Nimefiwa na Mama yangu usiku wa kuamkia 19.11.2011 na kuzika jana.

Ooh mpenzi pole sana. Mungu akupe nguvu na faraja katika hiki kipindi kigumu. Tupo pamoja.
 
Pole sana kaka Uporoto, ni safari yetu sote... Mungu awatie nguvu na niwatakia maandalizi mema ya kumpumzisha mama yetu mpendwa.
 
pole sana mkuu, nayajua maumivu unayopata kwani duniani hakuna kama mama ila mshukuru MUNGU kwa kila jambo. RIP mama.
 
Pole sana kwa msiba mkuu. mungu akupe faraja ya pekee katika kipindi hiki cha majonzi
 
Pole sana sana Mkuu. Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu. Mungu pia aipumzishe roho ya mama mahali pema peponi apumzike kwa amani.
 
Pole sana ndugu yangu, kazi ya mungu haina makosa. Nawaombea mungu awape moyo wa uvumilivu wote waliofikwa na msiba huu mzito.


RIP mama yetu!
 
Pole sana rafiki. Bwana awatie nguvu na kuwapa faraja ya pekee katika kipindi hiki kigumu. POLENI SANA.
 
Tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu. Mungu akupe nguvu na faraja. Bwana ametoa, bwana ametwaa, jina la bwana libarikiwe. Ameni.
 
Nilikwambia zamani kuwa tutakuwa tunafahamiana baada ya kusoma watu wengi unaowaongelea.

Tupo sote na kesho InshaAllah ntakuwepo mchana. Mwenyeezi amrehem, aturehem na sisi ambao tupo njiani kuelekea huko.

Mwenyeezi Mungu awape subra wote.
 
Pole sana Uporoto1
Mungu akupe amani moyoni wakati wa kipindi hiki kigumu cha majonzi
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom