Nimefika Kigoma Hii Leo; Ni Yepi Ya Kuyaangalia Ukiwa Kigoma? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimefika Kigoma Hii Leo; Ni Yepi Ya Kuyaangalia Ukiwa Kigoma?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, May 20, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  [h=6]Ndugu zangu,[/h] [h=6]Nimefurahi sana kufika tena Kigoma kwa mara ya pili. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2006. Kuna mabadiliko chanya nimeyaona. Naamini, kuna ya kuyaangalia unapokuwa Kigoma. Ni yepi hayo? Mwenye kuijua zaidi Kigoma anijuze.

  Na kabla sijasema mengi, ngoja kwanza nifike kwenye vijiwe vya wenyeji. Huko nipata picha ya kinachoendelea Kigoma Mjini na pembezoni. Hata mitazamo ya wenyeji juu ya wawakilishi wao; akina Zitto, Serukamba, Sabrina Sungura, Kafulila, Machali na wengineo. Inasemwa pia, mgeni huona, kile ambacho mwenyeji hakioni. Hivyo hivyo, husikia kile ambacho mwenyeji hakisikii.

  Naam, Kigoma ina historia ya siasa. Hapa watu wanachambua siasa. Bila shaka , kuna nitakayojifunza. Nitawamegea pia.[/h] Angalia picha za Kigoma kwenye;Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo

  [h=6]Maggid,[/h] [h=6]Kigoma. [/h]0788 111 765
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,642
  Likes Received: 3,019
  Trophy Points: 280
  Safi sana M/kiti...ningekuwepo Kg ningekutembeza...sema niko kikazi Dar, narud mwez ujao...Ila fanya kila linalowezekana nenda Kigoma kask...ususani Kijiji cha Nyurubanda,Mkigo,usikie watu wanavyo lalamiko..nitakupigia tuongee vizuri..usikose kwenda ujiji
   
 3. m

  muhinda JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 340
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  yaani kigoma is such a beutiful place, mimi nilishangaa sana nilipofika hapo mara yangu ya kwanza, maana mawazo yangu nilikuwa nafikiria vinginevyo kabisa. Watanzania tujenge utamaduni wa kutembelea mikoa mbalimbali, tutapanua mawazo na kujifunza mengi. Kigoma is so peaceful and naturally beautiful
   
 4. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  anzia hapo website bar utakutana na wafanyakazi wa kila idara hapo kigoma
  shuka chini pale nenda sandra utamkuta bwana mmoja anitwa Mrefu atakupa
  kila kinachojiri kigoma,then tanganyika hotel then pitia gerezani pale kuna discko la mchana kandoni mwa ziwa
  bila kusahau usiogolee bila kupata kibali cha wazee wa huko.
  usisahau kwenda kibirizi pia(sea breaze) kutizama machweo ya jua
  ukitaka usirudi iringa usimchekee binti pale mwanga, ujiji au mwandiga
  kwa jinsi walivo utatelekeza familia yako.
   
 5. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  usisahau kunywa maji safi ya Nyakageni
   
 6. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Maggid, angalia totoz za ukweli hapo kg, tuletee picha hapa nasisi tufaidi hata kwa macho tu.
   
 7. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Mkuu nenda Kibirizi ukaone bandari ndogo ya kusafirisha bidhaa kwenda DRC na Burundi. Pia muda wa jioni nenda kabarizi upepo mwanana pale Lake Tanganyika Beach Hotel. Ukiwa hapo utaona mandhari nzuri ya ziwa na milima ya DRC. Kama haujachoka, subiri muda usiku kidogo uone mabadiliko katika ziwa. Utashuhudia mji mzuri sana ziwani wenye umeme usiokatika. Hao ni wavuvi wanavua dagaa kwa kutumia vipe! Siku ya pili nenda Ujiji. Huko unaweza kufananisha na Bagamoyo, Mafia, Kilwa Kivinje na Mikindani, Mtwara. Hiyo ni sehemu ya biashara ya utumwa. utaona pia makumbusho ya Dr. David Livingstone! Siku ya tatu pata usafiri wa boti la TANAPA ili ukaone Sokwe mtu huko Hifadhi ya Gombe. MKUU UMEME UMEKATIKA NITAKUJUZA UKIRUDI!
   
 8. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna jamaa anaitwa Jack anatengeneza ugari saafi na samaki wa kigoma yupo kwenye njia yakwenda mwanga.

  mida ya saa tisa au kumi nenda Bangwe beach pale utapata vinywaji saafi kisha unaweza piga mbizi bila shida.
   
 9. pgasper

  pgasper JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 311
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanzania yangu Dunia yangu
   
 10. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  huwa tunaambiwa kigoma mwisho wa reli,je umeshahakikisha kuwa kweli reli imishia kigoma?hahaha!
   
 11. mwandiga

  mwandiga JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Karibu mkuu, japo haujasema ungependelea vitu gani lakini Mida ya jioni kuanzia kumi na mbili na nusu nenda mwanga utafurahi, usiache kwenda mambo hadharani maweni, disco kibo, ujiji tembea kwa mguu sio ndani ya gari, kisha nenda Manyovu mpakani mwa Burundi na tz kisha kasulu na kibondo
   
Loading...