Nimefunguliwa kwenye kifungo cha hofu na mashaka

Nimegundua kuwa ukipima unakuwa na furaha zaidi kwa matokeo yoyote yale. Nenda tu mkuu usihofu, mimi mara tatu narudia getini na ya nne ndo sikurudi kabisa kuchukua matokeo. Tena sasa hivi simple sana damu wanatoa kwenye kidole!

mimi huwa naamini wakinitoa kwenye mshipa.....sijui kwa nini
 
Sijajua kwanini sasa hivi wanatoa kupitia kidoleni lakini yale ambayo nilikimbia hawakutoa kidoleni.
 
Mkuu! Hongera kwa kitendo cha ujasiri.
Nakumbuka nilipokua std 7 niliwahi kula Chipsi ambazo zilikuwa na damu ya mtu ambaye alikuwa ameathirika...
Nilipoanza kidato cha kwanza kama miezi minne tu yule mama alifariki na ilijulikana moja kwa moja ni ngoma tangu hapo nilikuwa naishi maisha ya wasiwasi mpaka nilipo hitimu form 4 nikajipanga kwenda kupima mara 8 nilikuwa naishia getini,
Siku moja nikapiga moyo konde nikatia timu mpaka angaza Mnazi mmoja nikafika nikaeleza kila kitu nikapewa ushauri baadae nikapimwa majibu yakatoka safi kabisa.
Japo nilikuwa natolea watu damu lakini sikuwahi kuuliza ishu ya majibu ya HIV
Yaani niliishi kwa uoga kuanzia mwaka 2001 April mpaka 2004 November.
KUNA UMUHIMU WA KUPIMA KWA KILA MMOJA WETU ILI AJUE AFYA YAKE NA HII INASADIA KUJUA UPO KATIKA HALI GANI.
 
Sijajua kwanini sasa hivi wanatoa kupitia kidoleni lakini yale ambayo nilikimbia hawakutoa kidoleni.

hongera sana....hilo huwa ni zoezi gumu kidogo.....nina imani utakuwa muangalifu sana kwa sasa
 
Hongera sana mwana, maana inataka ujasiri, ngoja niwachekeshe, kuna siku nilienda kupima pale red cross, nilipoona muhudumu aliyenipima anakuja kuniita nikaanza kuondoka akaanza kunifata nyuma ananiita jina langu mie siangalii nyuma mkuku nilipofika kwenye ngazi ya mwisho kabisa akaniita jina ,akaniambia kwa sauti usikimbia mambo mazuri nikafunga bonge la brake, imagine hapo nageuka huku nasema beeeeee!!!
allicheka sana na mimi pia huku nilikuwa nimelowa jasho, kwa kweli unajisikia vizuri sana unapopima afya na kujikuta uko fresh
 
Duh!
Mimi mara 8 nimeshaishia getini!
 
Ha ha haaa haaaa we Gaga unachekesha sana, Mwenzio leo niliuliza chooni nikaonyeshwa choo kiko mulemule ndani halafu hakuna mlango mwingine wa kutokea lazima upite pale alipokaa daktari. Nikaona hakuna sababu ya kutoroka katika hali kama hiyo. Halafu nilichokuwa naogopa zaidi niliwahi kuota napima pale mnazi mmoja nikakutwa nimeathirika. Si mfuasi sana wa imani za ndoto lakini hiyo ilinifanya nisiende kupima mnazi mmoja ambako ni free badala yake nikaendfa kupima sehemu ambayo nilichajiwa 10,000
 
Hapa siwezi kukuongopea yale maswali yanatisha ndugu yangu na usipokuwa jasiri unaweza kujikuta unabadilisha uamuzi wakati uleule wa maswali
Safi sana mkuu kwa kuwa jasiri, mimi nimepima nimekutwa navyo but ajabu ni kwamba ninaishi kwa furaha kuliko hapo kabla.
 
Ahsante vijisenti. Naona umekuja na AVATAR baku kubwa.
 
Hapa siwezi kukuongopea yale maswali yanatisha ndugu yangu na usipokuwa jasiri unaweza kujikuta unabadilisha uamuzi wakati uleule wa maswali
Hongera sana mdau,ni hatua kubwa na muhimu sana katika karne hii,nenda tena after 3months,tunza status yako,usimwamini hata atakayekwambia yeye ni neg bila kwenda nae mguu kwa mguu tena kabla hajawa mke/MUME usikubali bila kinga kijana.Napenda waJasiri kama wewe.HONGERA SANA!:smiling::smiling:
 
Sasa nyie mnaosema hamtapima inamaana hamtakujaoa? Mi navyojua mfano kwa wakristo ukitaka kuoa inakubidi mpime kwanza.

ndugu yangu hayo unayosema ni serious?au kautani?lakini siamini kama nitaweza hata kufika pale getini
 
Sasa nyie mnaosema hamtapima inamaana hamtakujaoa? Mi navyojua mfano kwa wakristo ukitaka kuoa inakubidi mpime kwanza.
Halafu kwa jinsi nilivyokiona kile kipimo kilichotumika kuna uwezekano mkubwa kila mmoja akawa nacho. Ingekuwa ni uwezo wangu vile vifaa ilibidi vipatikane kwenye GESTI zoote, pia kila anayehusika na ufungishaji ndoa kwa namna moja au nyingine pia awe nacho. Ingependeza sana.
 
Gazeti, watu wako tayari kupima uzito lakini siyo hayo unayoyataka. Kama utataka gesti ziwe hivyo si ajabu vichochoro na magofu vikawa kimbilio lao.
 
Hongera sana Gazeti sasa ubadili Tabia. Lakini hujatuambia kama hukukwenda Samunge kupata kikombe kikakupa ujasiri.
 
Haya bwana mimi nilikuwa kama wewe pia,nlikuwa muoga sana kupima lakini 2009 nikapima,ila sasa naogopa tena kupima sijui mpaka nini ndio nipime..anwy hongera sana.
 
Ingekuwa kinyume ungemshauri yeyote kufanya hivyo?Au ungepotea hata JF tusingekusoma tena!
 
Hongera sana kwa uamuzi uliofanya maana sasa upo huru ..ila hebu niambie ...yaani tangu 2002 hadi 2011 umekuwa na mashaka lakini mwoga kupima, Ni vipi ulipokuwa na homa? itakuwa ulikuwa unaugua mara mbili yani homa yenyewe na h:confused2:fu juu!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom