Mbona hatujaona nguvu kama hii ikitumika kwenye kesi nyingine? Subirini kesi ya msingi, ushahidi wote utawekwa hadharani! Kama Mwamba hana hatia ataachiwa, huu uoga wenu unatoka wapi? Mbona inaonekana kama inatumika nguvu kubwa sana kuhakikisha kesi kuu haisikilizwi? Nini kinafichwa? Au kuna ushahidi huko unamvua mtu nguo na njia pekee ya kuukwepa ni kuhakikisha kesi kuu haisikilizwi? Subira inahitajika, Muda utatoa majibu, hizi panicks sijui mnazitoa wapi
Kwa nini atoe rushwa ya cheo kwa Jaji anayeisikiliza hii kesi, wakati yeye ndiye anayemshtaki Mbowe?

Kwa nini mtu ambaye ni TISS apewe cheo kikubwa ndani ya mahakama? Hii siyo kuvuruga mahakama?

Huyu ni shetani katika umbile jingine. Na anaweza kuwa hatari kuzidi hata marehemu. Marehemu alikuwa muwazi. Kama anakuchukia au anataka kukuonea, atasema wazi. Huyu ni mnafiki. Sauti ya upole, ushungi haubanduki, lakini kilichopo ndani ni uchafu mtupu.

Amekuwa kama kaburi ambalo nje limepambwa kwa maua lakini kilichopo ndani kila mmoja anajua.

Anayemshtaki Mbowe ni Serikali, na kiongozi mkuu wa Serikali ni yeye, halafu anampandisha cheo jaji anayesikiliza kesi ambayo yeye ninmlalamikaji. Hii siyo rushwa ya wazi kabisa?
 
Back
Top Bottom