Nimefikiri hivi katika kuogeza kipato

mapipando

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
2,921
3,549
Heshima kwenu wakuu.

Nilianzisha uzi hapa "huu ni mwaka wangu wa mwisho kuajiriwa" na kweli nilipanga kuacha kazi baada ya kuona mshahara hautoshelezi mahitaji yangu na familia kwa ujumla.

Lakini kutokana na baadhi ya michango yenu hasa mlioniambia nisiache kazi bali nitafute namna yeyote niweze kuongeza kipato nimeheshimu ushauri wenu na ninawashukuru sana sana.

Nimegundua kuna biashara nyingi ambazo ukiziangalia kwa kawaida unazidharau lakini ni biashara ambazo sio pasua kichwa na zina faida sana ila sisi tunazichukulia poa ama kama uchafu flani na kujirundika kwenye aina moja za biashara ambazo ziko na ushindani mkubwa sokoni mfano ufugaji na kilimo.

Mfano biashara ya chuma chakavu, hii inalipa sana kwani kilo moja inanunuliwa kwa 500 na kuuzwa 800, na wewe unauza kuanzia tani moja na kuendelea. Ikitokea kwa mwezi umekusanya tani 3 na kuziuza zote maana yake uko na faida ya 900k

Pia biashara ya makopo ya plastiki pia ni nzuri maana nayo haina stress nyingi lakini inalipa. Kilo moja inanunuliwa 150-200 na kuuzwa kwa 500. Kwa maana hiyo hapo kuna faida sawa na mtaji...ukiwa na mzigo laki tano faida laki tano pia.

Nimeulizia mzani wa kupimia chuma nimeambiwa unanzia laki 7 na mzani wa chupa (ile ya kuning'iniza) inaanzia elfu 25.

Wakati huu ambao siwezi kuanzisha biashara ya chuma, nimeona nianze na hii ya chupa. Nitatengeneza mazingira rafiki hapa home kwangu ili niweze kuiendesha hii biashara na hapo baadae nitafute mashine ya kukatakata ili niwe nahifadhi kwenye mifuko.

Kama kuna mwenye uzoefu na hizi biashara karibu kwa mawazo.
Shukrani.
 
That's nice namjua mtu anayejihusisha na hiyo biashara na sasa anaishi maisha ambayo wengi tunawish.
 
Umewaza usafirishaji na mahala pakuhifadhi huo mzigo Mkuu?. Kwanini hilo eneo usifikirie tena jambo lakufanya hapo?

Na vipi utakuwa unaisimamia wewe au utaweka mtu wakusimamia Mkuu.
 
Kwangu kuna eneo ambalo naweza kulitumia...na kuhusu usafirishaji sidhani kama kutakuwa na changamoto kwani kunafikika.
Kuhusu usimamizi ataanza wife kwa kipindi hiki cha mwanzo then mbele ya safari biashara yenyewe itashauri ni nini kifanyike zaidi.
Vilevile nitaulizia mashine za kuchakata ili niweze kuhifadhi mzigo mwingi kwenye eneo dogo na hii pia itasaidia sana kwenye usafirishaji na upimaji.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom