Nimefukuzwa na mwenyeji wangu naomba msaada wa hifadhi Dodoma

DavidM15

Member
Oct 20, 2022
5
65
Habari za wakati huu Wana JF.

Kwa majina naitwa David Mathias. Nilikuja Dodoma kutafuta maisha kutokea jijini Dar na nikafikia kwa rafiki yangu niliesoma nae chuo kimoja ambaye anaishi Nkuhungu. Rafiki yangu ameleta mwanamke ghafla na kuniambia kuwa anataka aishi nae kwahiyo mimi niondoke.

Hapa nipo barabarani tu begi langu sina pa kwenda na mimi huku mgeni. Naomba kwa mwenyeji yeyote wa Dodoma atakayeguswa kunisaidia hifadhi kwa siku kadhaa nikitafuta nauli ya kurudi nyumbani. Naomba sana na natanguliza shukurani.
 
Mkuu

Endapo hautopata msaada wowote hadi muda huu basi fika kituo chochote cha polisi utapta msaada bana.

Ukiwaeleza issue yako wanaweza hata kushauriana na mwenyeji wako au namna ya kukupatia hifadhi kwa muda unaosubiri nauli.

Na kama unataka kurudi Dar kwa namna yeyote, polisi wanaweza kukuombea lift kwenye malori ya mizigo ukafika Dar hata kesho.
 
Umenikumbusha kipindi fulani naenda Mkoa X. Nimefika usiku saa 7 alietakiwa kunipokea hapatikani kwa simu, Sema kuna mama nilimsaidia kulea mtoto wakati tupo ndani ya gari wakati nimeshuka sijui nifanyeje niende wapi yule mama akaniona akaniomba nimsinfikize kwake coz ana mizigo na watoto 2 so hawaamini madereva bajaji wanaweza kumuibia.

Aisee sikuamini,Mungu anatoa msaada pale plan zako zote zimefeli hujui ushike lipi. Btw nilienda kwake nikashinda mpaka jioni ndio niliondoka. Sijawahi kumuona wala kuwasiliana nae tena
 
Pole jamaa, nakumbuka kuna kipindi natoka mkoani naenda Dar nimeshaa chonga na ndugu yangu vzr kabisa kwamba nitatua kwake.

Nakaribia kufika napiga simu haipokelewi, nikajua normal tu, hee nashuka naona simu haipokelewi.
Asnte Yesu nikikua vzr mfukoni ikabidi niingie lodge tu, nikapata akili kumbe binadamu sie dah.!

Hakunitafutaga mpaka leo japo kwenye masuala muhimu huwa tunakutana mfano misiba, harus lkn hakuwahi wala sikuwah muuliza ilikuaje.
 
Naona jamaa wako kakufukuza kijanja usikute hata mwanamke hatokaa nae katafuta njia ya kukutoa hapo geto
Niliwahi karibisha jamaa yangu akae siku tatu tukiwa chuo akakaa miezi mitatu na point. Sikuwa na mambo mengi na tuliendana vitu vingi basi alikaa mpaka alipoamua kuondoka. Inaleta changamoto ukikaa na mtu mko tofauti sana na bado unapenda uhuru wako
 
Back
Top Bottom