Nimefika umri wa kuoa, lakini sijui nimuoe nani

Hello guys,


Sijui kama kuna kuna wengine humu wamekutana na kitendawili kama hiki, nimemaliza chuo, na kwa position ya kifedha nliopo nayo sahivi kwenye maisha, vijana wengi wa umri wangu wangekuwa wameshaweka mke ndani. ila ugumu unakuja sehemu hizi:


1) Wanawake ninaowapenda hawanipendi, na nisiowapenda wananipenda, nshawahi kuwa kwenye relationships miaka ya nyuma lakini hao wadada nlikuwa sina malengo nao, so nkawatema, hlf kujifosi nioe mwanamke nisiempenda eti kisa ananipenda siwezi, naona nitajitesa kwenye ndoa, pia kuoa mwanamke asienipenda eti kwasababu nampenda, naogopa coz naona huyo mwanamke atateseka na atanitesa pindi tukiingia kwenye ndoa


2) Nimejaribu kutafta basi wale wadada ambao nawatamani kimwili (sio kuwapenda) ili niwaoe, majority of them wapo kimaslahi (wananipiga mizinga au wananipendea pesa) wengine wananichukulia poa kwenye mahusiano though nakuwa nimewawazia mazuri tu pindi tukishaingia kwenye ndoa.

Jamani mliokwisha oa humu ndani mliwezaje kuchagua wenzi wenu wa ndoa? Je mliwapenda toka mwanzo? Hao wenzi wenu MNA hakika wanawapenda? Au mtu unakuwa humpendi ila unamuoa/unaolewa nae tu kwa kuvumilia, coz naona kwenye ndoa nyingi waume na wanawake hawakuwapenda wenzi wako toka mwanzo ila waliolewa/walioa tu coz hamna namna/option nyingine.
Nayapitia unayopitia. Kila mpenzi Wangu was zamani sioni kama anafaa kuolewa.

Ninaowapenda kwa sasa bado wanataka maisha nje ya ndoa na wengine hawana mpango wa kuolewa
 
Nadhani linapokuja suala la kuoa angalia we moyo wako unaelekea wapi kwanza usije kumuoa mtu kwa kumuonea huruma na wala usije kuoa mtu kwa kuogopa kuchelewa kuoa
Keep calm muombe Mungu muda ukifika utampata mtu sahihi
 
Kina jamaa aliwahi kutoa ushauri kama unataka kuoa mke udumu nae basi kaoe kahaba
NDIO KAHABA
Wengi wa hawa watu hua wamekata tamaa na maisha na kwa kweli hua wanatafuta stara kwa hali na mali na ukicheki background yao waweza kutokwa na machozi

Pia hua sio limbukeni wa mapenzi

Kumbuka Sio wote ndio wanafaa kuoa inafaa pia ufanyie uchunguzi
Kizuri huja kwa kitafutwa

Nb. Sio wazo langu nimeyakuta tu humuhumu jf
Kunandugu yangu ameoa kahaba tena wale waliokuwa wanasimama usiku barabarani lakini alioa ivyo ivyo mpaka leo anaaman na ndoa yake na uso wake unaonyesha ni jinsi gani anaamani na furaha,wanamiaka 5 sasa kwenye ndoa
 
Kunandugu yangu ameoa kahaba tena wale waliokuwa wanasimama usiku barabarani lakini alioa ivyo ivyo mpaka leo anaaman na ndoa yake na uso wake unaonyesha ni jinsi gani anaamani na furaha,wanamiaka 5 sasa kwenye ndoa
Hahahahaaa sasa kaige na wewe uje utufungulie uzi unalialia
 
Nadhani linapokuja suala la kuoa angalia we moyo wako unaelekea wapi kwanza usije kumuoa mtu kwa kumuonea huruma na wala usije kuoa mtu kwa kuogopa kuchelewa kuoa
Keep calm muombe Mungu muda ukifika utampata mtu sahihi
Na kuongezea asioe sababu ya msukumo. Au pressure kutoka kwa marafiki, ndugu. Ataumia
 
Angalia mazingira unayotafutia Make.
Kwenye nyumba za starehe, Kanisani ama Msikitini?

Unapotafuta mke kwenye nyumba za ibada risk ya kupata mke asiyesahihi inakuwa ndogo kulinganisha na maeneo mengine.
 
Kuna taraka kwakuwa waliliona hilo kuwa unawezapenda kimwili akikuchosha unafukuza unaoa mnayependana
 
Usipende kujifunza kwa watu walio feli kwenye ndoa hafu ukate tamaa utaumia, changamoto ziko kila mahali
Ni kweli ziko kila mahali, ila kwa niliyo na ninayokutana nao kwa waliooa, eeeeeh!
 
Nani kakuambia kuna kupendana duniani? Eti umpate anayekupenda na wewe unampenda! Cha muhimu kuvumiliana tu
 
Ni kweli ziko kila mahali, ila kwa niliyo na ninayokutana nao kwa waliooa, eeeeeh!
Changamoto hazikwepeki duniani kwenye jambo lolote kikubwa nikuzishinda tu basi, sasa zikidi isiwe sababu yakutokufanya jambo
 
Wanawake wa kileo kuolewa sio issue tena kwao -- kuolewa ni kama jambo la kawaida tu, wala sio tena jambo la heshima kama ilivyokuwa zamani. Wanawake wanaohitaji ndoa ni wachache kuliko wasiohitaji, hapa utaona kabisa suala la kuoa ni changamoto kubwa sana kwa sisi vijana wa kiume, vijana wa kileo. Muda unakimbia sana na umri haurudi nyuma unakwenda tu, kuna wakati fulani nilikuwa najiuliza hili tatizo ninalo mimi tu!? Aisee kumbe sipo peke yangu.
Sio peke tako mko wengi sana.
 
"Ninao wapenda hawanipendi" utakuwa mtu wa misifa sana..wanawake wastaarabu hawapendi watu wa hivyo...katazame movie Coming to America ..ukijishusha warembo wananasa kiulaini..ukijipandisha utawanasa wachunaji tu...
Umeongea kitu kikubwa sana, hii inaaply pande zote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom