Nimefanikiwa kupambana na kunguni na kuwapunguza kwa kiasi kikubwa sana

Simba Forever

JF-Expert Member
May 4, 2021
886
1,000
Kunguni wanakera sana, unakosa usingizi wakati mwingine unadhalilika!

Basi bwana kuna hii dawa inaitwa diazinone, niliitumia mwaka 2015 na nikafanikiwa kuwaangamiza hawa wadudu korofi.

Ghafla tena naitwa nyumbani kwamba wadudu wanasumbua, njoo utupe msaada, nikaenda kweli nikakuta wamejaa kwenye neti, godoro mpaka kitandani, hadi watoto wamehamishiwa vyumba vingine.

IMG_20210910_092310_384.jpg
IMG_20210910_092519_207.jpg


Nilivyoona hii hali basi nikaingia mjini na sh elfu 10 tu nikiwa na uhakika hii inamaliza kila kitu.

Kweli, nikapata dawa chupa 1 sh elfu 2.5 nikachukua 2 kwa elfu 5.

Chupa ya spray nikabeba kwa elfu 4.

IMG_20210910_092914_727.jpg


Chupa 1 unachanganya na lita 2 za maji safi.

IMG_20210910_100015_943.jpg


Kisha unakoroga vizuri (hakikisha kama unaweza uvae gloves, barakoa kuoa suffocation, PPE ni muhimu maana hii ni sumu hatari sana)

Nikachanganya dawa vizuri na maji mpaka ikawa kama maziwa

IMG_20210910_100246_454.jpg


Baada ya hapo nikaweka kwenye chupa nikaanza spray, vitu vyote lazima viwe katika sehemu ya wazi yenye hewa na mwanga wa kutosha ili mdudu aonekane vizuri na kuepuka suffocation.

Kusema kweli hii dawa ilileta matokeo mazuri sana mpaka sasa wadudu wamepungua kwa asilimia 90
 

Simba Forever

JF-Expert Member
May 4, 2021
886
1,000
Japo imekaa kama tangazo la biashara ila asante sana mkuu, kizuri mgawie jirani yako.... Mkuu ungesema uko sehemu gani maana kunguni wa Mwanza hawasikii sumu yoyote!
Huku MWanza Kunguni ni janga kuu la Mkoa! Ngoja tu
Kaka hii sio tangazo, its real hapo ni nyumbani kwa bro.

hio dawa nilishauriwa na daktari wa mifugo miaka 6 iliyopita. Ikanisaidia sana mpaka leo imenisaidia

nipo mwanza, IGOMA!
 

darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
6,009
2,000
Wakati niko hostel nilikuwa natumia dawa ya kupiga kwenye vyandarua maarufu kama NGAO. Ile ilikuwa kiboko. Inaua kunguni taratibu. Ndani ya wiki hakuna kunguni Wala Mtoto wa kunguni.

Sijui imeenda wapi,siku hizi haipo madukani!
 

Dumas the terrible

JF-Expert Member
Jan 20, 2021
1,299
2,000
Kunguni hawangalii masikini wala tajiri.
prado hizo ziko 2. noah 2. Amarok 1. Pick up 1, Terrano 1, Pikipiki XL 250 iko 1.

vikorokoro ni vingi ndio maana wadudu wanaingia bila taarifa
mpo uchumi wa kati aisee pongezi ziende kwa awamu ya tano
Anyway nilikua suwajui kunguni mbaka siku nilipokua Huko Unguja Zanzibar kwenye Bungalow za Hotel moja ya huko Nungwi aaaah aisee wale wadudu ni kijiji wanauma na hata hawasikii dawa yani!
 

pamjela

JF-Expert Member
Jun 18, 2016
374
1,000
Hivi kunguni mpaka leo wapo kweli, hawa si wanaletwa na tabia ya uchafu!
kunguni sio uchafu mzee hawa wadudu hawana adabu tu
nakumbuka mwaka fulani MAREKANI kunguni lilikuwa JANGA kubwa kwao mpk likajadiliwa kwenye BUNGE nakumbuka kipindi hicho RAISI alikuwa OBAMA
hoja ilikuwa KUNGUNI wao dawa zote zimegonga mwamba na wanekuwa wengi mno

HUKO uganda JESHI la KULINDA nchi liliingilia kati na kuchukua OPERESHENI maalum ya kuwa tokomeza Baada ya wananchi kuomba msaada zaidi toka serikalini


hawa wanajeshi wanaweza kukaa kimya mwaka mzima tena bila hata ya kula
wakiwa wanafanya tafiti zao katika maabara kutengeneza chanjo zao kukabiliana na madawa mbalimbali

na dawa ikiwa kali sana kwao inawaua
wanachukua sample na kuisambaza katika maabara zao dunia nzima na kuifanyia uchunguzi mpk wanapata SOLUTION
ndio ile unakuta wametulia hata mwaka mzima lkn ghafla wanaibuka tena na ukitumia hiyo dawa tena haiwadhuru kumbe wajomba washaifanyia utafiti na kupata ANTDOTE yake

hawa wadudu inahitajika kampeni ya mwakamzima wewe ukisikia dawa yoyote unawapelekea moto tu hata kma unaona wameisha inakupaswa kila baada ya wiki 2 au mwenzi unapuliza dawa tofauti tofauti
 

G bznes

JF-Expert Member
Jul 19, 2014
903
1,000
Suluhisho pekee la Kunguni ni Maji ya Moto. Chemsha Maji yapate Moto kwa kiwango cha Juu kabisa halafu kamwagie Sehemu zote zenye Mazalia yao. Fua vitu vyote halaf anika Juani baada ya hapo kunguni utawasikia kwa wengine
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom