falcon mombasa
JF-Expert Member
- Mar 5, 2015
- 9,186
- 9,287
wakuu habari za jioni. mimi nikiwa kama mmoja wa watu wanaopenda mabadiliko nimeshindwa kuvumilia kuwa mbali na sehemu unakofanyika uchaguzi wa kihistoria kwenye tasnia ya sheria Tanzania. hivyo kwa moyo mmoja nimeamua kuja arusha na muda huu ndio nimefika, watu wanaonekana kuwa na morale kubwa ya kisiasa hapa arusha huku majina ya lema na lissu yakiwa hametawala vinywani mwa watu. tetesi nilizozipata ni kuwa eneo litakaloluzunguka ukumbi wa uchaguzi ulinzi umeimarishwa mno. tuwe pamoja nitawapa kila wanachosema watu wa arusha juu ya uchaguzi huu. pia kama kuna wanajf hapa arusha tutafutane jameni